TUESDAT 07/03/2017

 

 

 

Kituo cha Mafuta Tegeta Jijini Dar Chateketea Kwa Moto 


SeeBait

Kituo cha mafuta kilichopo eneo la Tegeta Azania jijini Dar as Salaam kineteketea kwa moto.Chanzo cha ajali hiyo ni gari lililokuwa likishusha shehena ya mafuta kushika moto.


Mrisho Mpoto awataka wananchi kuangalia utendaji kazi wa Makonda na siyo vyeti Vyake

Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto ameamua kumkingia kifua RC Makonda ambaye kwa siku za karibuni amekuwa aki-trend kwenye mitandao ya kijamii akituhumiwa kufoji vyeti.

Mpoto amedai anashangaa kuona hata wale ambao walikuwa wanamsupport na kumsifia mkuu huyo wameshinndwa kufungua midomo yao.

“Hii nchi ya ajabu sana ukifanya vizuri lazima upate maadui mpaka wakushushe, ndiyo waanze kumpansisha mwingine. Wako wapi waliosema Makonda songa mbele usirudi nyuma? mko wapi mliomuita Makonda shujaa mkombozi wa Wa watoto wetu, leo kila mtu anamruka na kuona hakuna alichofanya This is not Fair at all,” alianidika Mpoto Instagram.

“Angalieni utendaji wake Wa kazi na siyo vyeti vyake guys!! Songa Songa Songa Makonda kama ulivyosema hii vita siyo ndogo na ina wanafiki wengi. @paulmakonda @paulmakonda unawaona waleeeeeee ndiyo siyo watu wazuri kabisa!!,” aliongeza Mpoto.

Mkuu huyo hivi karibuni alidai hayo yote yamezalishwa kutokana na vita yake dhidi ya madawa ya kulevya ambayo umezaa matunda kwa kiasi kikubwa.
 
 

Sasa Ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji


SeeBait

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Ian Ferrao
**
Kampuni ya simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania itakuwa kampuni ya kwanza inayotoa huduma za mawasiliano kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam maarufu kama “DSE”. 
Hii inafuatia rasimu ya waraka wa matarajio (Prospectus) na maombi yaliyotumwa kwenye Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kukubaliwa.  CMSA ndiyo mamlaka inayosimamia masoko ya mitaji na dhamana nchini.
 
Uuzaji wa hisa za awali wa Vodacom Tanzania Limited PLC ni katika utekelezaji wa Sheria ya Posta na Mawasiliano iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha mwaka 2016 ambayo inaagiza kampuni zote za simu za mikononi kuuza 25% ya hisa zao kwa umma.
 
Hisa za kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi zaidi nchini, huenda sasa zikaanza kuuzwa muda wowote kuanzia wiki hii au wiki ijayo. 
Vodacom Tanzania inatarajia kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika soko la mitaji ambayo ni sawa ni hisa milioni 560 zitakazokuwa na thamani ya shilingi bilioni 476 huku kila hisa ikiuzwa kwa Tsh 850. 
 
Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom Tanzania ikizingatiwa kwamba kampuni nyingine za simu zinasuasua. Vodacom inatarajiwa kuwa miongoni mwa kampuni zitakazokuwa na mitaji mikubwa katika soko la DSE. 
Kampuni nyingine zenye mitaji mikubwa ni Acacia, EABL na TBL. Hadi hivi sasa DSE ina kampuni 25 zilizoorodheshwa ambapo kampuni za ndani ni 18 na zile zilizoorodheshwa kutoka masoko ya kigeni yakiwemo London na Nairobi ni 7.
 
Taarifa rasmi za mauzo ya awali ya hisa hizo milioni 560 lini zitaanza kuuzwa, na wawekezaji gani watakidhi vigezo zitatangazwa hivi karibuni. Tutazidi kukuletea taarifa hizi za uwekezaji kwa makampuni ya simu nchini. 
 
 

Lipumba Amtumbua Maalim Seif......Amteua Magdalena Sakaya Kukaimu Nafasi ya Katibu Mkuu CUF


SeeBait

Mgogoro wa Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake kwenda Ofisi kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne

Prof. Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho, amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao Makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho

Aidha, Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kimekumbwa na Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF bara na CUF Zanzibar.
 

Wanafunzi Wapingwa Mabomu ya Machozi Wakati Wakiandamana Kupinga Mwalimu Wao Kuhamishwa



Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Bariadi mkoani  Simiyu, jana liliwapiga mabomu ya machozi wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi waliokuwa wakiandamana kupinga Mkuu wa Shule yao, Deus Toga, kuhamishwa.

Wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika saa 6.00 mchana wanafunzi hao wapatao 600, walifunga barabara kuu ya Bariadi – Lamadi.

Pia, shughuli mbalimbali za  jamii mjini Bariadi zilisimama kwa zaidi ya saa mbili kwa kuwa hakukuwa na utulivu.

Taarifa zilizopatikana zinasema   wanafunzi hao waliandamana wakipinga Mwalimu Toga kuhamishiwa katika Shule ya Sekondari Giriku.

Kabla ya wanafunzi hao hawajapigwa mabomu hayo, walianza kuandamana kuelekea ofisi ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Merkzedek Humbe, ambaye ndiye aliyemhamisha Mwalimu Toga.

Wakati wakielekea ofisini kwa mkurugenzi huyo, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliwadhibiti kabla hawajafika walikokuwa wakielekea.

Taarifa zinasema   walipozuiwa kuelekea ofisini kwa mkurugenzi, walibadili mwelekeo na kuelekea ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili wakapeleke malalamiko yao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wanafunzi hao walisambaratishwa na askari hao baada ya kufika jirani na Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu iliyoko Somanda.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao wa kidato cha kwanza hadi cha sita, walilazimika kutanda katikati ya barabara ya Bariadi – Lamadi.

Wakiwa barabarani hapo, walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kutomtaka Mkuu mpya wa Shule yao, Paul Lutema, aliyepelekwa  kushika nafasi ya Mwalimu Toga.

Pamoja na nyimbo hizo, walikuwa pia wamebeba mabango mbalimbali yenye ujumbe tofauti yakiwamo yaliyosema ‘mlimleta kuinua elimu shuleni kwetu mnamuondoa’, ‘D.E. O’ ni jipu na mengine yalisomeka ‘tunamtaka mkuu wetu Toga’.

Baada ya kukaa kwa muda barabarani hapo, walianza kuwarushia mawe polisi waliokuwa wamewazunguka wasielekee ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Polisi hao walipozidi kupigwa mawe, walilazimika kujibu mapigo kwa kuwarushia mabomu ya machozi   kuwatawanya wanafunzi hao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakutaka jina lake litajwe , alisema walifikia uamuzi huo baada ya kutangaziwa na mwalimu wao wa zamu kwamba Mwalimu Toga, alikuwa amehamishwa.

“Baada ya kutangaziwa hivyo, tuligoma kuingia madarasani na kuamua kuandamana kwenda ofisini kwa mkurugenzi na ofisi ya mkuu wa mkoa kutaka mwalimu wetu arudishwe kwa sababu ni mchapa kazi.

“Wanafunzi wanamtaka Mwalimu Toga kwa sababu tangu afike shuleni kwetu, ufaulu umeongezeka na migogoro ya shule iliyokuwapo imekwisha.

“Hata duka la shule lililokuwa limefungwa kutokana na migogoro ya walimu, limefunguliwa, ndiyo maana wanafunzi wanamtaka mwalimu huyo,” alisema mwanafunzi huyo.

Kutokana na hali ilivyokuwa, Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga na Ofisa Elimu wa Mkoa, Julius Nestory, walifika  shuleni hapo kuwatuliza wanafunzi kwa kuzungumza nao.

“Kaimu mkuu wa mkoa aliwasihi wanafunzi warejee madarasani kuendelea na masomo kwa kuwa madai yao ya kumtaka Mwalimu Toga yalikuwa yamekubaliwa.

“Lakini ofisa elimu alisema ofisi ya mkurugenzi ilimhamisha Mwalimu Toga kwa makosa kwa sababu haikuzingatia sheria na taratibu za uhamisho kwa sababu mwenye mamlaka ya kuwahamisha wakuu wa shule ni Katibu Tawala wa Mkoa.

“Ofisi ya katibu tawala wa mkoa na ofisi yangu ya elimu, hatukuwa na taarifa za uhamisho huu. Kwa hiyo, tumeamua kuutengua na tunawataka viongozi wenzangu wasifanye uamuzi bila kufuata utaratibu na sheria,”alisema ofisa elimu huyo.

Mwalimu Toga alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo  alikataa kusema chochote ingawa alionyesha kushangazwa na uamuzi huo wa wanafunzi.

“Naomba nisizungumze lolote kwa sababu hata mimi nashangaa kusikia haya. Yaani sielewi ni nini kimesababisha yote haya mpaka wanafunzi kufikia uamuzi huu, niacheni,” alisema Mwalimu Toga.
 

TADB, BODI YA NYAMA KUWAWEZESHA WADAU WA UFUGAJI WA NG’OMBE

1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia) akiwakaribisha maafisa kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017. Kushoto ni Afisa Masoko na Utafiti, Bw. Nicholai Chiweka na Afisa Sheria, Bw. Praisegod Lukio (katikati).
2
Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (aliyeinama) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipomtembelea TADB. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto), Afisa Sheria wa TMB, Bw. Praisegod Lukio (wa pili kushoto). Kulia ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John.
3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza na maafisa kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Afisa Sheria, Bw. Praisegod Lukio (wa pili kushoto) na Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (wa pili kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017. Kulia ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John.
4
Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (kulia) akizungumza wakati walipomtembelea Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB (hayupo pichani) kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017.

AFRICA: GE PARTNERS WITH THE TONY ELUMELU FOUNDATION ON LAGOS GARAGE

MAANDALIZI YA TANZANIA DAY 2017 DALLAS TEXAS

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI KUJADILI MASUALA YA USALAMA NA MAENDELEO KWA MASHIRIKA NA VIKUNDI VYA KIJAAMII

KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI TFF

MANISPAA YA UBUNGO YABAINISHA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.
 
                                                                                      Na Mathias Canal, Dar es salaam
 
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi wake.
Mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa (BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa.
 
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.
 
Alisema kuwa Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.
 
 
 
TUESDAT 07/03/2017 TUESDAT 07/03/2017 Reviewed by RICH VOICE on Machi 07, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...