Thursday, June 29, 2017

 

Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amtoa Machozi Rais Magufuli......Ni Baada ya Kufariki Ghafla Akiwa Ofisini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa benki ya AFDB Dkt Tonia Kandiero kilichotokea usiku wa jana, na kusema kwamba ni mtu aliyechangia maendeleo Tanzania.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo za rambirambi kwa Rais wa benki hiyo Akinwumi Adesina na kusema kuwa Dkt Tonia atamkumbuka kama hodari na mchapakazi katika kipindi cha uhai wake na kwamba kwa kushirikiana kwao kulifanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa iliyokuwa chini ya ufadhili wa AFNB.

Kifo cha Dkt Tonia kimetokea usiku wa jana Juni 28 alipokuwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika kusini.
==>Hapo chini ni taarifa ya IKULU 

Rais Mgufuli Akutana na Wataalam Wa Umeme Ehiopia .......Wazungumzia Uzalishaji wa Megawati 2, 100 za Umeme katika Maporomoko ya mto Rufiji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  jana  tarehe 28 Juni, 2017 amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli alisema timu hiyo inayoongozwa na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele imekuja nchini kubadilishana uzoefu na timu ya wataalamu wa Tanzania ambayo inasimamia utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project).

Katika mazungumzo na timu hiyo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli alielezea nia yake ya kuhakikisha mawazo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka maporomoko ya mto Rufiji, yanatekelezwa haraka iwezekanavyo.

“Sasa hivi nchi yetu inazalisha megawatts 1,450 tu, lakini Stiegler’s Gorge itatuzalishia megawatts 2,100 umeme huo ni mwingi na utatusaidia katika viwanda, hivyo Serikali tumeamua kutekeleza mradi huu.

“Najua kutaanza kutokea vipingamizi mbalimbali, lakini naomba Watanzania tuwe na sauti moja, eneo litakalotumia ni Kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na asilimia 3 tu ya eneo lote la hifadhi ya Selous yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 45,000” alisema Mhe. Rais Magufuli na kuongeza kuwa mradi huo utakuwa na faida nyingi zikiwemo uvuvi, maji kwa ajili ya wanyamapori na kilimo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele alisema Ethiopia ambayo kwa sasa inazalisha megawatts 4,300 za umeme kwa kutumia maji, inayo miradi mingi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji ambayo itaiwezesha kufikia uzalishaji wa megawatts 17,000 ifikapo mwaka 2020 na kwamba yeye na watalaamu wa nchi wapo tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Dkt. Medard Kalemani na timu ya wataalamu wa Tanzania wanaosimamia utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project).
 
 
 

Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza

Na Veronica  Martine, Mwanza
 Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.

“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya zamani,” walisema Wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.

Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.

Thursday, June 29, 2017 Thursday, June 29, 2017 Reviewed by RICH VOICE on Juni 29, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...