Monday, July 17, 2017
TFF Yamwachia Huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuachia
huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara kuendelea
na majukumu yake kama kawaida.
Hayo yameweka wazi na Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Abasi Tarimba katika mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo.
Manara
alifungiwa na Shirikisho hilo baada ya kubainika utovu wa nidhamu wa
kutoa matamshi yasiyo na staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya
uongozi wa mchezo huo ambapo alihukumiwa muda wa miezi 12 na kutakiwa
kulipa faini ya shilingi milioni tisa adhabu iliyotolewa na Makamu
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome.
Reviewed by RICH VOICE
on
Julai 17, 2017
Rating:
Hakuna maoni