HABARI ZA JUMAMOSI HII TAREHE 11/02/2017


.

 

 

 

 

.Saturday, February 11, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya February 11

Exim Bank Ad

Friday, February 10, 2017

Yusuf Manj na Askofu Gwajima Kuendelea Kusota Selo.....Sirro Asema Upelelezi Bado Unaendelea Exim Bank Ad

Kamanda Sirro amesema  bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.

Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.

Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .

Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.
 
 

Freeman Mbowe Kagoma kwenda Polisi Kuitikia Wito wa Makonda......Kasema Lazima Amshitaki Kwa Kumchafulia Jina

 
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.

Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.

Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.

Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa. 
Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.

Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.

Wakati huo huo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Hai,  Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge kutoka Bunge la Ulaya, David Martin, Gerrard Quille, Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Roeland Van De Beer  na Waziri Kivuli wa Mambo  ya Nje, Afrika Mashariki na Kikanda,Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, mjini Dodoma leo Ijumaa 10/02/2017.

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

Agizo wa Rais Magufuli uwanja wa ndege Dar laanza kutekelezwa

Shughuli za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017 zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08 Februari, 2017.

Wafanyakazi 850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.

Pia, timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.

Mkandarasi ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za ujenzi kuendelea.

Katika ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa dosari na kuahidi kuchukua hatua.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa ujenzi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Zitto Kabwe amkingia kifua Mbowe....Msikilize Hapa Akiongea

Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amemkingia kifua Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kusema kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha na dawa za kuleva kwa namna yoyote

Zitto ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano wake na wanahabari leo mjini Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni sawa na kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.

Amesema kuichafua CHADEMA ni sawa na kuuchafua upinzani hivyo na yeye hawezi kukaa kimya kuona upinzani ukishambuliwa, na ndiyo sababu ya kuongeza nguvu kwa kuungana naye. 
 

Rais Magufuli ateua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya

Anaswa na mzigo wa dawa za kulevya chumbani..... RPC Mwanza asimulia Sakata Zima

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha pinchi 240 na ndonga mbili.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43,  amekamatwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza

Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni  mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na  tuhuma hizo.

Aidha wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.

Tukio lilivyokuwa
Askari walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo maarufu kama pichi.

Wakati askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi.

Aidha askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi YA askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo.

Msangi amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje walikwenda kuvunja bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na kuweka kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku nyingine zikibebwa na maji .

 Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya kulevya.
HABARI ZA JUMAMOSI HII TAREHE 11/02/2017 HABARI ZA JUMAMOSI HII TAREHE 11/02/2017 Reviewed by RICH VOICE on Februari 10, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...