JUMATANO 01/02/2017

...

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA KUTOKA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, ALIKOHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA (AU)

TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA

HISTORIC COMMITMENT FROM AFRICAN HEADS OF STATE TO ADVANCE IMMUNIZATION IN AFRICA

MGODI WA BUZWAGI WALIPA KODI ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo.
Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu tawala wa wilaya Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.


PRESS RELEASE

CUF YA PROFESA LIPUMBA YAJIBU MAPIGO KUHUSU RUZUKU WALIYOPEWA NA HAZINA

Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam leo kuhusu ruzuku ya chama hicho iliyopokelewa kupitia akaunti namba 2072300456 ya Benki ya NMB Tawi la Temeke. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar na Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud.
Meza Kuu. Kutoka kulia ni Kamanda Mkuu, Athumani Hamadi,Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima, Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Masha Amour.
                                                                     Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
                                                                                                                 TAARIFA KWA UMMA 
The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) chini ya Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kinaishukuru na kuipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kukipatia Chama chetu Ruzuku yake inayopatikana kwa Mujibu wa Sheria ya vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992.

Pamoja na Ruzuku ya CUF kuzuiwa kwa Muda wa miezi mine (4) kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi Desemba 2016 kutokana na sintofahamu ya uongozi wa Kitaifa wa CUF, Msajili hakuona haja ya kuendelea kuizuia wakati shughuli za chama zinafanyika kila siku. Kuendelea kuizuia Ruzuku halali ya chama ni kukizuia kufanya kazi zake halali za kisiasa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika chaguzi mbali mbali za kiserikali zinazoendelea nchini.

Waheshimiwa wanahabari, Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia katiba ya CUF ya mwaka 1992, Toleo la 2014 alijiridhisha kuwa Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ndiye Mwenyekiti halali wa CUF kwa kuwa mchakato wa kukamilisha kujiuzulu kwake haukukamilika kabla yeye kutengua barua yake ya kujiuzulu.

Mnamo Tarehe 23 Septemba 2016 , Msajili aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa CUF kumjulisha msimamo na mwongozo wa wake kuwa “Mwenyekiti wa Taifa wa CUF ni Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba”


MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya Upandaji MitiKimkoa .

Na Emanuel Madafa,Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.

Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.

Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa mazingira katika maeneo yot.

"Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala.

Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku.

"Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema .

Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Mwisho

Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017
Afisa habari na Mawasiliano Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)akichukua matukio katika tukio hilo la kilele cha upandaji miti kimkoa katika safu ya Mlima Mbeya Itagano.

Wednesday, February 1, 2017

Breaking News: Mtokeo ya Kidato cha Nne 2016 Yametoka......Bofya Hapa Kuyatazama

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.


Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali

Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara

********
==>>Bofya  <<HAPA>  Kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne

Wednesday, February 1, 2017

Bunge Lapitisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016.

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua ya kujadiliwa na Bunge tukufu.

Aliendelea kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na Madai kwa mahitaji.

Aidha utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.

“Kumekuwepo na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua Dkt. Mwakyembe.

Vile vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya Jinai).

Kwa upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa Kisheria.

Aidha, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili kuwa Sheria.
 

Wednesday, February 1, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya February 1

Wednesday, February 1, 2017

Mafuriko ya Mvua yabomoa nyumba na Kuua Watu Wanne Mpwapwa- Dodoma

Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Hata hivyo, viongozi mbalimbali wametoa takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema watu wanane walikuwa wameripotiwa kufariki dunia na kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilikuwa inajiandaa kwenda eneo la tukio ili kujionea uharibifu uliotokea.

Lakini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema taarifa alizonazo ni za watu watatu waliopoteza maisha na kwamba bado hajapata taarifa sahihi za tukio ambalo lilitokea katika vijiji vya Mang’angu na Chinyika katika Kata ya Ving’awe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mmoja wa manusura, Beka Mlami (10) alisema walikuwa wamelala wakiwa watano katika nyumba yao mvua kubwa ilipoanza kunyesha kuanzia saa tatu usiku na ilipofika usiku wa manane nyumba yao iliyojengwa kwa udongo ilisombwa na maji.

Mbali na yeye, wengine waliokuwa katika nyumba hiyo ni Martha Sumisumi (60), Shukuru Donald (15) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mwanakianga, Bernadetha Sumisumi (9) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ilolo na Joseph Sumisumi (12) ambaye alinusurika.

Beka alisema baada ya kuona maji yameingia ndani, aliwaambia ndugu zake wakimbie watoke nje na wakati wanajiandaa kuvaa nguo nyumba yao ilianguka na kuwaponda, lakini yeye alifanikiwa kutoka na kupanda juu ya bati.

Alisema baada ya kutoka nje ndipo gogo kubwa la mti lililosombwa na maji lilipopiga nyumba yao na kuanguka chini hivyo ndugu zake wengine kushindwa kutoka na hivyo kusombwa na maji.

Alisema baada ya kutoka nje alimwona ndugu yake mwingine Joseph akiwa anapelekwa na maji, lakini alifanikiwa kujiokoa.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Steven Noel alisema nyumba iliyosombwa na maji ilikuwa imejengwa karibu na korongo la maji, hivyo baada ya mvua kunyesha, maji yaliacha mkondo wake na kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa hayo.

“Mvua ilisababisha mafuriko makubwa ambayo yalikuwa yamebeba na magogo makubwa ambayo yaliipiga ile nyumba na kuivunja katikati,” alisema Noel.

Alisema baada ya gogo la mti kuipiga nyumba hiyo, maji yalijaa ndani na kwa kuwa milango ilikuwa imefungwa, yalikosa njia ya kutokea na kuiangusha.

Noel alisema kulipopambazuka, walifukua na kuipata miili ya watu hao watatu huku mwili mwingine wa Jesca Lubeleje (19) mkazi wa Kijiji cha Chinyika ukiokotwa.

JUMATANO 01/02/2017 JUMATANO 01/02/2017 Reviewed by RICH VOICE on Februari 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...