Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito


Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .

Radio na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekua akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.

Mwanamke huyo alikua akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka.

Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.

Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano.

Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito Reviewed by RICH VOICE on Mei 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...