Trump asema itakuwa 'raha' kushindana na Oprah Winfrey 2020

Oprah Winfery kushoto na Donald Trump kulia
Image captionOprah Winfery kushoto na Donald Trump kulia
Rais Donald Trump anasema kuwa ''itakuwa furaha'' kutetea wadhfa wake wa urais dhidi ya aliyekuwa nyota wa kipindi cha mazungumzo nchini Marekani Oprah Winfrey huku kukiwa na wito wa yeye kuzindua kampeni ya kuwania urais.
''Ndio nitamshinda Oprah'', bwana Trump aliwaambia maripota wakati wa mkutano kujadili mabadiliko ya sheria za uhamiaji na maseneta wa Marekani.
Mwanawe wa kike Ivanka Trump alijiunga na raia wengine wa taifa hilo kusifu hotuba ya Oprah wakati wa tuyo za Golden Globe.
Mwandani wa Winfrey anasema muigizaji huyo 'havutiwi' na uwezekano wa kutangaza kuwania urais 2020.
Hotuba yake kuhusu umuhimu wa kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia ilivutia pongezi kutoka kila eneo la Marekani.
Bwana Trump alisema wakati wa mkutano wake siku ya Jumanne kwamba kampeni dhidi ya bi Winfrey itakuwa ya kufurahisha sana.
Aliongezea: Nilishiriki miongoni mwa vipindi vyake vya mwisho.
Alikuwa na Trump na familia yake. Nampenda sana Oprah lakini sidhani kwamba atawania urais.Nilimjua sana, aliongezea.
Miongo miwili iliopita katika CNN, bwana Trump alisema kwamba iwapo atawania urais basi atamchagua bi Winfrey kuwa mgombea mwenza .''Oprah. Nampenda Oprah''.
''Oprah atakuwa chaguo langu la kwanza'', alimwambia mtangazaji Larry King mwaka 1999.
''Iwapo atawania itakuwa vyema.Ni mtu maarufu, ni mtu mwenye kipaji na mwanamke mzuri sana''.
Mwanawe wa kike wa Trump , Ivanka Trump
Image captionMwanawe wa kike wa Trump , Ivanka Trump
Mwaka 2015 - wiki moja kabla ya kutangaza kuwa atawania urais-bwana Trump alisema kuwa angependelea kumchagua bi Oprah kuwa makamu wake wa urais.
''Nadhani Oprah angekuwa bora. Ningependa kuwa na Oprah'', alisema akiongezea ''tutaibuka washindi kwa urahisi mno''.
Mwandani wa Winfrey Gayle King alisema mapema siku ya Jumanne kwamba mtangazaji huyo hawanii urais.
''Sidhani kwamba anavutiwa na wazo hilo sidhani'', bi King aliambia chombo cha habari cha CBS alfajiri.
''Najua kwamba baada ya miaka kadhaa ya kutazama kipindi cha The Oprah Winfrey, huwa una haki ya kubadili mafikira. Lakini sidhani kwamba anafikiria wazo hilo''.
Lakini mwanawe rais aliingia katika mtandao wa kijamii na kutuma ujumbe wa twitter akimuunga mkono bi Winfrey.
Ivanka Trump, ambaye amejielezea kuwa mshauri wa rais kuhusu maswala ya ajira, uwezeshaji wa kiuchumi, maendeleo ya kikazi, na biashara amefanya sera ya maswala ya wanawake kuwa swala kuu tangu alipojiunga na ikulu ya whitehuse.


Trump asema itakuwa 'raha' kushindana na Oprah Winfrey 2020 Trump asema itakuwa 'raha' kushindana na Oprah Winfrey 2020 Reviewed by RICH VOICE on Januari 10, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...