Kamanda Muliro amzungumzia mwalimu ‘aliyewapapasa’ wanafunzi wa St. Florence


Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro, ametoa ufafanuzi wa Jeshi la Polisi kuhusu Mwalimu wa Shule ya Msingi ya St Florence iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ayoub anayedaiwa kuwadharirisha kingono wanafunzi wake wa kike wanne kwa kuwaingilia huku akimpapasa mwanafunzi wake mwingine.

Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa kushirikiana na wanafunzi hao wanne wanaodaiwa kuingiliwa na ‘mwalimu Ayoub’ na uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Aidha, Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi pia linaendelea kumtafuta mtuhumiwa anayedaiwa kukimbia baada ya taarifa za tukio hili kusambaa na kwamba hajaripoti shuleni hapo tangu Mei 24 mwaka huu.

Jana, Wabunge waliihoji Serikali kuhusu hatua gani imechukua baada ya kuwepo kwa taarifa za mwalimu huyo kufanya kitendo hicho kichafu kwa watoto ambapo Waziri Jenister Mhagama alisema Serikali inalifanyia kazi na itaeleza Bungeni hatua gani imechukua baada ya uchunguzi kukamilika.
Kamanda Muliro amzungumzia mwalimu ‘aliyewapapasa’ wanafunzi wa St. Florence Kamanda Muliro amzungumzia mwalimu ‘aliyewapapasa’ wanafunzi wa St. Florence Reviewed by RICH VOICE on Juni 01, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...