Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi


Waziri wa Elimu Nchini Afrika Kusini, Angie Motshekga amesikitishwa na kwaya ya kundi moja la wanafunzi ambao wamekuwa wakiimba wakiwa watupu.

Amesema kuwa amesikitishwa sana baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana kama “inkciyo”.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na maadili ya tamaduni za taifa hilo hasa kwa watoto wa kike.

“Tabia hiyo mbaya sana inaenda kinyume na maadili ya tamaduni zetu, mtoto wa kike anafaa kuthaminiwa na si kufundishwa mila potofu,”amesema Waziri Motshekga

Hata hivyo, mkufunzi wa Kwaya hiyo ya wanafunzi amesema kuwa ni fahari kubwa kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa huku wasichana wakiwa watupu.
Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi Reviewed by RICH VOICE on Juni 01, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...