TUESDAT 07/03/2017
Kituo cha Mafuta Tegeta Jijini Dar Chateketea Kwa Moto
Kituo
cha mafuta kilichopo eneo la Tegeta Azania jijini Dar as Salaam
kineteketea kwa moto.Chanzo cha ajali hiyo ni gari lililokuwa likishusha
shehena ya mafuta kushika moto.
Mrisho Mpoto awataka wananchi kuangalia utendaji kazi wa Makonda na siyo vyeti Vyake
Msanii
wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto ameamua kumkingia kifua RC
Makonda ambaye kwa siku za karibuni amekuwa aki-trend kwenye mitandao ya
kijamii akituhumiwa kufoji vyeti.
Mpoto amedai anashangaa kuona hata wale ambao walikuwa wanamsupport na kumsifia mkuu huyo wameshinndwa kufungua midomo yao.
“Hii
nchi ya ajabu sana ukifanya vizuri lazima upate maadui mpaka
wakushushe, ndiyo waanze kumpansisha mwingine. Wako wapi waliosema
Makonda songa mbele usirudi nyuma? mko wapi mliomuita Makonda shujaa
mkombozi wa Wa watoto wetu, leo kila mtu anamruka na kuona hakuna
alichofanya This is not Fair at all,” alianidika Mpoto Instagram.
“Angalieni
utendaji wake Wa kazi na siyo vyeti vyake guys!! Songa Songa Songa
Makonda kama ulivyosema hii vita siyo ndogo na ina wanafiki wengi.
@paulmakonda @paulmakonda unawaona waleeeeeee ndiyo siyo watu wazuri
kabisa!!,” aliongeza Mpoto.
Mkuu
huyo hivi karibuni alidai hayo yote yamezalishwa kutokana na vita yake
dhidi ya madawa ya kulevya ambayo umezaa matunda kwa kiasi kikubwa.
Sasa Ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Ian Ferrao
**
Kampuni
ya simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania itakuwa kampuni ya kwanza
inayotoa huduma za mawasiliano kuuza hisa zake katika soko la hisa la
Dar es Salaam maarufu kama “DSE”.
Hii
inafuatia rasimu ya waraka wa matarajio (Prospectus) na maombi
yaliyotumwa kwenye Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
kukubaliwa. CMSA ndiyo mamlaka inayosimamia masoko ya mitaji na dhamana
nchini.
Uuzaji
wa hisa za awali wa Vodacom Tanzania Limited PLC ni katika utekelezaji
wa Sheria ya Posta na Mawasiliano iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya
Fedha mwaka 2016 ambayo inaagiza kampuni zote za simu za mikononi kuuza
25% ya hisa zao kwa umma.
Hisa
za kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi zaidi nchini,
huenda sasa zikaanza kuuzwa muda wowote kuanzia wiki hii au wiki ijayo.
Vodacom
Tanzania inatarajia kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika soko la
mitaji ambayo ni sawa ni hisa milioni 560 zitakazokuwa na thamani ya
shilingi bilioni 476 huku kila hisa ikiuzwa kwa Tsh 850.
Hii
ni hatua kubwa sana kwa Vodacom Tanzania ikizingatiwa kwamba kampuni
nyingine za simu zinasuasua. Vodacom inatarajiwa kuwa miongoni mwa
kampuni zitakazokuwa na mitaji mikubwa katika soko la DSE.
Kampuni
nyingine zenye mitaji mikubwa ni Acacia, EABL na TBL. Hadi hivi sasa
DSE ina kampuni 25 zilizoorodheshwa ambapo kampuni za ndani ni 18 na
zile zilizoorodheshwa kutoka masoko ya kigeni yakiwemo London na Nairobi
ni 7.
Taarifa
rasmi za mauzo ya awali ya hisa hizo milioni 560 lini zitaanza kuuzwa,
na wawekezaji gani watakidhi vigezo zitatangazwa hivi karibuni. Tutazidi
kukuletea taarifa hizi za uwekezaji kwa makampuni ya simu nchini.
Lipumba Amtumbua Maalim Seif......Amteua Magdalena Sakaya Kukaimu Nafasi ya Katibu Mkuu CUF
Mgogoro
wa Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo
Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya
Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara,
Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad
baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake kwenda Ofisi kuu
Buguruni kwa zaidi ya mara nne
Prof.
Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja
na wafuasi wa chama hicho, amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda
Makao Makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia
mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya
chama hicho
Aidha,
Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo
Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe
Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha
na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima
Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi
na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.
Chama
cha Wananchi CUF kimekumbwa na Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba
alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu
ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF bara na CUF
Zanzibar.
Wanafunzi Wapingwa Mabomu ya Machozi Wakati Wakiandamana Kupinga Mwalimu Wao Kuhamishwa
Jeshi
la Polisi katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, jana liliwapiga
mabomu ya machozi wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi waliokuwa
wakiandamana kupinga Mkuu wa Shule yao, Deus Toga, kuhamishwa.
Wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika saa 6.00 mchana wanafunzi hao wapatao 600, walifunga barabara kuu ya Bariadi – Lamadi.
Pia, shughuli mbalimbali za jamii mjini Bariadi zilisimama kwa zaidi ya saa mbili kwa kuwa hakukuwa na utulivu.
Taarifa
zilizopatikana zinasema wanafunzi hao waliandamana wakipinga Mwalimu
Toga kuhamishiwa katika Shule ya Sekondari Giriku.
Kabla
ya wanafunzi hao hawajapigwa mabomu hayo, walianza kuandamana kuelekea
ofisi ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Merkzedek
Humbe, ambaye ndiye aliyemhamisha Mwalimu Toga.
Wakati
wakielekea ofisini kwa mkurugenzi huyo, askari wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU), waliwadhibiti kabla hawajafika walikokuwa wakielekea.
Taarifa
zinasema walipozuiwa kuelekea ofisini kwa mkurugenzi, walibadili
mwelekeo na kuelekea ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili wakapeleke
malalamiko yao.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, wanafunzi hao walisambaratishwa na askari hao
baada ya kufika jirani na Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu iliyoko
Somanda.
Kutokana
na hali hiyo, wanafunzi hao wa kidato cha kwanza hadi cha sita,
walilazimika kutanda katikati ya barabara ya Bariadi – Lamadi.
Wakiwa
barabarani hapo, walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kutomtaka Mkuu
mpya wa Shule yao, Paul Lutema, aliyepelekwa kushika nafasi ya Mwalimu
Toga.
Pamoja
na nyimbo hizo, walikuwa pia wamebeba mabango mbalimbali yenye ujumbe
tofauti yakiwamo yaliyosema ‘mlimleta kuinua elimu shuleni kwetu
mnamuondoa’, ‘D.E. O’ ni jipu na mengine yalisomeka ‘tunamtaka mkuu wetu
Toga’.
Baada
ya kukaa kwa muda barabarani hapo, walianza kuwarushia mawe polisi
waliokuwa wamewazunguka wasielekee ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Simiyu.
Polisi hao walipozidi kupigwa mawe, walilazimika kujibu mapigo kwa kuwarushia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakutaka jina lake
litajwe , alisema walifikia uamuzi huo baada ya kutangaziwa na mwalimu
wao wa zamu kwamba Mwalimu Toga, alikuwa amehamishwa.
“Baada
ya kutangaziwa hivyo, tuligoma kuingia madarasani na kuamua kuandamana
kwenda ofisini kwa mkurugenzi na ofisi ya mkuu wa mkoa kutaka mwalimu
wetu arudishwe kwa sababu ni mchapa kazi.
“Wanafunzi
wanamtaka Mwalimu Toga kwa sababu tangu afike shuleni kwetu, ufaulu
umeongezeka na migogoro ya shule iliyokuwapo imekwisha.
“Hata
duka la shule lililokuwa limefungwa kutokana na migogoro ya walimu,
limefunguliwa, ndiyo maana wanafunzi wanamtaka mwalimu huyo,” alisema mwanafunzi huyo.
Kutokana
na hali ilivyokuwa, Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Festo Kiswaga na Ofisa Elimu wa Mkoa, Julius Nestory, walifika
shuleni hapo kuwatuliza wanafunzi kwa kuzungumza nao.
“Kaimu
mkuu wa mkoa aliwasihi wanafunzi warejee madarasani kuendelea na masomo
kwa kuwa madai yao ya kumtaka Mwalimu Toga yalikuwa yamekubaliwa.
“Lakini
ofisa elimu alisema ofisi ya mkurugenzi ilimhamisha Mwalimu Toga kwa
makosa kwa sababu haikuzingatia sheria na taratibu za uhamisho kwa
sababu mwenye mamlaka ya kuwahamisha wakuu wa shule ni Katibu Tawala wa
Mkoa.
“Ofisi
ya katibu tawala wa mkoa na ofisi yangu ya elimu, hatukuwa na taarifa
za uhamisho huu. Kwa hiyo, tumeamua kuutengua na tunawataka viongozi
wenzangu wasifanye uamuzi bila kufuata utaratibu na sheria,”alisema ofisa elimu huyo.
Mwalimu
Toga alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alikataa kusema chochote
ingawa alionyesha kushangazwa na uamuzi huo wa wanafunzi.
“Naomba
nisizungumze lolote kwa sababu hata mimi nashangaa kusikia haya. Yaani
sielewi ni nini kimesababisha yote haya mpaka wanafunzi kufikia uamuzi
huu, niacheni,” alisema Mwalimu Toga.
TADB, BODI YA NYAMA KUWAWEZESHA WADAU WA UFUGAJI WA NG’OMBE
MANISPAA YA UBUNGO YABAINISHA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele
ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi
wake kwa kuweka mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 –
2019/2020 ambao unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili
kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa
wananchi wake.
Mpango
huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu
wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025 ambapo Mpango mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa
(BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi
Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa.
Hayo
yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea
juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya maendeleo kwa
kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa
Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza maalumu la
madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo.
Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.
Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.
Alisema
kuwa Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza
kutoa matokeo ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi
kwa haraka katika kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa
Ubungo.
TUESDAT 07/03/2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Machi 07, 2017
Rating:
Hakuna maoni