TUESDAY 07/03/2016

  .....

 

HABARI ZA ASUBUHI MSOMAJI WANGU WA NGU , NAAMINI UMEAMKA SWALAMA NIKUKARIBISHE KATIKA  MAGAZETI HASYA UPATE KUHABARIKA ,
































 

KATIBU TAWALA IRINGA JOSEPH CHITINKA CHEZENI MPIRA ACHENI KUKAA VIJIWENI

Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
 Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
                                                                                                      Na Fredy Mgunda,Iringa.

MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.

Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka

Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.

“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema Chitinka

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.

“Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Msigwa

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo kamanda wa vijana wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya Iringa Jackson Kiswaga alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya Iringa.

“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema Kiswaga.

Mashindano ya Mbuzi Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

 

AFRICA: ORANTO PETROLEUM LAUNCHES $500 MILLION OIL EXPLORATION CAMPAIGN IN SOUTH SUDAN

RAIS MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGEVITA WA KAMBI YA NGERENGERE, MOROGORO

MAZISHI YA MAREHEMU MTONGORI MANG'ACHE YAFANYIKA TARIME MKOANI MARA.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Mchungaji Canon Yohana Chacha (katikati), akiongoza ibada ya mazishi ya Anna Mtongori Mang'ache hii leo Machi 06,2017 katika Mtaa wa Kenyamanyori, halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara.

Wengine ni Mchungaji wa Kanisa la Angilikana Parishi ya Kenyamanyori Tarime, Wyclif Chereme (kulia) pamoja na Mchungaji wa Kanisa Anglikana Parishi ya Kemange Tarime, Charles Mwita (kushoto).

Marehemu Anna Mtongori Mang'ache aliyezaliwa mwaka 1931 Kenyamanyori Tarime, alifariki dunia alihamisi iliyopita Machi 02,2017 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.

Familia ya Mang'ache inawashukuru Madaktari wote wakiwemo wa Hospitali ya Winani Tarime, CF na Bugando Jijini Mwanza, jeshi la polisi, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na marafiki kwa ushirikiano wao wa dhati katika kumuuguza marehemu Anna Mtori Mang'ache na hata katika kufanikisha mazishi yake. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!
#BMGHabari

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Mchungaji Canon Yohana Chacha (katikati), akiongoza ibada ya mazishi ya Anna Mtongori Mang'ache
Mchungaji wa Kanisa la Angilikana Parishi ya Kenyamanyori Tarime, Wyclif Chereme, akizungumza kwenye ibada ya mazishi hayo
Mwinjilisti Foredy Qojedy, akisoma maandiko ya biblia kwenye mazishi hayo wakati wa ibada

Rais Magufuli Atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za kiutendaji zinazomkabili ikiwemo uendeshaji wa shirika hilo

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amesema moja ya tuhuma zinazomkabili ni pamoja na kuingia mikataba kiholela.

Shirika la Elimu Kibaha ni Shirika la umma linalotoa huduma mbalimbali likiwa na ofisi zake Mkoa wa Pwani kilomita 40 Magharibi mwa Mji wa Dar es salaam.

Tundu Lissu Aachiwa Kwa Dhamana

Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana (ya polisi) iliyowekwa na wanasheria wawili, Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu baada ya kushikiliwa na polisi  kwa saa kadhaa leo.

Lissu alikamatwa ghafla leo alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mashitaka yake ya uchochezo katika moja ya kesi zinazomkabili, kufutwa.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lissu alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini katika jamii wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani, Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.

Baada ya mahojiano ya leo, Lissu ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.

Rais Magufuli azindua uwanja wa ndegevita wa Ngerengere

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 06 Machi, 2017 amezindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere uliopo Mkoani Morogoro, uliofanyiwa ukarabati mkubwa baada ya miundombinu ya uwanja uliojengwa tangu mwaka 1970 kuharibika.

Sherehe ya uzinduzi wa uwanja huo imefanyika uwanjani hapo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wastaafu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amesema ukarabati wa uwanja huo ulioanza tarehe 15 Julai, 2013 umegharimu Shilingi Bilioni 137 na Milioni 631 ikiwa ni ufadhili wa Serikali ya China na umehusisha kujenga upya njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 3,000 upana wa mita 45 na unene wa sentimeta 45 pamoja na maegesho ya ndege za kivita na ndege za abiria.

Jenerali Mabeyo ameongeza kuwa uwanja huo ni miongoni mwa viwanja bora zaidi duniani kwa sasa na una uwezo wa kutumiwa na ndege za aina zote zilizo chini ya Boeing 777 huku akibainisha kuwa pamoja na ndege za kivita pia unaweza kutumiwa na ndege za kawaida za abiria kwa dharula.

Nae Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing amesema kujengwa kwa uwanja huo kumeimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na China na amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuendeleza uhusiano huo.

Pamoja na kuzindua uwanja huo, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia maonesho ya ndege za kivita zilizorushwa kwa mbinu mbalimbali za kivita, kutoa heshima na kutua katika uwanja huo.

Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kazi kubwa linayofanya na pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na Serikali yake kwa msaada mkubwa iliyoutoa kujenga uwanja huo.

“Mhe. Balozi Lu Youqing naomba unipelekee shukrani zangu za dhati Mhe. Rais wa China kwa kutoa msaada huu mkubwa wa kujenga uwanja wa ndegevita wa Ngerengere, najua China imetusaidia kujenga Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki na Uwanja wa Mpira, hii yote inathibitisha uhusiano wetu mzuri, urafiki na undugu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli ameahidi kujenga barabara ya lami ya kuunganisha Kamandi ya Jeshi la anga ya Ngerengere na barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Vurugu za machinga zajeruhi watu 9 Jijini Mwanza wakiwemo mgambo wa jiji.

Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa.

Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga.

Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.

Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.

 
TUESDAY 07/03/2016 TUESDAY 07/03/2016 Reviewed by RICH VOICE on Machi 07, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...