Thursday, June 29, 2017
Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amtoa Machozi Rais Magufuli......Ni Baada ya Kufariki Ghafla Akiwa Ofisini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli amesema
amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa benki ya AFDB
Dkt Tonia Kandiero kilichotokea usiku wa jana, na kusema kwamba ni mtu
aliyechangia maendeleo Tanzania.
Rais
Magufuli ametuma salamu hizo za rambirambi kwa Rais wa benki hiyo
Akinwumi Adesina na kusema kuwa Dkt Tonia atamkumbuka kama hodari na
mchapakazi katika kipindi cha uhai wake na kwamba kwa kushirikiana kwao
kulifanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa iliyokuwa chini ya ufadhili
wa AFNB.
Kifo cha Dkt Tonia kimetokea usiku wa jana Juni 28 alipokuwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika kusini.
==>Hapo chini ni taarifa ya IKULU
Rais Mgufuli Akutana na Wataalam Wa Umeme Ehiopia .......Wazungumzia Uzalishaji wa Megawati 2, 100 za Umeme katika Maporomoko ya mto Rufiji
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana
tarehe 28 Juni, 2017 amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme
na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri
Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana
uzoefu na Tanzania.
Mhe.
Rais Magufuli alisema timu hiyo inayoongozwa na Waziri wa Maji,
Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele imekuja nchini
kubadilishana uzoefu na timu ya wataalamu wa Tanzania ambayo inasimamia
utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya
mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project).
Katika
mazungumzo na timu hiyo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mhe.
Rais Magufuli alielezea nia yake ya kuhakikisha mawazo ya Baba wa Taifa
Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya
kuzalisha umeme kutoka maporomoko ya mto Rufiji, yanatekelezwa haraka
iwezekanavyo.
“Sasa
hivi nchi yetu inazalisha megawatts 1,450 tu, lakini Stiegler’s Gorge
itatuzalishia megawatts 2,100 umeme huo ni mwingi na utatusaidia katika
viwanda, hivyo Serikali tumeamua kutekeleza mradi huu.
“Najua
kutaanza kutokea vipingamizi mbalimbali, lakini naomba Watanzania tuwe
na sauti moja, eneo litakalotumia ni Kilometa za mraba 1,350 ambalo ni
sawa na asilimia 3 tu ya eneo lote la hifadhi ya Selous yenye ukubwa wa
Kilometa za mraba 45,000” alisema Mhe. Rais Magufuli na kuongeza
kuwa mradi huo utakuwa na faida nyingi zikiwemo uvuvi, maji kwa ajili ya
wanyamapori na kilimo.
Kwa
upande wake Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt.
Seleshi Bekele alisema Ethiopia ambayo kwa sasa inazalisha megawatts
4,300 za umeme kwa kutumia maji, inayo miradi mingi ya kuzalisha umeme
kwa kutumia maji ambayo itaiwezesha kufikia uzalishaji wa megawatts
17,000 ifikapo mwaka 2020 na kwamba yeye na watalaamu wa nchi wapo
tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika masuala ya umeme na
ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme.
Mazungumzo
hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Dkt. Medard Kalemani na
timu ya wataalamu wa Tanzania wanaosimamia utekelezaji wa ujenzi wa
mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya mto Rufiji
(Stiegler’s Gorge Power Project).
Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza
Na Veronica Martine, Mwanza
Mtoto
mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la
Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja
ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.
Wakizungumzia
tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na
kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.
“Kitendo
cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini
hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya
zamani,” walisema Wananchi.
Kwa
upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea
kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa
huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.
Thursday, June 29, 2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 29, 2017
Rating:
Hakuna maoni