Tuesday, June 20, 2017 Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.
Jeshi
la Magereza limefanikiwa kumkatamata Ramadhan Nombo mkazi wa Mabibo
jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutaka kuingiza simu tano kinyume cha
sheria katika gereza la Keko wilayani Temeke.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustine Mboje jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni katika gereza hilo.
Alisema
Nombo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kuanzia 30 na kuendelea
alidakwa wakati akifanyiwa upekuzi katika eneo maalumu la ukaguzi wa
wageni mbalimbali wakiwamo wanaowatembelea ndugu na marafiki walioko
mahabusu kwenye gereza hilo.
“Huyu
(Nombo) alikuwa katika foleni ya mstari wa mwisho ya watu wanaokwenda
kuwaaona ndugu zao walioko ndani ya gereza hili. Nadhani hakujua kama
sisi kama magereza tuna vifaa vya kisasa vya ukaguzi.
“Ilipofika
zamu yake askari wetu walimfanyia ukaguzi na kabla haujaisha kifaa hiki
maalumu kiliita alamu kuashiria kuna kitu tofauti,” alisema Mboje.
Alisema
alibainika kuwa na simu hizo alizozifunga kitaalaamu na kuficha katika
mapande ya nyama yaliyopikwa kwa ustadi wa juu na kuchanganywa na viazi
aina ya mbatata.
Mkuu
huyo wa magereza, alisema tukio hilo siyo la kwanza katika gereza hilo
kwani linatokea katika magereza mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam
likiwamo la Segerea.
“Wengine
wanatumia hadi mbinu ya kuficha simu hizi katika ugali na mikate lakini
tunafanikiwa kuwakamata kutokana na uimara wa vifaa na askari wetu,”alisema Mboje
Tuesday, June 20, 2017 Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni