Updates: Idadi ya Waliofariki Dunia Baada ya Kivuko cha MV Nyerere Yafika 86


Zoezi  la ukoaji wa miili ya watu waliopoteza maisha katika Kivuko cha MV Nyerere limeanza rasmi baada ya kusimama jana usiku, ambapo Vikosi Maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na Jeshi la Zimamoto na uokoaji vinaendesha zoezi hilo.

Hadi sasa idadi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea jana tarehe 20 Septemba 2018 imeongezeka kutoka watu 44 hadi 86.

Kivuko cha MV Nyerere kilizama katika Ziwa Victori kikitokea Bugorora kisiwani Ukerewe kuelekea Kisiwa cha Ukara.

Inahofiwa kuwa, mamia ya watu waliokuwamo katika kivuko hicho wamepoteza maisha, ambapo watu 37 walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai hapo jana.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Maghembe amesema kuwa sababu ya kuzama kwa kivuko hicho inasadikika kuwa ilibeba watu zaidi ya 400 ambapo kilizidisha uwezo wake ambao ni watu 101.

Maghembe amesema kuwa imezama mita chache kabla ya kuwasili eneo la Ukara ambapo dereva alipunguza mwendo kuashiria amekaribia kutia nanga ndipo abiria wengi walihamia upande wa lango la kutokea wakiwahi kusogea ili washuke ndipo uzito ulizidi na kupinduka.

“Abiria walipoona mwendo umepunguzwa walikimbilia kuwahi mbele ya lango ili kujiandaa kushuka, ndipo uzito ukaegemea upande mmoja”, amesema Maghembe
Updates: Idadi ya Waliofariki Dunia Baada ya Kivuko cha MV Nyerere Yafika 86 Updates: Idadi ya Waliofariki Dunia Baada ya Kivuko cha MV Nyerere Yafika 86 Reviewed by RICH VOICE on Septemba 21, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...