Baraza la Seneti lanusuru shughuli za serikali kuu kufungwa nchini Marekani
Baraza la Seneti la Marekani limepitisha muswada wa matumizi ya muda wa wiki moja hatua inayozuia uwezekano wa kufungwa kwa shughuli za serikali kuu saa chache kabla ya muda wa mwisho wa bajeti ya sasa kumalizika.Masenta walipiga kura ya sauti kurefusha matumizi ya serikali kuu hadi Ijumaa inayokuja ili kutoa muda zaidi kwa Ikulu na Bunge la Marekani kufikia makubaliano kuhusu matumizi ya mwaka unakuja.Muswada huo tayari ulipitishwa na Baraza la Wawakilishi Jumatano iliyopita na rais Donald Trump ameutia saini jana kuwa sheria.Wabunge bado wanavutana kuhusu mpango mpana wa matumizi ya mwaka 2021 ambao sehemu ya fedha zitakazoidhinishwa zitatumika kuchochea ufufuaji wa uchumi uliothiriwa na janga la virusi vya corona.
Hakuna maoni