Spika Ndugai Awashauri Vijana Wagombee Udiwani na Ubunge Kukabiliana na Tatizo la Ajira


Spika wa Bunge la Tanzania mheshimiwa Job Ndugai amewataka vijana nchini kugombea nafasi mbalimabali  za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge ili kutatua tatizo la kukosa ajira kutokana na kukosa uzoefu.

Spika Ndugai amesema hayo Bungeni leo, Mei 18, 2018 baada majibu ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Bunge, Jenista Mhagama, kutokana na swali la mbunge wa viti maalumu Zainab Katimba aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana wasomi wasikuwa na uzoefu.

“Asante sana Waziri wa nchi kwa majibu ya nyongeza, Vijana wasomi, zipo kazi nyingine hazihitaji uzoefu, mnaweza mkagombea Udiwani, mkagombea Ubunge, nawatangazia vita waheshimiwa hapa” amesema Spika Ndugai.

Awali Naibu Waziri, Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira  na walemavu Anthony Mavunde amesema kwamba serikali imeendaa utaratibu wa kuwapa vijana nafasi za kujitolea katika makampuni na mashirika mbalimbali ili kupata uzoefu wa kuweza kuajiliwa

“Kupitia mpango huu utawasaidia sana vijana wasomi  wa nchi yetu ambao walikuwa wakipata tabu na kikwazo cha uzoefu, kwa hivi sasa atapata nafasi ya kujifunza katika kampuni kwa muda huo wa mwaka mmoja na badae tutampatia cheti cha kumtambua ili iwe kama kiambatanisho chake” amesema Naibu Waziri Mavunde.
Spika Ndugai Awashauri Vijana Wagombee Udiwani na Ubunge Kukabiliana na Tatizo la Ajira Spika Ndugai Awashauri Vijana Wagombee Udiwani na Ubunge Kukabiliana na Tatizo la Ajira Reviewed by RICH VOICE on Mei 18, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...