Breking News: Msafara Wa Waziri Kigwangala Wapata Ajali,mwandishi Afariki.


Na John Walter –Babati
Taarifa ambazo zimepatikana muda huu kutoka Magugu Babati mkoani Manyara  zinaeleza kuwa gari la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakitokea Arusha kwenda Dodoma wamepata ajali mbaya na inaelezwa kuwa mwandishi wake amepoteza maisha pale pale.

Kamanda wa polisi mkoa wa  Manyara Agustino Senga amesema kuwa Dr.Kigwangala aliejeruhiwa  vibaya maeneo ya kifuani  na dereva wake wamelezwa katika kituo cha Afya Magugu kwa matibabu.

Taarifa za awali kutoka kwa kamanda wa polisi Agustino Senga  zinaeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na mnyama aliekuwa akivuka bara bara eneo la Magugu. 

Breking News: Msafara Wa Waziri Kigwangala Wapata Ajali,mwandishi Afariki. Breking News: Msafara Wa Waziri Kigwangala Wapata Ajali,mwandishi Afariki. Reviewed by RICH VOICE on Agosti 04, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...