Uchaguzi Zimbabwe: Maduka yafungwa Harare huku jeshi likipiga doria

Wanajeshi wanapiga doria katika barabara za HarareWanajeshi waliojihami wamepiga doria wakiwataka raia kuwa na nidhamu.Watu watatu waliuawa mjini humo siku ya Jumatano wakati wa ghasia kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nelson Chamisa.
Bwana Chamisa alisema siku ya Jumatatu kwamba uchaguzi huo wa Jumamosi ulifanyiwa udanganyifu ili kumpatia rais Mnangagwa ushindi.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.Biashara zimefungwa katika mji mkuu wa Zimbabwe harare huku taifa hilo likisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa.
Matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya upinzani nchini Zibabwe baada ya uchaguzi wa Jumatatu yameichochea jamii ya kimataifa kutoa wito wa kumaliza vurugu.
Umoja wa mataifa na umoja wa ulaya kwa pamoja wamekemea juu vurugu zilizotokea na polisi kufyatua risasi kwa waandamanaji.
Uchaguzi Zimbabwe: Maduka yafungwa Harare huku jeshi likipiga doria Uchaguzi Zimbabwe: Maduka yafungwa Harare huku jeshi likipiga doria Reviewed by RICH VOICE on Agosti 02, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...