Joseph Kasheku Msukuma Afunga Bara Bara Kwa Muda Babati.



Na John Walter- Babati
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘King Msukuma’ amemwakikishia mgombea udiwani wa chama cha Mapinduzi Nikodemus Bonifasi kuwa atashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Marudio utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.

Msukuma amemtabiria ushindi huo Mgombea huyo akiwa katika mkutano wa kampeni  kata ya Bagara mjini Babati uliofanyika mtaa wa Osterbay na kuhudhuriwa na Mamia ya wakazi wa Babati.

Huku msukuma akitumia zaidi ya dakika 45 kumnadi mgombea huyo maarufu kwa jina la Nyeusi aliongoza maandamano ya amani hadi ofisi za Ccm mtaa wa Osterbay kwa miguu na kuziba bara bara kwa muda huku wakiimba na kucheza nyimbo maarufu ya chama hicho ‘Ccm mbele kwa mbele.

Uchaguzi huu katika kata ya Bagara unakuja baada ya diwani wa Chadema Bwana Nyeusi ambaye ndiye mgombea wa Ccm kukihama cha hicho.

Kwa upande wa Chadema wamemsimamisha mwenyekiti wa mtaa wa Miomboni  Mathayo Zebedayo kugombea nafasi hiyo.

BY RICH OICE.
Joseph Kasheku Msukuma Afunga Bara Bara Kwa Muda Babati. Joseph Kasheku Msukuma Afunga Bara Bara Kwa Muda Babati. Reviewed by RICH VOICE on Agosti 02, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...