Diamond Amuunga Mkono Jokate....Aahidi Kukamilisha Madarasa Matatu Kisalawe



Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ni miongoni mwa waliojitolea kuinua elimu ya watoto katika Wilaya ya Kisarawe ambayo inaongozwa na Jokate Mwegelo.

Muimbaji huyo ameahidi kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu kwa upande wa madirisha na milango. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Kwa kutambua thamani ya Elimu kwa watoto na wadogo zetu........Kwa kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli katika kuhakikisha watoto wetu wa Tanzania wanapata elimu Bora na Bure. Na kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mh Jokate Mwegelo Katika kampeni ya kutokomeza Zero Kisarawe." ameeleza.

"Mimi Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz Naahidi kuchangia madirisha na milango kwa Madarasa Matatu, kwa ajili ya Shule Kisarawe. tafadhali tuwasaidie watoto au wadogo zetu kwa Kisarawe kwa kuchangia kupitia maelekezo yalio kwa clip hii ama, kufika pia Tarehe 22/09/2018 pale Minaki Sekondari kwenye Harambee ya Kuchangia Kampeni Hii ya Tokomeza Zero," ameeleza Diamond.
Diamond Amuunga Mkono Jokate....Aahidi Kukamilisha Madarasa Matatu Kisalawe Diamond Amuunga Mkono Jokate....Aahidi Kukamilisha Madarasa Matatu Kisalawe Reviewed by RICH VOICE on Septemba 22, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...