Safari ya matibabu ya Hawa wa Diamond kwenda India yakwama


Msanii Hawa Said maarufu Hawa wa Diamond, amejikuta akirudishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) baada ya kutotimiza vibali vya kusafiri vya kimatibabu kwenda India.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi  baada ya kukwama jana Oktoba 13, 2018 meneja wa Diamond Platinumz ambao ndiyo wamechukua jukumu la kugharamia matibabu hayo, Babu Tale amesema hali hiyo imewakuta wakiwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa ndege na kuanza kukaguliwa nyaraka zao mbalimbali.

Babu Tale amesema nyaraka iliyowakwamisha kusafiri ni kibali cha daktari kuelezea hali ya mgonjwa ili wahudumu ndani ya ndege wajue namna watakavyomhudumia.

“Kuna mgonjwa anaweza akawa katika hali ya kuzimia, kutapika anatakiwa ahudumiwe tofauti, hivyo Hawa imeshindikana kwa kuwa hakuna hizo nyaraka inayoonyesha hivyo kutoka kwa daktari na wametwambia turudi itakapokamilika,” amesema.

Hawa, Babu Tale na mama yake, Ndagina Hassan ilikuwa waondoke jana saa 10:45 na ndege ya Shirika la Emirates.

Hawa na mama yake, Ndagina, walifika uwanjani hapo tangu saa 7:00 mchana huku Babu Tale akiwasili saa 9:00 alasiri.

Naye Hawa amewaomba Watanzania kumuombea dua katika matibabu hayo.
Safari ya matibabu ya Hawa wa Diamond kwenda India yakwama Safari ya matibabu ya Hawa wa Diamond kwenda India yakwama Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 14, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...