HABARI ZA JUMAMOSI HII TAREHE 11/02/2017
Saturday, February 11, 2017
Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya February 11
Friday, February 10, 2017
Yusuf Manj na Askofu Gwajima Kuendelea Kusota Selo.....Sirro Asema Upelelezi Bado Unaendelea
Kamanda
Sirro amesema bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji
pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma
za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.
Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.
Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.
Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .
Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.
Freeman Mbowe Kagoma kwenda Polisi Kuitikia Wito wa Makonda......Kasema Lazima Amshitaki Kwa Kumchafulia Jina
Mbunge
wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.
Mbowe
ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini
Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha
Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.
Mbowe
amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za
kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa
wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.
Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa.
Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.
Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.
Wakati
huo huo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Hai, Freeman
Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge kutoka Bunge la Ulaya,
David Martin, Gerrard Quille, Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Roeland
Van De Beer na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na
Kikanda,Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, mjini Dodoma leo Ijumaa
10/02/2017.
Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru
atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda
wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe
kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda.
Amesema
operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa
hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na
wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani
taarifa imeshatolewa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
Agizo wa Rais Magufuli uwanja wa ndege Dar laanza kutekelezwa
Shughuli
za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017
zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08
Februari, 2017.
Wafanyakazi
850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya
ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia
na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.
Pia,
timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo
wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.
Mkandarasi
ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri
ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika
mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za
ujenzi kuendelea.
Katika
ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji
wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni
kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa
dosari na kuahidi kuchukua hatua.
Mhe.
Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa
malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa
ujenzi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Zitto Kabwe amkingia kifua Mbowe....Msikilize Hapa Akiongea
Mbunge
wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto
Kabwe amemkingia kifua Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kusema
kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha na dawa za kuleva
kwa namna yoyote
Zitto
ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano wake na wanahabari leo mjini
Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni sawa na
kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.
Rais Magufuli ateua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya
Anaswa na mzigo wa dawa za kulevya chumbani..... RPC Mwanza asimulia Sakata Zima
Mtu
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la
kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha
pinchi 240 na ndonga mbili.
Taarifa
ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa
jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43, amekamatwa majira ya
saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba
wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza
Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi
walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja
na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Aidha
wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za
mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa
kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa
madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.
Tukio lilivyokuwa
Askari
walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo
ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani
anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia
dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo
maarufu kama pichi.
Wakati
askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na
kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi.
Aidha
askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi YA askari
waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini
bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la
choo.
Msangi
amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje walikwenda kuvunja
bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na kuweka
kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku
nyingine zikibebwa na maji .
Polisi
wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa
watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya
kulevya.
HABARI ZA JUMAMOSI HII TAREHE 11/02/2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 10, 2017
Rating:
Hakuna maoni