HABARI ZA ALHAMISI YA TAREHE 23/02/2017


Image may contain: 1 person, text Picha ya NYU FM Radio 99.3MHz Arusha TZ.....

SASA HIVI FUATILIA RADIO YETU MTANDAONI  REDIO NYU FM 99.3 >> BONYEZA HAPA>>www.nyufmradioonline.radio12345.com 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 23

 

 

RAIS DKT. MAGUFULI AMSAIDIA DADA NEEMA MWITA WAMBURA ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE MKOANI MARA.

Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano. Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.
  Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni kitendo kilichofanywa na mume wake.


 
AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUENDELEA KESHO

Baada ya Simba kutangulia robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup kwa kuifunga African Lyon kwa bao 1-0, mechi nyingine za kuwania nafasi hiyo zitaanza kuchezwa kesho Ijumaa Februari 24, mwaka huu.

Simba iliilaza African Lyon katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliofanyika Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


LIGI KUU YA WANAWAKE SASA KUANZA FEBRUARI 26

Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye kituo kimoja cha Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.

Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.

RAIS WA UGANDA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni atakayoifanya hapa nchini tarehe 25 na 26 Februari, 2017.Kulia ni Balozi Innocent Shiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, kushoto ni Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani

BALOZI SEIF AZINDUA JENGO LA MADARASA YA SKULI YA MAANDALIZI YA KIOMBAMVUA HUKU AKIWATAKA WANAFUNZI KUJIKITA KATIKA MASOMO YA SAYANSI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa wanafunzi Nchini kujikita zaidi katika jitihada za kupenda somo la Sayansi ili kunusuru hali iliyopo hivi sasa ya upungufu wa Walaamu wa fani hiyo maskulini na hata katika Taasisi za Umma.

Alisema licha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuajiri walimu wengi wa masomo ya Sayansi katika azma yake ya kukabiliana na tatizo hilo lakini bado upungufu huo unaendelea kuziathiri skuli nyingi Unguja na Pemba.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa angalizo hilo baada ya kuzindua rasmi jengo jipya la madarasa Mawili ya Skuli ya Maandalizi ya Kiombamvua lililojengwa na Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff kutekeleza ahadi uliyotoa wa kusaidia huduma za Kijamii na maendeleo ya Wananchi wa Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli hiyo.

Alisema baadhi ya wakati Serikali hulazimika kuagiza walimu wa fani ya sayansi kutoka nje ya Nchi jambo ambalo husababisha kutumia gharama kubwa ya fedha ambayo inaweza kupunguzwa iwapo wanafunzi wenyewe wataamua kupenda masomo ya sayansi.

Balozi Seif ambae pia ni mwakilishi wa Jimbo la Mahonda aliwahimiza wanafunzi wote wa Jimbo hilo kuongeza juhudi za masomo wakati Uongozi wao unajitahidi kujenga mazingira mazuri yatakayowaondolea changamoto zinazowakabili katika masomo yao.

Alisema Uongozi wa jimbo la Mahonda una malengo katika kuona wanafunzi wote wa skuli zilizomo ndani ya jimbo hilo wanaendelea kupata elimu yao hadi upeo wa uwezo wao kimasomo.

Balozi Seif alifahamisha kwamba juhudi kubwa zimeanza kuchukuliwa na Uongozi huo katika kuzijengea miundombinu pamoja na vifaa vya Maabara na Maktaba baadhi ya skuli za sekondari za Jimbo hilo ili kuwa na uwezo na maarifa wanafunzi hao ya kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya Taifa.

Alikemea tabia ya baadhi ya wanafunzi kupenda kuzurura ovyo wakati wa masomo maskulini na kuagiza kutaka kuachwa mara moja kitendo hicho kisicholeta tija katika hatma yao ya baadae.

Balozi Seif aliushukuru Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff kwa uungwana wake wa kutekeleza ahadi uliyotoa wakati wa vikao vyake na Uongozi wa Kamati ya Bandari ya Kiombamvua katika njia ya kuleta maridhiano ya pande hizo mbili.

Balozi Seif alisema hali haikuwa shwari kati ya Wananchi wa Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli ya Sea Cliff na Uongozi wa Hoteli hiyo iliyotaka kulitumia eneo la pembezoni mwa Bahari ya Kiombamvua kwa ajili ya kujenga uwanja wa mchezo wa Golf licha ya kufuatwa kwa taratibu zilizohusika.

Alisema mzozo huo ulikuwa ulichochewa na baadhi ya wanasiasa na kupelekea Kamati ya Bazara la Wawakilishi Zanzibar kuingilia kati na hatimae kuagizwa kufuatwa kwa muongozo uliokubalika na pande hizo mbili.

Mapema akikabidhi funguo za Jengo la Skuli hiyo ya Kiombamvua kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye na yeye kumkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma, Mwakilishi wa Hoteli ya Sea Cliff Nd. Yasser De Costa alisema Uongozi huo utaendelea kusaidia kuduma za Kijamii kadri hali itakavyoruhusu.

Nd. De Costa aliwashukuru Wananchi wa Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli hiyo kwa ushirikiano wao wa kina uliopelekea kuchanyua kwa maendeleo yanaoanza kuonekana ndani ya Vijiji hivyo likiwemo suala zito la kuimarika kwa huduma za Elimu.

Mwakilishi huyo wa Sea Cliff aliwasihi wanafunzi wa Vijiji hivyo kuacha mzaha na badala yake akili na maarifa yao wakayaelekeze katika kusaka Elimu itakayowajengea nuru njema katika mustakaba wa maisha yao ya baadaye.

Akitoa salamu za Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bwana Jean Claude alieleza kwamba matunda ya jengo hilo Jipya la Skuli ya Maandalizi ya Kiombamvua lazima yaonekane.

Bwana Claude alisema elimu ndio kila kitu ikiwa ni msingi imara wa maendeleo wakati na mahali popote pale Duniani.

Akipokea funguo za Jengo hilo jipya la Skuli ya maandalizi ya Kiombamvua Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziri Pembe Juma aliwahakikishia Wananchi wa Kiombamvua kwamba kazi iliyobaki ya kumalizia uwekaji wa vikalio na huduma za Walimu ndani ya jengo hilo ni ni jukumu la Wizara hiyo.

Akiushukuru Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff kwa misaada yake ya kuunga mkono sekta ya Elimu Zanzibar Mh. Riziki alisema jitihada zitafanywa mara moja katika kuona majengo hayo yanaanza kazi mara moja ili kuwaondoshea usumbufu watoto wa maeneo hayo.

Alishauri ipo haja ya kuchukuliwa kwa hatua za mapema kati ya Wananchi wa Kiombamvua na Wizara ya Elimu katika kufikiria wazo la kuanza ujenzi wa majengo ya Skuli ya Msingi ili watoto wanaomaliza mafunzo yao ya maandalizi Skulini hapo waendelee kwa hatua ya elimu ya msingi.

Ujenzi wa Jengo jipya la Skuli ya Maandalizi ya Kiombamvua lenye madarasa Mawili, Vyoo, Ofisi ya Walimu pamoja na Tangi la kuhifadhia Maji lililojengwa na Hoteli ya Sea Cliff limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 70,000,000/-.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/2/2017.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akifarajika pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Issa Juma mara baada ya kulizindua rasmi jengo jipya la Madarasa Mawili la Skuli ya Maandalizi ya Kiombamvua lililojengwa na Hoteli ya Sea Cliff.
Balozi Seif akimkabidhi Ufunguo wa Jengo la Skuli ya Maandalizi ya Kiombamvua Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma katika hafla rasmi ya uzinduzi wa Skuli hiyo.


WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

WAKALA WA WAYNE ROONEY AENDA CHINA KUMTAFUTIA TIMU

KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA TAYODEA KWA KUSAIDIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga, Faidha Salim.
Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa baadhi ya vifaa vya ushonaji waliokabidhiwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa kitu na Meneja wa Mradi wa WEKEZA wa Tayodea Michael Mchomvu wakati wa halfa hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akitazama vifaa mbalimbali vya ushonaji wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea ,David Chanyegea.


MBUNGE WA JIMBO LA ILEJE, JANETH MBENE AMTEMBELEA NAIBU WAZIRI MASAUNI, OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

JUVENTUS YAITUNDIKA MBILI FC PORTO LIGI YA MABINGWA ULAYA

MANCHESTER UNITED YATINGA KIULAINI HATUA YA 16 BORA LIGI YA UROPA

JAMIE VARDY AFUNGA GOLI MUHIMU LICHA YA LEICESTER CITY KULALA

CRISTIANO RONALDO ASHINDWA KUISAIDIA REAL MADRID KUZAMA

BALOZI SEIF AKAGUA JENGO LA PALACE HOTEL

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali alipofika kulikagua Jengo la Mashariki Palace Hoteli Restaurent liliopo Pembezoni mwa Skuli ya Msingi Forodhani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif kati kati akiwa na Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume Kulia yake pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud kushoto yake na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani wakilikagua jengo hilo mapema asubuhi.
Balozi Seif kati kati akiwa na Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume Kulia yake pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud kushoto yake na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Said Sarboko Makarani wakilikagua jengo hilo mapema asubuhi.
  Balozi Seif na Viongozi mbali mbali aliyofuatana nao wakipanda ngazi ndani kulikagua jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko kushoto akimueleza Balozi Seif na baadhi ya Viongozi hatua iliyochukuliwa na Taasisi yake katika kulifanyia matengenezo makubwa Jengo Mashariki Palace Hoteli Restaurent liliopo Forodhani.


ASKOFU GADI AMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI KUMTEUA KAMISHNA WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, AMUOMBEA PAMOJA NA NCHI

Askofu wa Good News for All Ministry, Dkt. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari wakati madhehebu mbalimbali hapa nchini walipomuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nchi, pamoja na kumpongeza kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist jijini na katikati ni Askofu Ernest Sumisumi wa kanisa hilo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Askofu wa Good News for All Ministry, Dkt. Charles Gadi wakati alipokuwa akizungumza.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiongozwa na Askofu wa Good News for All Ministry, Dkt. Charles Gadi (katikati), wakiimba wimbo wa amani wakati wa kumuombea Rais Dk. Magufuli na Taifa.
Askofu Filbert Mbepera (wa pili kuli) wa Kanisa la EAGT, akiombea amani nchi.
Askofu Ernest Sumisumi (wa pili kushoto) wa Kanisa la Baptist akiiombea ramani ya Tanzania pamoja na picha ya Rais Dk. John Magufuli.


SERIKALI KUJENGA UWANJA WA NDEGE BABATI

Jumatano, 22 Februari 2017

KAMISHNA WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MASAUNI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga (kushoto), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati Kamishna huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu kupambana na dawa za kulevya nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KASEJA MCHEZAJI BORA WA JANUARI LIGI KUU YA VODACOM

MAJALIWA AZUNGUMA NA WATUMISHI NA KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI BABABTI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuhitimisha ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Babati wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuhutubia mkutano wa hadhara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi wa Babati wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Februari, 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya watumishi wa serikali na Halmashauri za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na Halmashauri za mkoa wa Manyara kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
HABARI ZA ALHAMISI YA TAREHE 23/02/2017 HABARI ZA ALHAMISI YA TAREHE 23/02/2017 Reviewed by RICH VOICE on Februari 23, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...