JUMATANO 01/02/2017
RAIS DKT MAGUFULI AREJEA KUTOKA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, ALIKOHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA (AU)
MGODI WA BUZWAGI WALIPA KODI ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja
Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi
ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili
Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa
kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi
Marry Manyambo.
Mkuu wa
Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi
wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 ,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama,
mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru
wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.
Baadhi ya
waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla
ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani
wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla
ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa
wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa
wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa
dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu tawala wa wilaya
Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.
CUF YA PROFESA LIPUMBA YAJIBU MAPIGO KUHUSU RUZUKU WALIYOPEWA NA HAZINA
Mkurugenzi
wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C
Malima (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam leo kuhusu ruzuku ya
chama hicho iliyopokelewa kupitia akaunti namba 2072300456 ya Benki ya
NMB Tawi la Temeke. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke
Jafar na Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud.
Meza Kuu.
Kutoka kulia ni Kamanda Mkuu, Athumani Hamadi,Mkurugenzi wa Mipango na
Uchaguzi, Mneke Jafar, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama
cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima, Katibu Jumuiya ya Wanawake
(JUKE), Salama Masoud na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Masha Amour.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.Mkutano ukiendelea. |
TAARIFA KWA UMMA
The Civic
United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) chini ya Uongozi thabiti wa
Mwenyekiti wake Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kinaishukuru na
kuipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kukipatia Chama chetu
Ruzuku yake inayopatikana kwa Mujibu wa Sheria ya vyama vya Siasa Namba
5 ya mwaka 1992.Pamoja na Ruzuku ya CUF kuzuiwa kwa Muda wa miezi mine (4) kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi Desemba 2016 kutokana na sintofahamu ya uongozi wa Kitaifa wa CUF, Msajili hakuona haja ya kuendelea kuizuia wakati shughuli za chama zinafanyika kila siku. Kuendelea kuizuia Ruzuku halali ya chama ni kukizuia kufanya kazi zake halali za kisiasa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika chaguzi mbali mbali za kiserikali zinazoendelea nchini.
Waheshimiwa wanahabari, Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia katiba ya CUF ya mwaka 1992, Toleo la 2014 alijiridhisha kuwa Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ndiye Mwenyekiti halali wa CUF kwa kuwa mchakato wa kukamilisha kujiuzulu kwake haukukamilika kabla yeye kutengua barua yake ya kujiuzulu.
Mnamo Tarehe 23 Septemba 2016 , Msajili aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa CUF kumjulisha msimamo na mwongozo wa wake kuwa “Mwenyekiti wa Taifa wa CUF ni Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba”
MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha
Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya
Upandaji MitiKimkoa . Na Emanuel Madafa,Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya. Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60. Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya. Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa mazingira katika maeneo yot. "Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala. Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku. "Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema . Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo. Mwisho |
Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017 |
Afisa habari na Mawasiliano Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)akichukua matukio katika tukio hilo la kilele cha upandaji miti kimkoa katika safu ya Mlima Mbeya Itagano. |
Wednesday, February 1, 2017Breaking News: Mtokeo ya Kidato cha Nne 2016 Yametoka......Bofya Hapa Kuyatazama
Baraza
la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne
mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53%
mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu
Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi
408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu,
wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424
sawa na asilimia 73.26.
Kwa
upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na
asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na
wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa
upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu
mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.
Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015. Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu. Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara
********
| |
Wednesday, February 1, 2017Bunge Lapitisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada
wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid
Bill, 2016).
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa
taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa
sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua
ya kujadiliwa na Bunge tukufu.
Aliendelea
kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada
wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya
nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua
utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na
Madai kwa mahitaji.
Aidha
utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu
baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya
kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa
ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale
inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au
yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.
“Kumekuwepo
na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na
wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa
kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili
kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa
taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua
Dkt. Mwakyembe.
Vile
vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa
kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya
Jinai).
Kwa
upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia
wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa
Kisheria.
Aidha,
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo
muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili
kuwa Sheria.
Wednesday, February 1, 2017Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya February 1Wednesday, February 1, 2017Mafuriko ya Mvua yabomoa nyumba na Kuua Watu Wanne Mpwapwa- Dodoma
Watu
wanne wakiwamo watatu wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba
zao kusombwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia
jana katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Hata hivyo, viongozi mbalimbali wametoa takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema watu wanane walikuwa
wameripotiwa kufariki dunia na kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
ilikuwa inajiandaa kwenda eneo la tukio ili kujionea uharibifu
uliotokea.
Lakini,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema taarifa
alizonazo ni za watu watatu waliopoteza maisha na kwamba bado hajapata
taarifa sahihi za tukio ambalo lilitokea katika vijiji vya Mang’angu na
Chinyika katika Kata ya Ving’awe.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, mmoja wa manusura, Beka Mlami (10) alisema
walikuwa wamelala wakiwa watano katika nyumba yao mvua kubwa ilipoanza
kunyesha kuanzia saa tatu usiku na ilipofika usiku wa manane nyumba yao
iliyojengwa kwa udongo ilisombwa na maji.
Mbali
na yeye, wengine waliokuwa katika nyumba hiyo ni Martha Sumisumi (60),
Shukuru Donald (15) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika
Shule ya Sekondari Mwanakianga, Bernadetha Sumisumi (9) aliyekuwa
mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ilolo na Joseph
Sumisumi (12) ambaye alinusurika.
Beka
alisema baada ya kuona maji yameingia ndani, aliwaambia ndugu zake
wakimbie watoke nje na wakati wanajiandaa kuvaa nguo nyumba yao
ilianguka na kuwaponda, lakini yeye alifanikiwa kutoka na kupanda juu ya
bati.
Alisema
baada ya kutoka nje ndipo gogo kubwa la mti lililosombwa na maji
lilipopiga nyumba yao na kuanguka chini hivyo ndugu zake wengine
kushindwa kutoka na hivyo kusombwa na maji.
Alisema baada ya kutoka nje alimwona ndugu yake mwingine Joseph akiwa anapelekwa na maji, lakini alifanikiwa kujiokoa.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo, Steven Noel alisema nyumba iliyosombwa na maji
ilikuwa imejengwa karibu na korongo la maji, hivyo baada ya mvua
kunyesha, maji yaliacha mkondo wake na kuingia kwenye makazi ya watu na
kusababisha maafa hayo.
“Mvua
ilisababisha mafuriko makubwa ambayo yalikuwa yamebeba na magogo
makubwa ambayo yaliipiga ile nyumba na kuivunja katikati,” alisema Noel.
Alisema
baada ya gogo la mti kuipiga nyumba hiyo, maji yalijaa ndani na kwa
kuwa milango ilikuwa imefungwa, yalikosa njia ya kutokea na kuiangusha.
Noel
alisema kulipopambazuka, walifukua na kuipata miili ya watu hao watatu
huku mwili mwingine wa Jesca Lubeleje (19) mkazi wa Kijiji cha Chinyika
ukiokotwa.
|
JUMATANO 01/02/2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 01, 2017
Rating:
Hakuna maoni