ALHAMISI HII YA LEO 05/01/2016


 PLAZA.jpgJEMBE1.jpg 

MKEKA.jpg

MWANAMKE ASHINDA BAHATI NASIBU BAADA YA KUBASHIRI NAMBA HIZO HIZO KWA MIAKA

WAZIRI MKUU AKAGUA GHALA LA NFRA SONGEA


JAMES RODRIGUEZ AIBEBA REAL MADRID COPA DEL REY


WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI

Waziri mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za serekali katika misa ya kumuombea maerehemu Kapteni K enan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea Parokia ya Mtoto Yesu Matogoro Songea
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakiweka shada la maua katika kaburi la aliye kuwa Mkuu wa ndege za serekali Kapteni Kenan Mhaiki aliye fariki tarehe 31/12/2016 nakuzikwa tarehe 4/1/2017 kijijini kwao Matogoro Mkoani Ruvuma. Picha na Chris Mfinanga
Mke wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake
Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Muahiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao. Picha na Chris Mfinanga

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI


DELE ALLI ATIKISA NYAVU MARA MBILI NA KUITIBULIA CHELSEA KUWEKA REKODI





Timu ya Tottenham imekwamisha jitihada za Chelsea kuweka historia ya kushinda michezo 14 mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kuifunga magoli 2-0 katika dimba la White Hart Lane.





Kwa ushindi huo Tottenham imekwea hadi katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi, shujaa akiwa Dele Alli aliyefunga kwa mpira wa kichwa katika kila kipindi, na kuifanya Chelsea iongoze ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Liverpool ya pili.





Alli alifunga goli la kwanza baada ya kuruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliopigwa na Christian Eriksen katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, na wawili hao tena walishirikina na Alli kufunga goli lingine katika kipindi cha pili.
                                Dele Alli akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli 
                   Pedro na Diego Costa walijikuta wakibwatukiana baada ya maji kuzidi unga



MADHARA YA KUTAMANI WASICHANA USIYO WAJUA


UZINDUZI WA VIFAA VIPYA VYA KUTEREMSHIA MAKONTENA UNGUJA.

ruge
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo Makontena ya mizigo mizito wakiwepo na Viongozi mbali mbali, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
ruge-1
Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
ruge-2
Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Picha na Ikulu.
ruge-3
Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Picha na Ikulu.
ruge-4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja katika Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(katikati) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahamoud, Picha na Ikulu.



MASAUNI AFANYA ZIARA MAGEREZA, AAGIZA SARE ZOTE ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA IDARA YA UHAMIAJI KUANZIA SASA ZISHONWE KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ESA SALAAM

uwe
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam.
uwe-1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika eneo la Ujenzi wa nyumba hizo 9,500, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo, ambazo Rais Dk. John Magufuli ametoa Shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa.
uwe-2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiiikagua moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zinazojengwa Ukonga, jijini Dar es Salaam. Jumla ya nyumba 9,500 zinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo mara baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa shilingi Bilioni Kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Masauni alifanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, na alitoa agizo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji, kuhakikisha kuwa, sare za idara hizo kuanzia sasa zitakuwa zinashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga. Mbele kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa.
uwe-3
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akitoka katika Jengo la Useremala mara baada ya kukagua mashine mbalimbali zinazotumika kuranda na kuchana mbao kwa ajili ya utengenezaji wa samani katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.
uwe-4
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikiangalia kikapu kilichoshonwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Watatu kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.



MADIWANI WASIPEWE FEDHA ZA MAENDELEO MKONONI


WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF

ppsf
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Semina hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na Pensheni. Katika senmina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF.
Meneja wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutambua na kusajili wanachama wapya, kukusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.

Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.
 
Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari. Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya. Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
 
“Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu. Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.

Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama
 Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada


Jumatano, 4 Januari 2017

MAANDALIZI YA AIRTEL RISING STARS YAKAMILIKA

Kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye Uwanja wa Karume huku wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki.

Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita.

Kliniki hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya taifa Oscar Milambo akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku wasichana wakifundishwa na Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Queens, Sebastian Nkoma.

Akizungumzia maandalizi ya kliniki hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo ya soka la vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi alisema, “Kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za mpira, na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili kuongezewa vipaji vyao.

“Sisi TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens.” alisema Nyenzi na kuongeza:

“Tunaamini ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars. Nachukua nafasi hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars.”

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa miaka 15, Oscar Milambo alisema: “Wachezaji watafundishwa nidhamu ya mpira, ndani na nje ya uwanja, jinsi kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia.”

Sambamba na hayo wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata mafunzo kutoka kwa makocha. Milambo aliongeza kuwa vijana hao watafundishwa jinsi mchezaji anavyotakiwa kujitunza kwa manufaa ya kuendelea kutunza kipaji chake.

Akizungumza juu ya kliniki hiyo, Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa kufanyika kwa kliniki kutahitimisha Airtel Rising Stars msimu wa sita na kufungua pazia kwa maandalizi ya Airtel Rising Stars msimu wa saba.

Michuano ya Airtel Rising Stars mwaka 2016 tuliunganisha na promosheni ya kampuni ya Airtel ya ‘Airtel Fursa’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha vijana kufanikisha malengo yao.

Matinde aliongeza kuwa Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza vipaji vya soka kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania. Airtel Rising Stars inalenga kutafuta vipaji chipukuzi kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa.

“Kampeni yetu ya Airtel Fursa inalenga kuwainua vijana na kuwawezesha kufikia ndoto zao inaenda sambamba na program hii ya Airtel Rising Stars na tunajisikia furaha kuendelea kuwafikia vijana katika nyanja mbalimbali,” aliongeza Matinde.

Wachezaji zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke,Lindi na Zanzibar.

Kafulila kupokea kadi ya Chadema jimboni Kwake Mwezi Huu

Aliyekuwa  Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema atapokelea kadi ya Chadema jimboni mwake baadaye mwezi huu.

Kafulila alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema kwa alichoeleza kuwa ndicho chama kilichojipambanua kuelekea safari ya mabadiliko ifikapo mwaka 2020.

Kada huyo tayari amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe kumjulisha kuwa anajivua uanachama na  anarudi Chadema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kafulila alisema ameamua kuwa atapokelea kadi hiyo jimboni kutokana na mapenzi aliyonayo kwa wananchi wake.

"Nimepanga kuchukua kadi mwezi huu jimboni, kwa kuwa ilikuwa nichukue kadi mwanzoni lakini ilishindikana kutokana na siku kuu, hivyo siku yoyote kuanzia sasa nitachukua," alisema.

Wakati anajiuzulu NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema, alisema hakufanya uamuzi kwa kukurupuka bali alitafakari na kushauriwa na wananchi wa jimbo lake, na kuridhika kurudi huko.

"Nilitafakari na kushauriwa sana jimboni na kuridhika kwamba Chadema ndiko sehemu inayojipambanua kwa mikakati ya kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania na ni vema kukusanya nguvu ya kila mwenye kiu ya mabadiliko ndani ya chama kimoja, ili kufupisha safari ya mabadiliko," alisema.

Alipoulizwa kwa nini amerudi Chadema wakati aliyekuwa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alipata kumwita sisimizi kwa  alichoeleza kuwa hakuwa na imani naye, alijibu kuwa siasa ni malengo si uhusiano binafsi.

Kafulila aliongeza kuwa wanasiasa wanaunganishwa na malengo zaidi ya urafiki na kwamba malengo yake sasa ni kuendelea kupigania mabadiliko ya kimfumo yanayoenea zaidi kwenye chama hicho (Chadema) kuliko kingine.

Novemba 10, 2009 Kafulila alijivua uanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi kutokana na kuondolewa kwenye nafasi ya uofisa habari wa chama hicho.

Pia akiwa NCCR-Mageuzi, alitimuliwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho na tuhuma za kutaka 'kumpindua' Mwenyekiti, James Mbatia.

Hata hivyo, suala hilo lilipata suluhu baada ya Mbatia kuteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Wakiwa bungeni, Mbatia na Kafulila walikutana, kuzungumza na hatimaye kumaliza mzozo wao.


Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humprey Polepole atangaza neema kwa Wanafunzi waliokosa mikopo


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humprey Polepole amewatangazia neema wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo, akiwataka wamtafute ili awaoneshe cha kufanya


Polepole ambaye alikuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV  aliuzwa na baadhi ya watu kuhusu tatizo lililopo la mikopo ya elimu ya juu, ambapo aliwajibu kuwa serikali imekwishatoa maelekezo kwamba haiwezi kumkopesha kila mtu na kwamba inatoa mikopo kwa vigezo vilivyowekwa.

Kuhusu watu wasioweza kujigharamia elimu hiyo na wamekosa mikopo, amewashauri kuahirisha masomo yao, ili wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata pesa na ndani ya mwaka mmoja ana uhakika watakuwa wamepata pesa zinazohitajika na kuendelea na masomo yao.

Polepole alitaja baadhi ya shughuli ambazo angewashauri wazifanye kuwa ni pamoja na kilimo huku akitolea mfano baadhi ya watu aliowashauri wajiingize kwenye kilimo cha matikiti na wakaufanyia kazi ushauri huo, ambapo baada ya muda wameona matunda yake.

"Waliokosa mikopo vyuo vikuu wanitafute, nitawaonesha cha kufanya, na wawe tayari kuahirisha masomo mwaka mmoja"

Akizungumzia uamuzi wa serikali kusimamisha ajira, Polepole amesema serikali haiwezi kuendelea kuajiri wakati inafanya kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa ambao wanalitia hasara taifa na kuwataka watanzania waendelee kuwa watulivu na kumuunga mkono Rais Magufuli, ili amalize mchwa wote serikali na kisha ajira zitatoka.

"Nawaambia vijana wakati unasubiri ajira usibweteke kwani mtu anayebweteka akipata kazi ataharibu kazi yetu"

Kuhusu serikali kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati pekee, Polepole amesema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa taifa lina uhaba mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati kuliko walimu wa masomo ya sanaa.

"Tunao utimilifu wa walimu wa sanaa, tunao upungufu wa walimu wa Sayansi"


Amuua Mkewe Kwa Visu na Kumnyonga Mtoto Baada ya Kuambiwa Ana Mchepuko Nje ya Ndoa

Mkazi  wa Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, amemuua mkewe pamoja na mtoto wake.

Mkazi huyo Rashid Nassoro, baada ya kuwaua watu wake wa karibu alikimbia na baadae kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amethibitisha tukio hilo na kusema lilitokea juzi eneo la Bukene, wilayani hapa baada ya Rashid Nassoro (22) kumuua mkewe kwa kumchoma visu tumboni.


Jeshi la Polisi Laua Majambazi Watatu Dar es Salaam

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado hayajafahamika.

Alisema marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni 26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Hata hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na taarifa rasmi atazitoa leo.

Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Taarifa zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha, ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.

Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa  zaidi leo. 

Alisema, baada ya kumuua mke wake, Rashid alimnyonga mtoto wake wa miezi minne na kukimbia.

Kamanda Selemani, alisema baada ya kukimbia Rashid aliamua kutaka kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za siri.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni mwanamke kumtuhumu mume wake kuwa ana uhusiano na mwanamke mwingine jambo lililomchukiza mwanaume huyo.


Habari Zilizopo Katika Magaeti Ya Leo Alhamisi ya January 5



Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani.....Ni Baada ya Serikali Kuwasilisha Notisi Ya Kupinga Dhamana yake Mahakama ya Rufaa

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi   alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga  Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.

Baada ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya  mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria kutoa uamuzi wa rufani hiyo.
ALHAMISI HII YA LEO 05/01/2016 ALHAMISI HII YA LEO 05/01/2016 Reviewed by RICH VOICE on Januari 05, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...