HABARI ZA LEO AUGUST 26 2016
FRIDAY 26/08/2016 NEWS AND SPORT
Majambazi
ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano hayo
kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.
Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.
Habari zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Polisi wameweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, wilayani Mkuranga ambapo magari yote yanayotoka na kuingia Dar yanapekuliwa.
Thursday, August 25, 2016
Mwakyembe Asema Jeshi la Polisi Liko Sahihi Kuzuia Mikutano ya Ndani ya Vyama Vya Siasa........Awataka Watanzania Wasishiriki Maandamano ya UKUTA
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amesema amri
ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya nje na ndani ya vyama vya
siasa ni halali ambayo kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote
cha siasa anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kutokufanya hivyo ni
kuvunja sheria za nchi.
Amesema
amri hiyo ni ya kudumu ambayo imelenga kuangalia na kufanya tathmini ya
hali ya nchi kutokana na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani
nchini ambavyo vimeanza kuonekana.
Dkt
Mwakyembe alikuwa akijibu swali kutoka kwa Kituo cha Televisheni cha
Taifa TBC 1 ambacho kilitaka kupata ufafanuzi kuhusiana na uhalali wa
kauli ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na ya hadhara kwa
vyama vya siasa nchini.
“Jeshi
la Polisi ni chombo halali cha cha dola kilichoanzishwa kisheria chenye
wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zake ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, na kuongeza kuwa uamuzi huo una lengo la kulinda
amani ya nchi na endapo kutakuwa na viashiria vya kutishia amani ya nchi
yetu lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe. Ni amri halali
na kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote nchini anapaswa kuitii
na kuizingatia na kwamba kwenda kinyume ni kukiuka sheria, ” alisisitiza Mhe. Mwakyembe.
Mhe.
Waziri amesema ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ila
wanatakiwa kutoa taarifa Polisi ili waweze kutoa ulinzi wakati wa
mkutano huo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaweza kuzuia mikutano
hiyo kwa sababu za kiusalama.
Mhe.
Waziri pia alisema sio kweli kuwa Mhe. Rais amezuia mikutano ya siasa,
bali alichofanya ni kudhibiti uendeshaji wa holela au huria wa shughuli
za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa na kuongeza kuwa Mhe.
Rais amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na
kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
“Mhe.
Rais hajapiga marufuku siasa, alichofanya ni kudhibiti uendeshaji
holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya
wanasiasa husika kuepusha shari na chuki na amefanya hivyo kutokana na
kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania na
taifa kwa ujumla wake. Kwa hatua hiyo Mhe. Rais hajafunga milango ya
majadiliano. Milango iko wazi na tulitegemea wenzetu wangekuja na njia
mbadala na kulizungumzia hilo badala ya kuitisha maandamano ya nchi
nzima," alisema.
Mhe
Mhe. Waziri amevitaka vyama vya upinzani nchini kukaa na kuzungumza na
Serikali na kuacha kufanya vitendo vya kutishia uvunjifu wa amani kama
kuitisha maandamano kwa nchi nzima.
“Njooni
tukae tuzungumze tupime ushauri wenu, hili ni taifa letu sote na
milango iko wazi, tuache kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani kama
ambavyo inavyoonekana nchini hivi sasa,” alisisitiza.
Amasema
Sheria ya Vyama vya siasa hairuhusu kufanyika kwa maandamano kwa nchi
nzima, kufanya hivyo ni kuchochea wananchi kuasi “civil disobedience” ni
kinyume cha sheria na serikali haiwezi kuivumilia hali hiyo.
Mhe.
Waziri ametoa wito kwa Watanzania wote kutoshiriki maandamano ya Ukuta
ambayo alisema hayatakuwa na tija kwa nchi bali kuleta vurugu katika
jamii........
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Friday, August 26, 2016
Godbless Lema Atiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) amekamatwa na polisi akiwa
nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro
amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge
huyo.
Jana
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa
Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa
ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
Waliokamatwa
na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally
Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi,
Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa
mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand
Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini
walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti
kituoni hapo leo Ijumaa.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Friday, August 26, 2016
RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu
Akizungumza
wakati wa kuaga miili ya askari watatu kati ya wanne wa Jeshi la Polisi
waliouawa wiki hii katika tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda alisema jambazi
atakapokutwa popote iwe msituni iwe wapi agongwe na apigwe.
Alisema
alipopata taarifa ya vifo vya askari hao wanne alifungua pazia za
madirisha nyumbani kwake na kuwaangalia askari wanaolinda na kulia kwa
uchungu na kwamba usiendelezwe ukichaa wa haki za binadamu kwani ni
uendawazimu ambao hauwezi kuvumilika.
“Kamanda
Sirro (Simon) mimi ndiyo mkuu wako wa mkoa nasema ukikamata hao watu
popote gonga, piga na watu wa haki za binadamu wakija waambie waje
kwangu, hatuwezi kukaa kwenye mkoa ambao haupo salama,” alisema
Makonda aliyedai hana maneno mazuri ya kusema kwa sababu hakuumbwa
kumfurahisha mtu, bali anafanya kazi ya Mungu na wakati wake ukiisha
ataondoka.
“Kama
kuna haki za binadamu nataka haki za askari wangu kwanza. Kama hao watu
wa haki za binadamu wapo nataka kuona wakiandamana kukilaani kitendo
hiki, ”alisema Makonda.
......................Friday, August 26, 2016
Mabasi Yaliyofungiwa Yaanza Kuachiwa
MABASI
yanayosafirisha abiria wanaokwenda mikoani yaliyofungiwa na Serikali
kwa kusababisha ajali yameanza kuruhusiwa kutoa huduma hiyo.
Mabasi
hayo yameruhusiwa baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu
na Majini (SUMATRA) na Wamiliki wa Mabasi ya Abiria (TABOA) kufikia
muafaka.
Makubaliano
hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yalilenga kuleta suluhu
kwa kuwataka TABOA kusimamisha mgomo wa mabasi uliopangwa kufanyika nchi
nzima Agosti 22 mwaka huu.
Zaidi
ya mabasi 60 ya kampuni tofauti yalifungiwa na Serikali baada ya kile
kilichodaiwa na serikali kwamba yalisababisha ajali kwa uzembe wao.
Wamiliki
wa mabasi hayo walikuwa wanahoji sababu ya SUMATRA kufungiwa leseni ya
usafirishaji kwa kampuni badala ya kupewa adhabu basi moja lililopata
ajali badala ya kufungiwa kampuni nzima.
Katibu
Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu jana alisema wamekubaliana mabasi ambayo ni
mazima yaliyofungiwa yaachiwe kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaweze
kuingia barabarani kutoa huduma ya usafirishaji.
“Tulikubaliana
na serikali ndani ya siku saba iwe imeyafungulia mabasi yetu mazima
kutegemeana na utaratibu wa ukaguzi yaendelee kutoa huduma kwa wananchi
na tayari serikali imeanza kuyaachia baadhi ya mabasi hayo,
“Baadhi
ya mabasi yaliyofungiwa ambayo yameachiwa kutoa huduma ni ya Mohammed
Trans, Mbazi, Kisbo Safari, City Boy, KVC, Wibonera na Kandahari”, alisema Mrutu.
Alisema
walikubaliana serikali iyakamate mabasi yote madogo nchini yanayofanya
safari za usafirishaji abiria mikoani bila ya kuwa na leseni ya biashara
hiyo.
Alisema
mabasi hayo yamekuwa kero kubwa kwa kugombania abiria na yanapokuwa
barabarani yanawachomekea madereva wa mabasi makubwa.
Pia aliomba idadi ya vituo vya polisi vya ukaguzi barabarani vipungue.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Friday, August 26, 2016
Polisi Yapambana na majambazi Mkuranga.....Difenda zaidi ya 16 Zipo Eneo la tukio Asubuhi hii
Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani asubuhi hii.
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yamefika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru yamefungwa kutokana na mapambano hayo.
26/08/2016 habari za leo za michezo ni pamoja na
KIMATAIFAAAAAAAAA
Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu
Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo
akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga.Nyota huyo huchambua soka katika Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport wakati wa Euro 2016.
Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani
...................
Ligi kuu za Ulaya kufaidi Ligi ya Mabingwa
Ligi nne kuu za mataifa ya
bara Ulaya zinazoongoza zitatengewa nafasi nne kila moja katika hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
kuanzia msimu wa 2018-19.
Ligi hizo ni za England, Ujerumani, Italia na Uhispania.Chini ya mfumo wa sasa, England, Ujerumani na Uhispania huwa na nafasi tatu, huku klabu zinazomaliza nambari nne ligini zikilazimika kucheza hatua ya muondoano wa kabla ya makundi.
Italia imekuwa na nafasi mbili pekee za uhakika, na nyingine moja ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi.
Mshindi wa ligi dogo ya Ulaya, Europa League, pia atahakikishiwa nafasi hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano wa Uefa Giorgio Marchetti, mpangilio wa Ligi ya Mabingwa hata hivyo utabaki vilevile.
Baada ya hatua ya kufuzu, klabu 32 zitapangwa katika makundi manane ya klabu nne ambazo zitapigania nafasi ya kuingia hatua ya muondoano ya klabu 16.
Aidha, wamekubali kutoa euro 20m (£17.1m) kumnunua mshambuliaji wa Deportivo La Coruna Perez, 27, aliyefunga mabao 17 kutoka kwa mechi 37 alizocheza msimu uliopita.
Ununuzi huo utapelekea kiasi cha pesa zilizotumiwa na Arsenal kuwanunua wachezaji kufika £100m tangu kumalizika kwa msimu uliopita.
Klabu hiyo imenunua kiungo wa kati Granit Xhaka, beki Rob Holding, mshambuliaji Takuma Asano na kiungo wa kati Kelechi Nwakali.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema si kweli kwamba hataki kutumia pesa kuwanunua wachezaji.
Hii ni baada ya kushurumiwa na baadhi ya wachezaji kwamba yeye huwa 'mchoyo sana' sokoni
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Klabu ya Nice nchini Ufaransa
imeeleza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli.
Mchezaji huyo wa miaka 26 amechezea
Liverpool mechi 28, na akawafungia mabao manne tangu anunuliwe na aliyekuwa
mkufunzi wa Liverpool Brendan ambaye alimtoa AC Milan kwa £16m mwaka 2014.
Mshambuliaji huyo ameambiwa na
meneja wa sasa Jurgen Klopp kwamba anaweza kutafuta klabu mpya.
Kufikia sasa hakuna mkataba uliotiwa
saini baina ya Nice na Liverpool, lakini Balotelli hakuhudhuria mazoezi ya
wachezaji wa Liverpool eneo la Melwood Alhamisi.
Balotelli, ambaye pia amefanya
mazungumzo na klabu ya FC Sion ya Uswizi alikaa AC Milan kwa mkopo msimu
uliopita ambapo aliwafungia bao moja Serie A.
Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa Alhamisi jioni.
Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.
Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.
Samatta pia alioneshwa kadi ya manjano dakika ya 69.
Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadaye leo Ijumaa mwendo wa saa tisa saa za Afrika Mashariki
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Polisi Brazil wamemshtaki muogeleaji wa Marekani Ryan Lotche
Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela.Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lotche atatakiwa kujibu mashtaka hayo. Idara ya marekani imesema inatambua ombi hilo.
Lotche ameondoka Brazil kabla hajahojiwa na polisi. Ameomba msamaha kwa kusema uongo juu ya kuibiwa. Lotche amepoteza wadhamini wake wakubwa wanne kufuatia tukio hilo na hivyo kuweka hatarini kazi yake ya uogeleaji
NANI KAMA CRISTIANO RONALDO….NDIE MCHEZAJI BORA ULAYA!
MCHEZAJI wa Real Madrid na Kepteni wa Timu ya Taifa ya Portugal, Cristiano Ronaldo, ametwaa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.Ronaldo aliwabwaga Gareth Bale, ambae wanacheza wote Real Madrid, na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kwenye Kura ambazo zimepigwa na Wanahabari maalum kutoka Nchi zote 55 Wanachama wa UEFA.
Hii ni mara ya Pili kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii.
Ronaldo alikuwa na Msimu mzuri wa 2015/16 akivuka Bao 50 kwa mara ya 6 mfululizo, yaani Miaka 6, katika Msimu mmoja akiichezea Real Madrid.
Kwenye UCL, Ronaldo aliibuka Mfungaji Bora akifikia Rekodi ya Bao 16 na Penati yake ndio iliipa ushindi Real kuibwaga Atletico katika Fainali kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano na kutwaa Ubingwa huko Milan.
Akiwa na Portgugal huko EURO 2016, Ronaldo alifunga Bao 3 na kutoa msaada mara 2 wakitwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza katika Historia yao.
Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011, 2015), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).
................................
EUROPA LIGI -MAKUNDI: MAN UNITED NA FENERBAHCE, FEYENOORD, ZORYA, GENK YA SAMATTA NA BILBAO, VIENNA NA GIURGIU!
DROO ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI imefanyika hii Leo huko Monaco na Makundi 12 ya Timu 4 kila moja yamepatikana.Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Septemba 15.
DROO KAMILI:
KUNDI A: Manchester United, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya
KUNDI B: Olympiacos, Apoel, Young Boys, FC Astana
KUNDI C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
KUNDI D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Haifa, Dundalk
KUNDI E: Viktoria Pizen, AS Roma, Vienna, Astra Giurgiu
KUNDI F: Athletic Bilbao,KRC Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
KUNDI G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
KUNDI H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
KUNDI I: Schalke, Salzburg, Krasnodar, Nice
KUNDI J: Fiorentina, PAOK, Slovan Liberec, Qarabag
KUNDI K: Inter Milan, Spata Praga, Southampton, Hapoel Be’er Sheva
KUNDI L: Athletic Bilbao, Steau Bucharest, FC Zurich,
EUROPA LIGI -MAKUNDI: MAN UNITED NA FENERBAHCE, FEYENOORD, ZORYA, GENK YA SAMATTA NA BILBAO, VIENNA NA GIURGIU!
DROO ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI imefanyika hii Leo huko Monaco na Makundi 12 ya Timu 4 kila moja yamepatikana.Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Septemba 15.
DROO KAMILI:
KUNDI A: Manchester United, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya
KUNDI B: Olympiacos, Apoel, Young Boys, FC Astana
KUNDI C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
KUNDI D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Haifa, Dundalk
KUNDI E: Viktoria Pizen, AS Roma, Vienna, Astra Giurgiu
KUNDI F: Athletic Bilbao,KRC Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
KUNDI G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
KUNDI H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
KUNDI I: Schalke, Salzburg, Krasnodar, Nice
KUNDI J: Fiorentina, PAOK, Slovan Liberec, Qarabag
KUNDI K: Inter Milan, Spata Praga, Southampton, Hapoel Be’er Sheva
KUNDI L: Athletic Bilbao, Steau Bucharest, FC Zurich
MAZEMBE KUMENYANA NA ETOILE DU SAHEL NUSU FAINALI AFRIKA
RATIBA NUSU FAINALI LIGI YA
MABINGWA
Sept 16-18, 2016
Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)
Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
RATIBA NUSU FAINALI KOMBE LA
SHIRIKISHO
Sept 23-25, 2016
TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)
MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco)
TIMU za Kusini mwa Afrika zitamenyana zenyewe kwa zenyewe
katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama itakavyokuwa kwa timu za
Kaskazini mwa Bara kuelekea kwenye kinyang'anyiro cha dola za Kimarekani
Milioni 1.5 na tiketi ya kucheza Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan.
Mabingwa mara tano barani, Zamalek ya Misri watamenyana
na vigogo wa Morocco, Wydad Athletic kuwania tiketi ya Fainali, wakati Zesco
United ya Zambia itamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Timu za Kusini mwa Afrika zimefuzu pasipo kutarajiwa
hususan Zesco, ambayo ilikuwa kundi moja na mabingwa watatu wa zamani, Al Ahly
ya Misri, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Wydad.
Wakiwa wanakwenda Nusu Fainali kwa mara ya pili tu, Zesco
inatarajiwa kuitoa Sundowns, iliyofungwa katika fainali miaka 15 iliyopita.
Kwa Zamalek, hii inaakuwa mara ya kwanza kufika Nusu
Fainali tangu mwaka 2005, wakati Wydad walifika hatua hiyo kwa mara ya mwisho
mwaka 2011, kabla ya kufungwa na Esperance ya Tunisia kwenye fainali.
Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya
Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23 na
25.
Na katika Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC itamenyana
na Etoile du Sahel ya Tunisia wakati MO Bejaia ya Algeria itamenyana
na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali.
Mechi za kwanza pia zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya
Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23 na
25.
kimataifa tuanze na
Baada
ya Yanga kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kocha wa timu hiyo, Hans
van Der Pluijm, ameeleza kuwa anataka kurejesha furaha kwa mashabiki wa timu
yake kwa kuifunga African Lyon na kuchukua pointi zote tatu katika mchezo wao
huo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, keshokutwa Jumapili.
Kocha
huyo raia wa Uholanzi amesema anafahamu wana muda mchache wa maandalizi ya
mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam lakini hiyo
haitawasumbua kwa kuwa tayari walishafanya maandalizi hayo kwa kutumia baadhi
ya michezo ya kimataifa.
“Nafahamu kuwa mashabiki wanahitaji furaha na hakuna njia nyingine ya kuirejesha zaidi ya kuanza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
"Tumetolewa
katika michuano ya kimataifa, hii ina maana kwamba moja kwa moja tunaelekeza
akili na nguvu zetu ligi kuu, ushindi ni lazima.
“Kwa
sasa tumebakiza siku chache za maandalizi lakini hiyo haitasumbua sana kwa kuwa
tulishaanza maandalizi kwa kutumia mazoezi na mechi za michuano ya kimataifa.
Wachezaji wengi tuliowakosa hivi karibuni, wameanza kurejea na mpaka siku hiyo,
tutakuwa kamili,” alisema Pluijm.
Aidha,
Pluijm aliongeza: “Mara baada ya kumaliza mechi ya mwisho dhidi ya TP Mazembe,
nilifanya kikao na wachezaji kwa ajili ya kuwatengeneza kisaikolojia ili
tutakaporejea kwenye ligi kuu, turudi na nguvu zote katika kulitetea taji hilo.
“Hivyo,
hatutaki utani wala kudharau timu yoyote inayoshiriki ligi kuu, zikiwemo
zilizopanda daraja, tuhakikishe tunautetea ubingwa wetu tunaoshikilia.”
............................
Kocha
wa African Lyon, Mreno, Bernardo Teveras, ameibuka na kusema kuwa anahitaji
matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga
kwa kuwa alishawaona walipocheza na Azam FC, hivi karibuni.
Mreno
huyo amechukua nafasi ya kocha wa zamani wa Simba aliyekuwa akiinoa timu hiyo,
Dragan Popadic raia wa Serbia aliyeondoka nchini kutokana na madai ya vyeti
vyake kuwa ni vya kizamani na havifai katika soka la sasa.
Tavares
amesema kuwa kwa sasa akili yake ameielekeza katika mchezo dhidi ya Yanga kwa
ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika ligi.
“Tulikuwa
na wakati mzuri katika mchezo wetu dhidi ya Azam, japokuwa wapinzani wetu
walipata nafasi ya kusawazisha dakika za mwisho, kwa sasa mipango yangu
naielekeza katika mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga kwani nahitaji ushindi kutoka
kwao.
"Uzuri
ni kwamba Yanga tayari nimeshawaona walipocheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi
ya Azam kwani ni timu nzuri na ya gharama, lakini ninachokitaka ni ushindi pekee
licha ya muda mchache ambao nimekaa nayo ila imani yangu ni kuwafunga tu,
hakuna kingine," alisema Tavares.
African
Lyon ilionyesha soka safi na kuibana Azam FC katika mechi ya ufunguzi wa Ligi
Kuu Bara iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Katika
kuhakikisha inakuwa na kikosi bora siku zijazo, uongozi wa Klabu ya Azam
umeanzisha mkakati wa kusaka vipaji vya vijana chini ya umri wa miaka 17
unaotarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, mwaka huu wakianza na Mkoa wa Dar es
Salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine.
Msemaji
wa Azam, Jaffar Idd ambaye timu yake inaongozwa na nahodha John Bocco, amesema
mpango umekamilika ingawa mpango mzima utaanza Agosti 28 wakianza na Wilaya za
Kigamboni na Temeke kwenye Uwanja wa Chamazi.
Septemba
3, mwaka huu majaribio yatakuwa kwa Wilaya ya Ilala ambapo zoezi la ung’amuzi
wa vipaji hivyo litakuwa kwenye Viwanja vya JMK kabla ya kuhamia kwenye Uwanja
wa Kawe Septemba 10 kuhusisha Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuhamia katika mikoa
mingine kama Zanzibar, Tanga, Morogoro, Arusha, Mwanza na Kigoma.
“Muhimu
ni kila mzazi kuja na mwanaye siku ya kuwajaribu kwa ajili ya kupata taarifa za
kina juu ya mtoto wake,” alisema Idd.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Wabunge
wa vyama mbalimbali ambao ni mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba, leo
wametoa msimamo wao kuhusiana na ombi la mfanyabiashara Mohammed Dewji kutaka
kuinunua klabu ya Simba kwa asilimia 51.
Wabunge hao wakiwemo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walitoa msimamo wao walipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, leo.
Mo
Dewji ametenga kitita cha Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 za klabu
hiyo.
Wabunge
hao wakiongozwa na Juma Ngamia, Adam Malima na Profesa Jay wamesema wanaamini
hilo ni jambo zuri.
Wamesisitiza
Simba inachotakiwa ni kuangalia huu ni wakati mwafaka wa maendeleo na
mabadiliko ambayo yatakuwa na tija.
Wamewataka
Wanasimba kutoa ushirikiano katika suala hilo la Mo Dewji ili kuisaidia klabu
hiyo kubadilika baada ya kuwa imesota miaka minne sasa bila ya ubingwa wala
kucheza michuano ya kimataita.
Mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa wakiunga kwa nguvu kuhusiana na Mo Dewji kununua hisa hizo ili kuchangia mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
Katika mkutano wa wanachama hivi karibuni, wanachama waliucharukia uongozi wakitaka upitishe mabadiliko hayo ili Simba itoke kwenye wimbi la kuwa msindikizaji na kurejesha heshima yake.
............................Mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa wakiunga kwa nguvu kuhusiana na Mo Dewji kununua hisa hizo ili kuchangia mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
Katika mkutano wa wanachama hivi karibuni, wanachama waliucharukia uongozi wakitaka upitishe mabadiliko hayo ili Simba itoke kwenye wimbi la kuwa msindikizaji na kurejesha heshima yake.
Taifa Stars mpya kuivaa Nigeria mechi ya AFCON 2017
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
Timu itaingia kambini Agosti 28, kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo.
Makipa
- Deogratius Munishi - Young Africans
- Aishi Manula - Azam FC
- Kelvin Yondani - Young Africans
- Vicent Andrew - Young Africans
- Mwinyi Haji - Young Africans
- Mohamed Hussein - Simba SC
- Shomari Kapombe - Azam FC
- David Mwantika - Azam FC
- Himid Mao - Azam FC
- Shiza Kichuya - Simba SC
- Ibrahim Jeba - Mtibwa Sugar
- Jonas Mkude - Simba SC
- Muzamiru Yassin - Simba SC
- Juma Mahadhi - Young Africans
- Farid Mussa Tenerif ya Uhispania
- Simon Msuva - Young Africans
- Jamal Mnyate - Simba SC
- Ibrahim Ajib - Simba SC
Mbwana Samatta - KRC Genk ya Ubelgiji.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Ivory Coast kuivaa Tanzania soka ya ufukweni
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, zitarudiana tena Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kwa upande wa Tanzania, Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu, anaendelea na mazoezi na ameahidi watafanya vizuri katika mchezo huo.
Wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.
Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
........................
HABARI ZA LEO AUGUST 26 2016
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 26, 2016
Rating:
Hakuna maoni