Saturday, August 27, 2016
Paul Makonda aitwa Tume ya Haki za Binadamu Kujieleza.....Ni kwa kauli yake aliyotoa Agosti 25 Akiwataka Polisi Wawapige Watu Wakiwakuta Msituni
Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi
ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi
ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili
ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26,
2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu
ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume
ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi
wa haki za binadamu.
Aidha,
Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la
Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa
Mkoa.
Kwa
mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a)
vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya
Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu
au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka
ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Saturday, August 27, 2016
Mkutano wa Baraza la Vyama Vya Siasa Ulioitishwa Kutafuta Suluhu ya Oparesheni UKUTA Wasogezwa Mbele hadi Septemba 3 na 4
Baraza
la Vyama vya Siasa nchini limesogeza tarehe ya mkutano wa kutafuta
suluhu ya operesheni Ukuta iliyotarajiwa kufanyika Septemba 1,2016
,kutoka Agosti 30 hadi Septemba 3 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa
baraza hilo Vuai Ally Vuai alisema mkutano huo umesogezwa hadi tarehe 3
na 4 Septemba,2016.
“Kamati ya uongozi leo tumekutana tena ili kufanya maandalizi ya mkutano tuliopanga kuufanya tarehe 30 na 31 mwezi huu.
“Tumepitia
list (orodha) ya wahudhuriaji, tumegundua siku zilizobaki kufikia
mkutano zisingetosha . Tumeamua kuusogeza mbali hadi tarehe 3 na 4,
Septemba mwaka huu ili mkutano uwe wa ufanisi,” alisema Vuai.
Aidha,
baadhi ya agenda zilizotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo ni
masuala ya amani na utulivu nchini pamoja na hali ya siasa kwa sasa.
Waandishi
wa habari walipohoji kwa nini baraza hilo lisifanye mkutano huo katika
tarehe zilizopangwa awali ili kutoa nafasi kwa wajumbe kujadili suala la
operesheni Ukuta ambayo imezua mabishano makali ya kisheria na kikatiba
kati ya serikali na Chadema, Cons Akitandi, Mwenyekiti wa fedha wa
baraza hilo alisema “kwanza ifahamike hatukutani kwa ajili ya Septemba
Mosi.”
“Upo
utaratibu wa kikanuni kwamba baraza lina vikao vya kila baada ya miezi
mitatu na vikao vya dharula. Haki haitapatikana katika mazingira ya
shari, wajumbe wanapaswa kutumia njia ya majadiliano na maridhiano
katika kufikia mwafaka,” alisema Akitandi.
.......................
HABARI ZA KIMATAIFA
Polisi wakabiliana na waandamanaji wa Upinzani Zimbabwe
Makabiliano yalichacha pale waandamanaji walipoamua kujibu mashambulio ya polisi kwa kuwarushia mawe na kuchoma mataili ya magari.
Kiongozi wa upinzani Joice Mujuru amesema kuwa zaidi ya watu hamsini wamejeruhiwa.
Makundi ya upinzani yaliandaa maandamani kushinikiza mageuzi ya sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.
Robert Mugabe --mwenye umri wa miaka 92 anasema anatarajia kugombea kiti hicho.
Kumekuwa na ongezeko la idadi ya maandamano ya upinzani dhidi ya serikali nchini Zimbabwe.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Marekani na Urusi zapiga hatua kuelekea usitishaji mapigano Syria
Marekani na Urusi zimefikia hatua muhimu kuelekea makubaliano mapya ya kusitisha mapigano nchini Syria, lakini hatua ya mwisho ya mpango huo bado haijafikiwa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na mwenziwe wa Urusi Sergei Lavrov baada ya kufanya mazungumzo ya saa nyingi mjini Geneva Uswisi. Waziri Kerry amesema wamebainisha mambo muhimu katika njia ya kusonga mbele, kuelekea usitishaji wa uhasama, na kuongeza kuwa vizingiti vikubwa kuhusu usimamishaji mapigano vimeondolewa, japo bado yapo masuala kadhaa ambayo hayajapatiwa muafaka. Lavrov kwa upande wake aliunga mkono aliyosema mwenziwe kwa kuwaambia waandishi habari kuwa hatua muhimu zimefikiwa katika mpango wa kuzifikisha kikomo vurugu. Marekani na Urusi zinaunga mkono pande zinazokinzana katika mgogoro wa Syria, ambao ulianza Machi 2011 baada ya Rais Bashar al-Assad kufanya ukandamizaji dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakidai demokrasia....................
Nchi za Ulaya ya Kati zataka jeshi la pamoja la Ulaya
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekutana na viongozi wa Hungary, Jamhuri ya Czech, Poland na Slovakia, ambao wanataka kuwepo kwa jeshi la pamoja la nchi za Umoja wa Ulaya. Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na mwenzake wa Jamhuri ya Czech Bohuslav Sobotka, wamesisitiza umuhimu wa mradi huo katika kuhakikisha usalama wa Umoja wa Ulaya. Pendekezo hilo la viongozi wa mataifa ya Ulaya ya Kati limekuja wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu kitisho cha ugaidi, kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi walioingia katika eneo hilo wakitokea Mashariki ya Kati. Kansela Merkel hakukubaliana moja kwa moja na pendekezo hilo, lakini ameafiki kuwa usalama ni suala la msingi. Vile vile ametoa wito wa kuwepo juhudi mpya za kuimarisha uchumi wa Ulaya.//////
Waliokufa katika tetemeko Italia wafikia 281
Idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi katika eneo la katikati ya Italia imefikia watu 281, wakati timu za uokozi zikionesha kuishiwa na matumaini ya kupata manusura wengine na mazishi ya kwanza ya waliokufa yakifanyika. Mapema Alhamis, tetemeko la ukubwa wa 6 kwenye kipimo cha richter lilikumba eneo la milima kati ya mikoa ya Umbria, Lazio na Marche, na kusababisha mamia ya watu kukwama katika kifusi, kwenye manispaa tatu tofauti, umbali wa kilometa 150 kaskazini-mashariki mwa Roma. Kwa mujibu wa shirika la ulinzi wa raia la Italia- Protezione Civile kiasi ya watu 221 wamekufa mjini Amatrice, 49 wamepoteza maisha katika mji wa Arquata del Tronto na katika mji wa Accumoli ni 11 waliofariki
...................
Wajumbe wa Baraza la Usalama kwenda Juba
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga kwenda Sudan Kusini wiki ijayo kwa lengo la kumshawishi Rais Salva Kiir kukubali kuruhusu kuingia kwa jeshi jipya la kikanda nchini humo au akabiliane na vikwazo vya silaha. Mabalozi kutoka mataifa wanachama 15 wamepangiwa kusafiri kuanzia Septemba 2 hadi 7 kwa ajili ya mikutano ya kupendekeza kupelekwa jeshi madhubuti la wanajeshi 4,000 mjini Juba kwa ajili ya kuwaongezea nguvu walinzi wa amani walio katika mpango wa Umoja wa Mataifa. Mpango huo, ujulikanao kama UNMISS, unakabiliwa na ukosoaji mkali kwa kushindwa kwake kuwalinda raia, wakiwemo idadi kubwa ya wanawake na wasichana ambao wamekuwa wakibakwa karibu na kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, baada ya kuzuka vurugu katika mji huo mkuu mapema Julai..........................
Mahakama Ufaransa yaondosha marufuku ya Burkini
Mahakama ya juu ya kiutawala nchini Ufaransa imeondosha kwa muda marufuku ya vazi la kuogelea la aina ya burkini linalovaliwa na wanawake wa kiislamu, lenye kufunika mwili wote kama inavyotakiwa na dini yao. Uamuzi huo umetokana na malalamiko ya wengi kupinga uamuzi wa miji kadhaa ya Ufaransa kupiga marufuku vazi hilo la kuogelea. Vazi la burikini limezusha mjadala mkubwa nchini humo kwa Waislamu, wakati Ufaransa ikikabiliwa na mrorongo wa matukio mabaya ya kigaidi yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Manuel Valls amesema taifa lake linakabiliwa na vita vya utamaduni na kwamba burkini inawakilisha utumwa kwa wanawake. Makundi ya haki za binaadamu kwa upande wao wanasema marufuku ya burkini inakiuka haki za msingi za binaadamu.'''''''CHANZO CHA HABARI HIZI NI DW HABARI ZA NULIMWENGU PAMOJA NA BBC SWAHILI
KATIKA HABARI ZA MICHEZO NI PAMOJA NA
EFL CUP: DROO RAUNDI YA 3 YAFANYWA, NORTHAMPTON KUIVAA MAN UNITED, LEICESTER v CHELSEA, SWANSEA v MABINGWA CITY!
DROO ya Raundi ya 3ya EFL CUP, Kombe la Ligi ya England ambalo kwa Miaka Minne lilikuwa likiitwa Capital One Cup kutokana na udhamini wa Capital One, imefanyika Jana mara baada ya kukamilika Raundi ya Pili.
Timu ya Daraja la chini Northampton Town watakuwa Nyumbani kuwakaribisha Vigogo Manchester United wakati Mabingwa wa Ligi Kuu England Leicester wakiwa kwao King Power Stadium kuivaa Chelsea na hilo ni moja ya mapambano Manne ya Timu za Ligi Kuu England pekee.
Mengine ni Southampton na Crystal Palace, Swansea na Mabingwa Watetezi Manchester City na Hull City kusafiri kwenda Stoke City.
Gillingham, ambao waliwatoa Watford Raundi ya Pili, watasafiri kwenda White Hart Lane kucheza na Tottenham.
Nao Nottingham Forest, wanaocheza Daraja la Championship, watakuwa Wenyeji wa Arsenal.
DROO KAMILI – Raundi ya 3:
**Mechi kuchezwa kwenye Wiki ya kuanzia Septemba 19
Nottingham Forest vs Arsenal
Leeds United vs Blackburn Rovers
Queens Park Rangers vs Sunderland
West Ham vs Accrington Stanley
Southampton vs Crystal Palace
Swansea vs Manchester City
Fulham vs Bristol City
Bournemouth vs Preston North End
Tottenham vs Gillingham
Everton vs Norwich City
Derby County vs Liverpool
Northampton vs Manchester United
Brighton vs Reading
Newcastle United vs Wolverhampton Wanderers
Stoke City vs Hull City
Leicester City vs Chelsea
+++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhanini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
+++++++++++++++++++++++++
Klabu za Ligi Kuu England ambazo ziko kwenye Mashindano ya Klabu Ulaya, yale ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI, zinaanza hii Raundi ya 3 ya EFL CUP wakati nyingine zilitokea Raundi ya Pili.
Klabu hizo ni Arsenal, Leicester City, Manchester City, Manchester United, Southampton, Tottenham Hotspur na West Ham United
............
VPL: LEO TAIFA SIMBA-JKT RUVU, CHAMAZI AZAM-MAJIMAJI, JUMAPILI MABINGWA YANGA DIMBANI NA LYON!
LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Agosti 27
JKT Ruvu v Simba
Mtibwa Sugar v Ndanda FC
Azam FC v Majimaji
Tanzania Prisons v Ruvu Shooting
Mbao FC v Mwadui FC
Kagera Sugar v Mbeya City
++++++++++++++++++++++
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, VPL, kwa Msimu mpya wa 2016/17 inaendelea Leo kwa Mechi 6 na kesho Jumapili Mabingwa wake Yanga kuanza utetezo wao.
Leo huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Simba watacheza na JKT Ruvu wakati huko Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC watakipiga na Majimaji.
Huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar watacheza na Ndanda FC wakati huko Sokoine, Mbeya ni Tanzania Prisons na Ruvu Shooting na huko Kirumba Mwanza ni Mabao FC na Mwadui FC.
Stand United wapo kwao Kambarage, Shinyanga kuivaa Kagera Sugar.
Kesho Jumapili zipo Mechi 2 ambapo Mabingwa Watetezi wa VPL, Yanga, wataanza utetezi wao Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kuivaa African Lyon na huko Mwanza ni Toto Africans v Mbeya City.
Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroun, Joseph Marius Omog, walianza Ligi Wikiendi iliyopita kwa kuipiga Ndanda FC 3-1 wakati Azam FC, chini ya Kocha kutoka Spain, Hernandez, walitoka 1-1 na African Lyon.
LIGI KUU VODACOM
Jumapili Agosti 28
Yanga v African Lyon
Toto Africans v Mbeya City
......
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 26, 2016
Rating:
Hakuna maoni