habari za alhamisi hii

 .

 .

 

Thursday, January 12, 2017

Dr. Shein: Sina Ugomvi na Maalim Seif na wala Sikushinikiza ZEC Ifute Matokeo

Wakati Wazanzibari leo wakiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein (pichani), amebainisha kuwa mapinduzi hayo ndio alama, sifa, ukombozi na uhuru wa raia hao wa visiwa vya Zanzibar.

Dk Shein amesema hana ugomvi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi na kubainisha kuwa wanatofautiana kisiasa, ni jambo la kawaida na mazungumzo ya muafaka yalishafanyika.

Pamoja na hayo, Rais huyo amebainisha kuwa anaamini amechaguliwa kihalali na Wanzanzibari, ambapo kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, hakukuwa na shinikizo lolote kutoka serikalini bali ni maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kubaini mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza katika kipindi cha Funguka kilichorushwa na Azam TV jana usiku, Dk Shein alisema kilichohitajika ni mazungumzo ya pande mbili ambayo yalifanyika baina yao na mwelekeo ulikuwa mzuri lakini Maalim Seif hakutaka kurudia uchaguzi. 

Mvutano huo ulijitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo hayo na kusababisha mvutano wa kisiasa kabla ya kutangaza kurudiwa Machi 20, 2016, ambao CUF iligoma kushiriki.

Katika mahojiano hayo, Dk Shein alisema, “Mimi nilikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yale na Maalim upande wa pili huku wajumbe wakiwa marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Aman Karume na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd. 

“ZEC ni tume huru na inayojisimamia kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Zanzibar, taasisi yoyote haiwezi kuiingilia hata kama ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ndiyo maana wao (NEC) hawakuona dosari katika uchaguzi lakini ZEC waliziona na kutoa sababu tisa za kufuta uchaguzi,” alisema Dk Shein.

 Alisema uchaguzi wa Zanzibar umekuwa na matatizo tangu mwaka 1957 na wa awamu hii, Tume ilikuwa na hoja za msingi kuurudia huku akisema mwenyekiti wa Tume anateuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba na si kwa ajili ya kumpendelea. 

Changamoto za Muungano 
Dk Shein alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa katika kudumisha Muungano na changamoto zake pekee anazozitambua ni tume ya pamoja ya fedha na suala la mafuta ambalo limepatiwa ufumbuzi. 

“Kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kelele za Muungano na muundo wa Serikali hazikuwahi kusikika lakini baada ya baadhi ya wanaCCM kuenguliwa na kuhamia upande wa pili, ndiyo walioanza kuwalisha watu sumu. Lakini anayeupinga Muungano haijui asili yake,” alisema Dk Shein. 

Mchakato wa Katiba 
Alipoulizwa kuhusu Katiba mpya baada ya Rais John Magufuli kusema hicho si kipaumbele chake, Dk Shein alisema hayo ni masuala ya kushauriana baina ya viongozi hao wawili.

“Mchakato wa Katiba tuliuanza mimi na Jakaya Kikwete (Rais mstaafu) na ile Katiba ni ya Muungano, hivyo jambo lolote ni lazima viongozi wa Serikali mbili washauriane. Mambo haya si ya kulazimisha...,” alisema.

 Uongozi wa Magufuli
 Rais huyo alisema anamfahamu Rais Magufuli tangu akiwa waziri na anajua uwezo wake, “Majipu anayoyatumbua Rais habahatishi kwani anafanya vile kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, na si kwamba mimi situmbui, natumbua sana, sema mimi staili yangu siyo ya kusema kila kitu na waandishi wa huku (Zanzibar) si wafuatiliaji sana kama wa Bara,” alisema Dk Shein. 

Aliongeza kuwa watu hawawezi kujua utumbuaji wake kama waandishi wa habari si wafuatiliaji, vilevile hawezi kuyajua majipu zaidi kama waandishi wa habari hawajayaibua, “Waandishi wa habari wa Zanzibar ni tofauti sana na wa Bara.” 

Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli kuwa awe mkali, Dk Shein alisema, “Kwa kuzungumza mimi ni mpole lakini mtu akikosea, mimi ni mkali kwelikweli, sema mimi siyo mtu wa kukasirika ovyo, busara zinaniongoza sana, japokuwa ukikosea sikuachi hata kidogo,” alisema Dk Shein. 

Alisema katika kipindi chote ambacho amekaa madarakani, anajivunia kuifanyia Zanzibar mambo mengi na bado anaendelea. 

“Katika utawala wangu nimeanzisha mpango wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari, sasa wazazi wanachangia ada ya mitihani tu ya kidato cha nne na cha sita na yenyewe muda si mrefu nitaiondoa,” alisema Dk Shein. 

Kuhusu afya, alisema licha ya Wazanzibari wengi kutibiwa nje ya visiwa hivyo kwa madai ya kukosekana kwa huduma bora, Serikali yake imeongeza vituo vya afya kutoka 31 hadi 154, ingawa bado kuna changamoto ya wataalamu.

 Dk Shein aligusia suala la mrithi wake akisema yeyote atakayeonesha nia kupitia CCM kwa wakati huu, atakuwa anakosea licha ya kwamba huu ndiyo muhula wake wa mwisho. 

“Hata kama namfahamu mtu ambaye naona anafaa, siwezi hata kumnong’oneza mpaka pale atakapopitishwa na chama,” alisema Dk Shein
 
 

WAFANYAKAZI BENKI YA POSTA TANZANIA TAWI LA MBEYA WASHEREKEA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI KITUO CHA AFYA KIWANJA MPAKA

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar 


Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo hicho cha Afya .

Zoezi la usafi likiendelea

Erick Mwaigomole Mfanyakazi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya akishiriki kikamilifu shughuli za usafi katika kituo cha Afya Kiwanja Mpaka jijini Mbeya kama sehemu ya kusherekea Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.

Zoezi la Usafi likiendelea........

WAZIRI MKUU AZINDUA SACCOS YA MELINNE

 

COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI,VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

MH. MAJALIWA AFUNGUA UKUMBI WA SACCOS YA MELI NNE, ZANZIBAR NA KUZUNGUMZA

Waziri Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati alipozungumza baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar Januari 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar Januari 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo Januari 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar Januari 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 

Picha: Rais Magufuli asafiri kwa gari toka Chato hadi Simiyu kwenye ziara ya kikazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyamikoma Wilayani Busega wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Magu mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita.

Picha: Rais Magufuli Awasili Bariadi Mkoani Simiyu, Aweka Jiwe La Msingi Hospitali Ya Rufaa Ya Simiyu .......Pia Afungua Barabara Ya Bariadi-lamadi (Km 71.8)



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za asili pamoja na kikundi cha Ngoma za asili Baseki cha Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za asili pamoja na kikundi cha Ngoma za asili Baseki cha Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua rasmi barabara hiyo la Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka kabla ya kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi na kuwahutubia wananchi wa mkoa huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka wakati vikundi vya kwaya mbalimbali vilipokuwa vikitumbuza Bariadi mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya nguzo katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.


Rais Magufuli Akerwa Na Wanasiasa Wanaodai Tanzania Kuna Njaa



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi

Dakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika  Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.

'' Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchi kwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa'' 

Akizungumzia gharama za  ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu, Rais Magufuli ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi na Wakala wa majengo nchini TBA kukaa na kurejea gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo wa Shilingi Bilioni 46 kuwa hauendani na hali halisi ya aina ya jengo linalotakiwa kujengwa.Rais Magufuli ametoa Shilingi bilioni 10 ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo.

''Haiwezekani  majengo ya ghorofa ishirini lijengwe kwa shilingi Bilioni Kumi wakati jengo la ghorofa moja moja lijengwe kwa gharama ya shilingi Bilioni 46''

Rais Magufuli pia ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu kuendelea na ujenzi wa mradi wa tenki la maji katika mlima Ngasamo ili wananchi wa mkoa wa Simiyu ikiwemo wilaya ya Bariadi kupata huduma ya maji badala ya kukwama kutokana na mwekezaji mmoja kutaka kuchimba madini ya Nikeli katika mlima huo.

Amesema haiwezekani wananchi zaidi ya milioni moja wakose maji kutokana na mwekezaji mmoja ni kukosa muelekeo na kumkosea Mwenyezi Mungu kitu kisichokubalika hivyo Waziri wa Nishati na Madini afute leseni ya mwekezaji huyo ili wananchi wa Simiyu wapate huduma ya maji.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla kutumia mvua chache zinazonyesha kulima mazao yanayostahamili ukame kama vile Mtama,viazi na Uwele ili kuweza kujikimu kwa chakula badala ya kutegemea chakula cha msaada kutoka Serikali.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Simiyu
11 Januari, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya January 12






NEC: Mbunge Peter Lijualikali kuendelea kuwa mbunge licha ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela



Mjadala umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Imeelezwa  kuwa kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan ameibuka na kukata kiu ya wananchi ya kutaka kujua endapo  baada ya hukumu hiyo Mhe. Lijualikali ataendelea kuwa mbunge.

Akihojiwa na TBC One wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili jana usiku,  Bw. Kailima aliweka bayana kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela.

"Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka  madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake", alisema Bw. Kailima.


Daktari Akwamisha Kesi Ya Scorpion

Ushahidi katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi  inayomkabili, Salum Njwete (34) maarufu Scorpion, umeshindwa kuendelea baada ya upande wa Jamhuri kudai shahidi  hakufika.

Sababu za kutofika kwa shahidi huyo ambaye  ni  daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ni kutokana na kuwa nje ya kituo chake cha kazi hivyo hakupatikana   jana.

Mshitakiwa Scorpion alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi upande wa Jamhuri.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai upande wa Jamhuri ulipanga kumhoji  shahidi ambaye ni daktari lakini kwa vile alikuwa  na dharura ingefaa mahakama impangie tarehe nyingine.

“Mheshimiwa hakimu shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa Jamhuri ulipanga kumleta shahidi ambaye ni daktari lakini ameshindwa kufika leo, ana dharura ambayo inaweza ikachukua wiki tatu.

“Hivyo kwa mujibu wa kifungu namba 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi ya Makosa ya Jinai ambayo inataka kesi isiahirishwe zaidi ya wiki mbili kama mshitakiwa yuko mahabusu,   tunaomba mahakama itaje hapa  tupange tarehe ya kusikilizwa,’’alisema.
habari za alhamisi hii habari za alhamisi hii Reviewed by RICH VOICE on Januari 12, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...