Mzee Majuto kupelekwa India leo
Msanii
wa filamu bongo Mzee Majuto leo Mei 1, 2018 anatarajiwa kusafiri na
kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo
aliyopata siku kadhaa zilizopita.
Steve
Nyerere ambaye amehusika kwa namna moja au nyingine katika kusaidia
kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa
matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo Mzee huyo atakwenda kwa
matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao wamehusika katika
kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.
"Niseme
ahsante sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy
Mwalimu na wadau pamoja na wasanii mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee
wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa njiani kwenda India kwa
matibabu zaidi"
Steve
Nyerere hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii
wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na
bima ya afya na kusema ni mkombozi kwao, anadai haiwezekani miaka nenda
rudi wakawa ni watu wa kuombaomba kila wakati pindi wanapopata matatizo
ili hali wanapata pesa za kutosha.
"Tuna
kuombea kwa namna moja ama nyingine ,Baba naamini kwa maombi ya
Watanzania utarudi katika kazi za ujenzi wa Taifa lako,Kuinua sanaa
yetu,Kupeperusha bendera ya mkoa wako ,Baba kuumwa kwako kuna mafunzo
mengi kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla wake, Wasanii wenzangu bima
ya afya ni kitu muhimu kwako na kwa familia yako, Bima ya Afya ni
mwokozi kwetu.
"Sidhani
kama miaka nenda rudi tutakuwa watu wa kuomba msaada ,tujiulize
tunafanya mapart, tunakunywa na kusaza ,tunajinadi kwenye mitandao nguo
zetu kuanzia milioni 3 mpaka 4 tukiulizwa umejipangaje kwa kesho amna
kitu, ni muda wa kuamka sasa ,naamini majukumu hayakimbiliki bali
tunayakabili" alisisitiza Steve Nyererere
Mzee Majuto kupelekwa India leo
Reviewed by RICH VOICE
on
Mei 01, 2018
Rating:
Hakuna maoni