Spika Ndugai Awashauri Vijana Wagombee Udiwani na Ubunge Kukabiliana na Tatizo la Ajira
Spika
wa Bunge la Tanzania mheshimiwa Job Ndugai amewataka vijana nchini
kugombea nafasi mbalimabali za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge ili
kutatua tatizo la kukosa ajira kutokana na kukosa uzoefu.
Spika
Ndugai amesema hayo Bungeni leo, Mei 18, 2018 baada majibu ya Waziri wa
nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Bunge, Jenista Mhagama, kutokana na
swali la mbunge wa viti maalumu Zainab Katimba aliyetaka kujua mkakati
wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana wasomi wasikuwa na
uzoefu.
“Asante
sana Waziri wa nchi kwa majibu ya nyongeza, Vijana wasomi, zipo kazi
nyingine hazihitaji uzoefu, mnaweza mkagombea Udiwani, mkagombea Ubunge,
nawatangazia vita waheshimiwa hapa” amesema Spika Ndugai.
Awali
Naibu Waziri, Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu Anthony
Mavunde amesema kwamba serikali imeendaa utaratibu wa kuwapa vijana
nafasi za kujitolea katika makampuni na mashirika mbalimbali ili kupata
uzoefu wa kuweza kuajiliwa
“Kupitia
mpango huu utawasaidia sana vijana wasomi wa nchi yetu ambao walikuwa
wakipata tabu na kikwazo cha uzoefu, kwa hivi sasa atapata nafasi ya
kujifunza katika kampuni kwa muda huo wa mwaka mmoja na badae tutampatia
cheti cha kumtambua ili iwe kama kiambatanisho chake” amesema Naibu
Waziri Mavunde.
Spika Ndugai Awashauri Vijana Wagombee Udiwani na Ubunge Kukabiliana na Tatizo la Ajira
Reviewed by RICH VOICE
on
Mei 18, 2018
Rating:
Hakuna maoni