Serikali yawataka waajiri kujiungana WCF
Serikali
imeagiza kwa waajiri wote nchini kujiunga Katika Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) ulioanzishwa hivi karibuni na sheria yake kupitishwa
na bunge.
Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya amesema hali
hiyo itawanufaisha wafanyakazi wanapoumia kazini kutokana na majanga
mbalimbali.
Waziri
Manyanya ameyasema hayo leo Mei 18, wakati akijibu swali la Lathifa
Chande Mbunge wa Viti Maalumu aliyekuwa akihoji iwapo Serikali ina
taarifa ya kukodishwa kwa kiwanda cha korosho cha Mtama Cashewnut
Factory kilichopo katika Jimbo la Mtama kilichokuwa chini ya bodi ya
korosho.
"Je
Serikali inachukua hatua gani juu ya mazingira magumu ya wafanyakazi
ambao hawana mikataba ya kazi katika kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa
na wageni," amehoji Chande
Manyanya
amesema kiwanda cha kubangua korosho cha Mtama kilibinafsishwa kwa
kuuza hisa asilimia 100 kwa Kampuni ya Lindi Farmers Association (LFA)
ambayo ndiyo inamiliki.
Hata
hivyo, amesema kufuatia umiliki huo, kiwanda hicho kilikodishwa kwa
makubaliano maalumu kwa Kampuni ya Sunshine ili iweze kukiendeleza.
Serikali yawataka waajiri kujiungana WCF
Reviewed by RICH VOICE
on
Mei 18, 2018
Rating:
Hakuna maoni