Mtoto wa mwaka Gitanjali Rao ameazimia 'kutatua matatizoya dunia

 


Msichana mwanasayansi na mvumbuzi aliyetangazwa kama Mtoto wa Kwanza wa Dunia wa mwaka amesema kuwa anatumai atawahamasisha wengine kubuni mawazo ya "kutatua matatizo ya dunia ".

Gitanjali Rao, mwenye umri wa miaka 15, amevumbua teknolojia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kifaa ambacho kinaweza kutambua muongozo katika kunywa maji, na app au programu ya mtandao ambayo inaweza kutambua uonevu wa kimtandao

Alichaguliwa miongoni mwa watoto zaidi ya 5,000 waliokuwa wameteuliwa kugombea nafasi ya -Mtoto wa Mwaka.

"Kama ninaweza kufanya uvumbuzi, unaweza pia kuufanya, na nina imani yeyote anaweza kuvumbua ,"alisema.

Katika mahojiano na jarida Time na muigizaji na Angelina Jolie, Bi Rao alisema kuwa hafanani na ''mwanasayansi halisi'',

"Kila kitu ninachokiona kwenye televisheni kiko hivyo , kwa kawaida utawaona wazungu wanaume ndio wanasayansi ," alisema.

"Lengo langu limegeuka kwa kweli si tu kuanzia kubuni kifaa changu binafsi kwa ajili ya kutatua matatizo ya dunia, bali kuwahamasisha wengine kufanya niliyofanya pia. Kwasababu, kutokana na uzoefu wangu binafsi , sio rahisi unapokosa kumuona mtu mwingine anayefanana na wewe ."

Bi Rao, kutoka jimbo la Marekani la Colorado, alisema kuwa kuma matatizo mengi yanayohitaji kutatuliwa.

" Kizazi chetu kinakabiliwa na matatizo ambayo hayakuwahi kushuhudia miaka ya nyuma . Lakini wakati huo huo tunakabiliwa na matatizo ambayo yalianza zamani na ambayo bado yapo ," aliliambia jarida la Time.

"Kwa mfano, tupo katikati ya janga la dunia,na wakati huo huo bado tunakabiliwa na matatizo ya haki za binadamu . Kuna matatizo ambayo hatukuyasababisha lakini ambayo tunahitaji kuyatatua sasa, kama vile mabadiliko ya tabia nchi na uonevu wa kimtandao yaliyoletwa na teknolojia ."

Tuzo ya Timeni ya hivi karibuni kutolewa kwa Bi Rao.

Awali alitangazwa kama ''mwanasayansi wa kwanza wa Marekani aliye na umri mdogo zaidi'' kwa kuvumbua kipimo cha haraka na cha rahisi cha maji machafu.

Mtoto wa mwaka Gitanjali Rao ameazimia 'kutatua matatizoya dunia Mtoto wa mwaka Gitanjali Rao ameazimia 'kutatua matatizoya dunia Reviewed by RICH VOICE on Desemba 12, 2020 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...