KAMPUNI YA SIMU TECNO YAJA NA PROMOSHENI KUBWA MSIMU HUU WA SIKUKUU.



 NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Kampuni ya Simu Tanzania TECNO imezindua promosheni inayojulikana kwa jina ‘Tunarudisha furaha nyumbani’ kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa kuwaletea wateja simu mpya aina ya TECNO SPARK 5 pro pamoja na TECNO CAMON 16s zenye ubora na gharama nafuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mahusiano Kampuni ya Simu TECNO Bw. Erick Mkomoye, amesema kuwa promosheni ya tunarudisha furaha nyumbani ni kwa ajili ya kipindi cha sikukuu ya krismasi pamoja na mwaka mpya.

Bw. Mkomoye amesema kuwa katika cha promosheni hiyo kuna simu mpya aina ya TECNO SPARK 5 pro, TECNO CAMON 16s pamoja na zawadi mbalimbali kwa wateja watakaofanikiwa kununua simu hizo ambazo zipo katika maduka yote nchini Tanzania.

“Ni simu bora na nzuri , kwa upande wa memori CAMON 16 ina GB 128 ROM kwa GB 8 RAM hii inamwezesha mtumiaji kuhifadhi vitu vyake kadiri awezavyo, huku simu ikisalia kuwa ufanisi mkubwa katika mifumo endeshi bila kukwamakwama” amesema Bw. Mkomoye.

Ameeleza kuwa skrini ya CAMON 16 ina kubwa yenye inchi 6.6 na ni HD+ huku uwezo wa camera ni 48MP pamoja na nafasi ya kutuza kumbukumbu ni GB12, na mteja atakayenunua anaingia katika droo ya kushinda zawadi mbalimbali.

Afisa Masoko Kampuni ya Simu TECNO Bw. Motta William amesema kuwa mteja atakayenunua simu hizo katika kipindi hiki cha sikukuu atashinda zawadi ikiwemo mashine ya kufulia nguo, Smart Tv, Blender pamoja na zawadi nyengine nyingi.

“Kauli mbiu ya promosheni hii tunarudisha furaha nyumani, kila mtu achangamkie fursa kwa kununua simu bora kwa gharama nafuu katika kipindi cha sikukuu kwa ajili ya kufurai na familia yake.” amesema Bw. William.

KAMPUNI YA SIMU TECNO YAJA NA PROMOSHENI KUBWA MSIMU HUU WA SIKUKUU. KAMPUNI YA SIMU TECNO YAJA NA PROMOSHENI KUBWA MSIMU HUU WA SIKUKUU. Reviewed by RICH VOICE on Desemba 12, 2020 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...