SIMBA QUEEN VS YANGA PRINCESS, DERBY YANGU YENYE BURUDANI YA KUTOSHA


Simba Queen vs Yanga Princess Uzuri wa mwanamke hupimwa kwa tabia yake tu na sio sura na umbo aliojaaliwa inapaswa tufahamu hili ndugu zangu kwani dunia ya sasa tuliowengi hatutazami hayo pengine kulingana na utandawazi uliopo na kusahau mila na desturi za babu zetu kuwa kilicho chema ni kile kilichohifadhiwa.

Simba Queen na Yanga Princess kwenye derby kubwa Afika mashariki na kati Yanga akiwa kileleni mwa msimamo mwa ligi akiwa na alama tisa huku akicheza michezo mitatu kama ilivyo kwa Simba akicheza michezo mitatu na alama saba kibindoni kwenye msimamo nafasi ya tatu wanaingia mzunguko wa nne wa ligi kuu ya wanawake.

Vita ya soka la Tanzania kwa kina dada kama ilivyo kwa wanawaume ni Simba na Yanga historia ya soka la wanawake nchini kwenye derby Simba ndio kinara wa kumfunga mpinzani wake mara nyingi hivyo Simba ndio mwenye rekodi nzuri kwenye derby hizi za wanawake.

Itoshe kusema ya kwamba rekodi inambeba Simba ila kwasasa kwa michezo mitatu waliocheza unaipa nafasi Yanga kwa kushinda michezo yote mitatu na kwa upande mwingine unaweza sema aliyefungwa mchezo mmoja ndio huenda akawa mzuri zaidi kwa kuonja radha ya kufungwa nafasi kubwa naipa Simba kwenye derby hii ya wanawake nchini.

Naiona vita ya Kocha Mgosi na Edina lema kwenye mchezo huu naweza sema ubora wa mbinu ndio ushindi wa leo kwa timu zote mbili hivyo atakae mzidi mbinu mwenzie ndio atakayepata matokeo mazuri kwenye mchezo huu.

Tanzania kwa ujumla ndio mda wa kuwaonesha kina dada kuwa tunawaunga mkono wanawake kwenye soka kwa kwenda kuutazama mchezo huu kwenye uwanja wa Mo Arena Bunju.

Imeandaliwa Na:Fadhila Kizigo 0673854979 instragram fadhilakizigo19

SIMBA QUEEN VS YANGA PRINCESS, DERBY YANGU YENYE BURUDANI YA KUTOSHA    SIMBA QUEEN VS YANGA PRINCESS, DERBY YANGU YENYE BURUDANI YA KUTOSHA Reviewed by RICH VOICE on Desemba 12, 2020 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...