Saturday, November 19, 2016

Waziri Mkuu akagua ujenzi wa nyumba za Magomeni Kota....Ataka Ukamilishwe Kwa Wakati


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Magomeni watumie utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa wakati.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati alipokagua ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mkuu amewataka wataalamu hao waendelee kufanya kazi hiyo kwa kufuata misingi ya weledi wa taalauma yao kwani Serikali inawaamini.
“Muhimu mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili wananchi waliokuwa wanaishi hapa waweze kurudi katika makazi yao,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Mhandisi Edwin Nnunduma alisema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha majengo matano ya makazi.
“Kati ya majengo haya matano, manne yatakuwa na ghorofa nane na moja litakuwa na ghorofa tisa, ambapo wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wanaishi eneo hili tangu zamani watakabidhiwa,” alisema.
 
Mhandisi Nnunduma alisema majengo hayo yanajengwa kwa teknolojia ambayo imezingatia uwezo wa wakazi wake ambapo ina majiko yanayoweza kutumia kuni na mkaa.
 
Alisema mradi huo ambao unajengwa kwa awamu tofauti utahusisha ujenzi wa nyumba za makazi, maduka makubwa na ya kisasa pamoja na ofisi.
 
Mhandisi huyo alisema awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba Mosi, mwaka huu inahusisha ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo ambayo inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 


Saturday, November 19, 2016

Polisi yaongeza muda wa zoezi la uhakiki wa silaha za kiraia kwa nchi nzima


Jeshi la Polisi limeongeza muda wa huruma kwa wamiliki wa silaha walioshindwa kuhakiki silaha zao katika zoezi la uhakiki wa silaha za kiraia Tanzania Bara lililoanza Machi 22 na kumalizika Juni 30, 2016.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Robert Boaz, amesema licha ya Jeshi la Polisi kuongeza muda wa uhakiki hadi mwezi Oktoba mwaka huu, bado wamiliki wengi hawakujitokeza kuhakiki silaha zao.

“Katika kipindi cha kuanzia tarehe 22 Machi, 2016 hadi Juni 30 serikali ilianza kufanya zoezi la uhakiki wa silaha zote za kiraia hapa Tanzania Bara, kutokana na sababu mbalimbali tuliongeza muda lakini bado baadhi ya watu hawakujitokeza,” amesema.

Amesema baada ya zoezi la awali kukamilika, tathmini inaonyesha kuwa asilimia 59.18 ya silaha zote zilizosajiliwa ndizo zilizohakikiwa na kwamba asilimia 40.82 hazijahakikiwa.

CP Boaz amesema polisi imeongeza muda wa mwezi mmoja ili wasio hakiki silaha zao wahakiki, na kwamba muda huo ni wa mwisho hautaongezwa tena.

“Tunatoa tena muda wa huruma tunawataka wamiliki wajitoekeze vituoni kuhakiki silaha zao ndani ya mwezi mmoja kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 20, 2016. Huu ni muda wa mwisho na utakapomalizika tutachukua hatua kali.”

Amezitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuta leseni za umiliki kwa silaha zote zisizohakikiwa, kuwatangaza wamiliki wote wa silaha kwenye vyombo vya habari walioshindwa kuhakiki pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Ametoa wito kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha silaha zao katika vituo vya polisi au ofisi za serikali za mitaa na kwamba atakae tumia kipindi hiki hawatachukuliwa hatua za kisheria.
 
 

Saturday, November 19, 2016

Maalim Seif kufuta nyayo za Lipumba Mikoa ya Kusini


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kuzuru mikoa ya Kusini mwa Tanzania katika kipindi ambacho bado kuna sintofahamu kuhusu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.

Mwanasiasa huyo ambaye ataongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu watazuru Mtwara na Lindi ikiwa ni miezi michache baada ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuzuru eneo hilo la kusini.

Akizungumzia ziara hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma wa chama hicho, Mbarala Maharagande alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli za chama na kupokea maoni ya pamoja ya namna ya kuboresha utendaji wa chama hicho kwa ngazi za chini.

Maalim Seif anatua katika eneo hilo wakati ambapo kukiwa na mvutano baada ya baraza la madiwani kufanya jaribio lililoshindikana la kumng’oa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Geofrey Mwanchisye.

Jaribio hilo liligonga mwamba baada ya Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Sifaeli Kulanga kueleza kuwa hoja zao hazina msingi kwani tuhuma zao kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma yanakinzana na ripoti ya kamati maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Kesi kuhusu Uenyekiti wa chama hicho inaendelea Mahakamani ambapo Baraza Kuu la chama hicho linapinga barua ya Msajili inayomtambua Lipumba kama Mwenyekiti wa chama hicho wakati ambapo Baraza hilo lilikuwa limetangaza kumfuta uanachama.
 
 

Saturday, November 19, 2016

Majibu ya Jeshi la Polisi Makao Makuu kuhusu tuhuma za Rushwa dhidi ya Kamanda Sirro


Jeshi la polisi nchini limesema litafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro na baadhi ya makamanda wa mikoa akiwemo kamanda wa mkoa wa Kinondoni Susan Kaganda.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya CP Boaz kwa niaba ya jeshi la polisi imetolewa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni kuwatuhumu makamanda hao kuwa wanasita kuwachukulia hatua watumiaji na wauzaji wa kilevi cha shisha kwa madai kuwa huenda wakawa wamepokea rushwa kutoka kwa wanaojishughulisha na biashara hiyo.

Makonda alitoa tuhuma hizo licha ya yeye ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika kanda hiyo kutoa maagizo wahusika kuchukuliwa hatua.

CP Boaz alisema, kuhusu tuhuma ya rushwa suala hilo lina taasisi zake zinazohusika, na kwamba jeshi hilo limepokea tuhuma hizo dhidi ya askari wao kwa hiyo watazichunguza kubaini ukweli.
 
 

Saturday, November 19, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Novemba 19


Reviewed by RICH VOICE on Novemba 19, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...