Wednesday, November 16, 2016
Rais wa Congo Joseph Kabila atangaza kutokuwania Urais tena
Rais
wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amelihutubia Bunge la
Taifa jana na kuwahkikishia wananchi kuwa hatogombea tena Urais katika
uchaguzi mkuu ujao.
Rai Kabila amesema anaiheshimu katiba ya nchi yake na kwamba ataifuata huku akisisitiza kuwepo kwa amani na utulivu.
“Jahmuri
ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba, hatujakiuka
katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni
kuangalia maisha ya wakongo,” alisema Kabila.
Hata
hivyo, juzi waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi
wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza vurugu za kisiasa nchini humo baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.
Awali
Kamisheni ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
iliahirisha uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu hadi
mwezi Julai mwakani.
Pia,
Mahakama ya juu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kuwa
iwapo serikali ya Rais Joseph Kabila haitaweza kuandaa uchaguzi wa rais
katika wakati ulioainishwa basi kiongozi huyo anaweza kubakia
madarakani.
Kabila
alishika hatamu za kuiongoza Congo mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba
yake, Laurent Kabila, na kisha akashinda uchaguzi wa rais uliofanyika
mwaka 2006.
Wednesday, November 16, 2016
Vyeti FEKI vya vifo Vyatumika Kupata mikopo Elimu ya Juu
Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imebaini kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi
ambao wamewasilisha vyeti feki vya vifo vya wazazi wao ili waonekane
kama ni watoto yatima; hivyo wapewe kipaumbele cha kupatiwa mkopo.
Kuwepo
kwa vyeti hivyo vya bandia kumegunduliwa na bodi hiyo baada ya kupeleka
nakala za vyeti vyote vya vifo ofisi ya Msajili wa Vizazi na Vifo
(Rita) kwa ajili ya uthibitisho ndipo ikagundulika kuwepo kwa kasoro
hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul- Razaq Badru, amesema
kuwa wahusika wote ambao wamewasilisha vyeti hivyo feki suala lao
limekabidhiwa kwa mamlaka zinazoshughulika na makosa ya jinai.
Hata hivyo, Badru hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo kwa maelezo kuwa bado wanaendelea na ukaguzi.
“Bado tunaendelea kuchunguza na idadi yao hapa sina, tukikamilisha tutawaita kuwaambia idadi yao,”
alisema Badru na kuongeza kuwa kutokana na kasoro hizo, ndio maana kuna
baadhi ya watu wanaolalamika kuwa ni yatima, lakini hawakupata mkopo.
“Hayo malalamiko ya kwamba kuna yatima wamekosa mikopo tumeyasikia, lakini na sisi tunajiridhisha kuwa huyu ni yatima baada ya kupata uthibitisho wa vyeti vya vifo kutoka Rita,” alisema Badru.
“Hayo malalamiko ya kwamba kuna yatima wamekosa mikopo tumeyasikia, lakini na sisi tunajiridhisha kuwa huyu ni yatima baada ya kupata uthibitisho wa vyeti vya vifo kutoka Rita,” alisema Badru.
Aliongeza
kuwa hata wale ambao ni wanafunzi wenye ulemavu, bodi hiyo haiwezi
kuwaamini kama ni walemavu, bali hadi wapate uthibitisho kutoka kwa
daktari wa wilaya (DMO) kuthibitisha ulemavu wa mwombaji.
Alisema
baadhi ya wanafunzi ambao wanalalamika kuwa wamekosa mikopo ni wale
ambao maombi yao yalikaguliwa na kukutwa na dosari kadhaa, na wakaombwa
wazirekebishe kasoro hizo, lakini baadhi yao hawakufanya hivyo.
Badru
alisema bodi yake baada ya kuchambua maombi ya waombaji wote; hadi sasa
imeshatoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili wakiwemo yatima,
walemavu, wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele na wahitaji wanaosoma
kozi zingine.
Akizungumzia
suala la baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambao
wamekosa mikopo na kulazimika kurudi makwao, Badru alisema wanafunzi hao
yawezekana ni miongoni mwa wale ambao hawakukidhi vigezo vya kuweza
kupewa mkopo.
“Pale
Dodoma tumetoa mkopo kwa wanafunzi wapya takribani 3,000, hivyo hao
wanaoondoka kurudi nyumbani yawezekana wako kwenye kundi la wanafunzi
ambao hawakukidhi vigezo vya kupewa mkopo,” alisema Badru.
Alisema
sio rahisi kutoa mkopo kwa wanafunzi wote, kwani Serikal inaendeshwa
kwa bajeti na mwaka huu wamechagua kusomesha wanafunzi 25,000 kulingana
na bajeti iliyopo pamoja na kulingana na mahitaji ya wataalamu
wanaotakiwa na kutokana na vipaumbele vyake.
Alisema anatambua kuna wanafunzi zaidi ya 10,000 ambao wamekosa mikopo na kuongeza; “lakini
bajeti ya mwaka huu imeishia hapo, mwaka kesho tunaweza kuishauri
Serikali iongeze fedha baada ya kuwa tumefanya tathmini uhitaji wa
mikopo hiyo.”
Hata
hivyo, Badru alisema kuna wanafunzi ambao wanasoma kozi za kipaumbele,
lakini wazazi wao wana uwezo, hao nao hawakupatiwa mikopo licha ya kuwa
kwenye kundi la wanaostahili mkopo.
“Kuna
mtu anasomea udaktari, lakini wazazi wake wana uwezo, na kuna
mwanafunzi anasomea sayansi ya jamii na wazazi wake ni watu wasio na
uwezo, hapo lazima tuangalie mhitaji ni yupi kati ya hao wawili na ndiye
tunampatia mkopo,” alisema Badru.
Alisema
kuna wanafunzi wanasoma kozi za kipaumbele baadhi yao hawakupata mkopo
kabisa na baadhi yao wamepatiwa mkopo kidogo baada ya bodi hiyo kufanya
tathmini ya hali ya uchumi ya wazazi au walezi wa mwombaji.
Wednesday, November 16, 2016
Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa atoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa ATCL kufanya mabadiliko ya menejimenti ya Shirika hilo
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa muda
wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),
kufanya mabadiliko katika menejimenti ya Shirika hilo ili kuongeza
ufanisi na kuboresha utendaji kazi.
Ametoa
agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika mkutano wa
Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo na kuwataka kutoa
huduma bora ili kulifanya Shirika hilo kuwa miongoni mwa mashirika bora
ya ndege barani Afrika.
“Nataka
ndani ya mwezi mmoja uwe umeshafanya mabadiliko katika menejimenti,
mabadiliko lazima yaanzie juu kwanza kwa watoa maamuzi na ishuke hadi
kwa wafanyakazi wazembe na wasio waadilifu,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amepinga nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa Shirika hilo
hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali ipo katika juhudi za kulifufua
na kuliimarisha Shirika hilo.
Aidha
Waziri Mbarawa ameitaka Idara ya Masoko ya shirika hilo kuzunguka
katika taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake na kuzishawishi kuweza
kutumia huduma za usafiri wa anga wa ATCL.
“Serikali imekamilisha upande wake wa ununuzi wa ndege, sasa kazi inabaki kwenu, sitaki watu wa masoko kukaa ofisini”, amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa wafanyakazi wa ATC wanatakiwa kujipanga kutoa huduma iliyotukuka
kwa wateja wake ili kuweza kuhimili ushindani uliopo katika mashirika ya
ndege nchini.
“Inabidi
tofauti kubwa ionekane kati yenu na mashirika mengine, yeyote ambaye
anaona hawezi kutoa huduma bora kwa mteja atafute sehemu nyingine kwani
hapa hatufai ”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amelitaka shirika hilo kutumia mfumo wa kisasa wa kukata tiketi
kwa njia ya simu na kompyuta ili kuwarahishia watumiaji wa shirika hilo
kuweza kupata tiketi kwa haraka na urahisi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Eng. Ladislaus Matindi
amemhakikishia Waziri Mbarawa kufanyia kazi maagizo aliyotoa na kuahidi
kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo kwa lengo la kuteka soko la
ushindani wa usafiri wa anga nchini.
“Kwa
sasa tumeanza vizuri na naamini uwezo wa kuzalisha faida zaidi tunao,
tunaahidi kuboresha utendaji kazi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya
Serikali ya Awamu ya Tano,” amesema Eng. Matindi.\
Wednesday, November 16, 2016
Dr. Shein Atia Saini Sheria ya Gesi na Mafuta.....Asema Wanaoikosoa ni Wachoyo na Hawana Nia Njema na Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amesaini sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ya Zanzibar.
Mbali ya kusaini sheria hiyo, amewapiga kijembe wanaoikosoa sheria hiyo kuwa ni wachoyo na wasioitakia mema Zanzibar.
Dk.
Shein aliwaambia viongozi na waandishi wa habari kuwa sheria hiyo namba
6 ya mwaka 2016, inaipa Zanzibar mamlaka ya kisheria ya kuendeleza
rasilimali ya mafuta na gesi asilia.
Alisema kitendo cha kutia saini sheria hiyo, hakijavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama baadhi ya watu wanavyodai.
“Hakuna
aliyevunja sheria, anayevunja sheria wala atakayevunja sheria. Lakini
kama wao wanadai kutia saini sheria hii ni kuvunja sheria, basi watafute
suluhisho la kisheria,” alisema.
Aliwashauri
wenye mawazo hayo wakasome vizuri Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015
iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo
imeweka msingi imara wa kisheria wa kutambua rasilimali ya mafuta na
gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyoorodheshwa kwenye Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yanahitaji usimamizi bora na
imara wa kisheria.
Alisema
sheria hiyo imeainisha mambo makuu matatu ambayo kwanza ni kuwa
shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Bara
zitasimamiwa na taasisi zilizoanzishwa ndani ya sheria namba 21 ya 2015.
Sheria
hiyo inatamka pia kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa
upande wa Tanzania Zanzibar zitafanywa na taasisi zitakazoanzishwa kwa
mujibu wa sheria za Tanzania Zanzibar.
Kuhusu
mapato yatokanayo na shughuli hizo, Dk. Shein alisema sheria inatamka
upande wa Tanzania Bara mapato yatatumiwa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa faida ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa
Tanzania Zanzibar yatatumiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
faida ya Zanzibar.
“Kila
upande ulishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tulishauriana kwa
kina viongozi na tukapata ushauri wa kutosha kutoka kwa wanasheria wetu
wakuu hadi kufika bungeni,” alisema Dk. Shein.
Alisema
anatambua sheria hiyo ni mpya na anaelewa changamoto ambazo zinaweza
kutokea, lakini akatoa wito kwa wananchi kuiunga mkono na kushirikiana
na Serikali.
“Mafuta ni jambo kubwa katika maendeleo, pia yasipotumika vyema yanaweza kuitikisa nchi,” alisema Dk. Shein.
Aliwatahadharisha wananchi kutegemea mafanikio ya haraka kutoka sekta hiyo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla
iliyofanyika jana ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali
mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na
Ikulu.]
Viongozi
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya
utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa jana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa
katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji
wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja jana
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na
Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika
hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa
Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja jana.
Wednesday, November 16, 2016
Meya wa West Virginia ajiuzulu baada ya kufurahia andiko lililomfananisha mke wa Obama na Nyani
Meya
wa mji wa Clay nchini Marekani, Beverly Whaling amejiuzulu wadhifa huo
baada ya kuunga mkono maandishi yenye ubaguzi wa rangi kwenye facebook
dhidi ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama.
Meya
huyo aliingia matatani na kuamua kujiuzulu nafasi yake baada ya
kuonesha kufurahishwa na ‘post’ ya kibaguzi iliyoandikwa na Mkurugenzi
wa shirika moja la kutoa misaada, Pamela Taylor aliyelenga kubainisha
tofauti kati ya mke wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Melania na
mama Michelle Obama.
Taylor alimtusi Michelle akimfananisha na sokwe huku akimpamba Melania kuwa ni mrembo.
Meya huyo aliandika chini ya ujumbe huo wa kibaguzi, “Just made my day Pam.”
Zaidi
ya watu 200,000 wamejiandikisha mtandaoni ndani ya muda mfupi kupinga
ubaguzi huo na kuwataka Whaling na Taylor kujiwajibisha haraka.
Vitendo vya kibaguzi vimeripotiwa kuongezeka nchini humo tangu Trump alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.
Ingawa
kauli zake wakati wa kampeni zilikuwa na matamko tata, Trump amewataka
wafuasi wake kuacha mara moja vitendo vyovyote vya kibaguzi akisisitiza
kuwa yeye atakuwa rais wa Wamarekani wote.
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 16, 2016
Rating:
Hakuna maoni