ALHAMISI HII YA LEO 05/01/2016
WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI
Waziri
mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za serekali katika misa ya
kumuombea maerehemu Kapteni K enan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la
Jimbo kuu Katoliki la Songea Parokia ya Mtoto Yesu Matogoro Songea
DELE ALLI ATIKISA NYAVU MARA MBILI NA KUITIBULIA CHELSEA KUWEKA REKODI
Timu ya Tottenham imekwamisha
jitihada za Chelsea kuweka historia ya kushinda michezo 14 mfululizo
ya Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kuifunga magoli 2-0 katika dimba
la White Hart Lane.
Kwa ushindi huo Tottenham imekwea
hadi katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi, shujaa akiwa Dele Alli
aliyefunga kwa mpira wa kichwa katika kila kipindi, na kuifanya
Chelsea iongoze ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Liverpool ya
pili.
Alli alifunga goli la kwanza baada
ya kuruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliopigwa na Christian
Eriksen katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, na wawili hao tena
walishirikina na Alli kufunga goli lingine katika kipindi cha pili.
Dele Alli akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli
Pedro na Diego Costa walijikuta wakibwatukiana baada ya maji kuzidi unga
UZINDUZI WA VIFAA VIPYA VYA KUTEREMSHIA MAKONTENA UNGUJA.
MASAUNI AFANYA ZIARA MAGEREZA, AAGIZA SARE ZOTE ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA IDARA YA UHAMIAJI KUANZIA SASA ZISHONWE KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ESA SALAAM
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi
la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo
alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya
kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya
Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara
hizo zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(katikati) akitoka katika Jengo la Useremala mara baada ya kukagua
mashine mbalimbali zinazotumika kuranda na kuchana mbao kwa ajili ya
utengenezaji wa samani katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,
Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.
WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF
Meneja wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutambua na kusajili wanachama wapya, kukusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.
Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.
Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari. Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya. Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu. Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama
Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada
Jumatano, 4 Januari 2017
MAANDALIZI YA AIRTEL RISING STARS YAKAMILIKA
Kliniki
ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa
inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye Uwanja wa Karume huku
wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki.
Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita.
Kliniki hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya taifa Oscar Milambo akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku wasichana wakifundishwa na Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Queens, Sebastian Nkoma.
Akizungumzia maandalizi ya kliniki hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo ya soka la vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi alisema, “Kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za mpira, na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili kuongezewa vipaji vyao.
“Sisi TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens.” alisema Nyenzi na kuongeza:
“Tunaamini ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars. Nachukua nafasi hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars.”
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa miaka 15, Oscar Milambo alisema: “Wachezaji watafundishwa nidhamu ya mpira, ndani na nje ya uwanja, jinsi kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia.”
Sambamba na hayo wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata mafunzo kutoka kwa makocha. Milambo aliongeza kuwa vijana hao watafundishwa jinsi mchezaji anavyotakiwa kujitunza kwa manufaa ya kuendelea kutunza kipaji chake.
Akizungumza juu ya kliniki hiyo, Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa kufanyika kwa kliniki kutahitimisha Airtel Rising Stars msimu wa sita na kufungua pazia kwa maandalizi ya Airtel Rising Stars msimu wa saba.
Michuano ya Airtel Rising Stars mwaka 2016 tuliunganisha na promosheni ya kampuni ya Airtel ya ‘Airtel Fursa’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha vijana kufanikisha malengo yao.
Matinde aliongeza kuwa Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza vipaji vya soka kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania. Airtel Rising Stars inalenga kutafuta vipaji chipukuzi kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa.
“Kampeni yetu ya Airtel Fursa inalenga kuwainua vijana na kuwawezesha kufikia ndoto zao inaenda sambamba na program hii ya Airtel Rising Stars na tunajisikia furaha kuendelea kuwafikia vijana katika nyanja mbalimbali,” aliongeza Matinde.
Wachezaji zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke,Lindi na Zanzibar.

Kafulila kupokea kadi ya Chadema jimboni Kwake Mwezi Huu
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema atapokelea kadi ya Chadema jimboni mwake baadaye mwezi huu.
Kafulila
alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema kwa alichoeleza kuwa
ndicho chama kilichojipambanua kuelekea safari ya mabadiliko ifikapo
mwaka 2020.
Kada
huyo tayari amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena
Nyambabe kumjulisha kuwa anajivua uanachama na anarudi Chadema.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana, Kafulila alisema ameamua kuwa
atapokelea kadi hiyo jimboni kutokana na mapenzi aliyonayo kwa wananchi
wake.
"Nimepanga
kuchukua kadi mwezi huu jimboni, kwa kuwa ilikuwa nichukue kadi
mwanzoni lakini ilishindikana kutokana na siku kuu, hivyo siku yoyote
kuanzia sasa nitachukua," alisema.
Wakati
anajiuzulu NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema, alisema hakufanya uamuzi kwa
kukurupuka bali alitafakari na kushauriwa na wananchi wa jimbo lake, na
kuridhika kurudi huko.
"Nilitafakari
na kushauriwa sana jimboni na kuridhika kwamba Chadema ndiko sehemu
inayojipambanua kwa mikakati ya kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na
Watanzania na ni vema kukusanya nguvu ya kila mwenye kiu ya mabadiliko
ndani ya chama kimoja, ili kufupisha safari ya mabadiliko," alisema.
Alipoulizwa
kwa nini amerudi Chadema wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho,
Dk Wilbrod Slaa alipata kumwita sisimizi kwa alichoeleza kuwa hakuwa na
imani naye, alijibu kuwa siasa ni malengo si uhusiano binafsi.
Kafulila
aliongeza kuwa wanasiasa wanaunganishwa na malengo zaidi ya urafiki na
kwamba malengo yake sasa ni kuendelea kupigania mabadiliko ya kimfumo
yanayoenea zaidi kwenye chama hicho (Chadema) kuliko kingine.
Novemba
10, 2009 Kafulila alijivua uanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi
kutokana na kuondolewa kwenye nafasi ya uofisa habari wa chama hicho.
Pia
akiwa NCCR-Mageuzi, alitimuliwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka taratibu
za chama hicho na tuhuma za kutaka 'kumpindua' Mwenyekiti, James Mbatia.
Hata
hivyo, suala hilo lilipata suluhu baada ya Mbatia kuteuliwa na Rais
mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Wakiwa bungeni, Mbatia na Kafulila
walikutana, kuzungumza na hatimaye kumaliza mzozo wao.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humprey Polepole atangaza neema kwa Wanafunzi waliokosa mikopo
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humprey Polepole
amewatangazia neema wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo,
akiwataka wamtafute ili awaoneshe cha kufanya
Polepole ambaye alikuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV
aliuzwa na baadhi ya watu kuhusu tatizo lililopo la mikopo ya elimu ya
juu, ambapo aliwajibu kuwa serikali imekwishatoa maelekezo kwamba
haiwezi kumkopesha kila mtu na kwamba inatoa mikopo kwa vigezo
vilivyowekwa.
Kuhusu
watu wasioweza kujigharamia elimu hiyo na wamekosa mikopo, amewashauri
kuahirisha masomo yao, ili wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata pesa
na ndani ya mwaka mmoja ana uhakika watakuwa wamepata pesa
zinazohitajika na kuendelea na masomo yao.
Polepole
alitaja baadhi ya shughuli ambazo angewashauri wazifanye kuwa ni pamoja
na kilimo huku akitolea mfano baadhi ya watu aliowashauri wajiingize
kwenye kilimo cha matikiti na wakaufanyia kazi ushauri huo, ambapo baada
ya muda wameona matunda yake.
"Waliokosa mikopo vyuo vikuu wanitafute, nitawaonesha cha kufanya, na wawe tayari kuahirisha masomo mwaka mmoja"
Akizungumzia
uamuzi wa serikali kusimamisha ajira, Polepole amesema serikali haiwezi
kuendelea kuajiri wakati inafanya kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa
ambao wanalitia hasara taifa na kuwataka watanzania waendelee kuwa
watulivu na kumuunga mkono Rais Magufuli, ili amalize mchwa wote
serikali na kisha ajira zitatoka.
"Nawaambia vijana wakati unasubiri ajira usibweteke kwani mtu anayebweteka akipata kazi ataharibu kazi yetu"
Kuhusu
serikali kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati pekee,
Polepole amesema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa taifa lina uhaba mkubwa
wa walimu wa Sayansi na Hisabati kuliko walimu wa masomo ya sanaa.
"Tunao utimilifu wa walimu wa sanaa, tunao upungufu wa walimu wa Sayansi"
Amuua Mkewe Kwa Visu na Kumnyonga Mtoto Baada ya Kuambiwa Ana Mchepuko Nje ya Ndoa
Mkazi wa Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, amemuua mkewe pamoja na mtoto wake.
Mkazi
huyo Rashid Nassoro, baada ya kuwaua watu wake wa karibu alikimbia na
baadae kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata
sehemu zake za siri.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amethibitisha tukio hilo na
kusema lilitokea juzi eneo la Bukene, wilayani hapa baada ya Rashid
Nassoro (22) kumuua mkewe kwa kumchoma visu tumboni.
Jeshi la Polisi Laua Majambazi Watatu Dar es Salaam
Watu
watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la
kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya
Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon
Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado
hayajafahamika.
Alisema
marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni
26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara,
Dar es Salaam.
Hata
hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao
walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na
taarifa rasmi atazitoa leo.
Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa
zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha,
ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi
katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.
Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa zaidi leo.
Alisema, baada ya kumuua mke wake, Rashid alimnyonga mtoto wake wa miezi minne na kukimbia.
Kamanda
Selemani, alisema baada ya kukimbia Rashid aliamua kutaka kujiua kwa
kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za siri.
Alisema
chanzo cha tukio hilo ni mwanamke kumtuhumu mume wake kuwa ana uhusiano
na mwanamke mwingine jambo lililomchukiza mwanaume huyo.
Habari Zilizopo Katika Magaeti Ya Leo Alhamisi ya January 5
Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani.....Ni Baada ya Serikali Kuwasilisha Notisi Ya Kupinga Dhamana yake Mahakama ya Rufaa
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi
ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya
mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama
ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi alitarajiwa kutoa
uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga Lema kupatiwa dhamana Novemba
11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha
katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya
Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya
mdomo.
Baada
ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi
mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani
na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya mawakili wa
pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya Jamhuri
kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria
kutoa uamuzi wa rufani hiyo.
ALHAMISI HII YA LEO 05/01/2016
Reviewed by RICH VOICE
on
Januari 05, 2017
Rating:
Hakuna maoni