SUNDAY NEWS 01/01/2017
SHEREHE ZA MWAKA MPYA ZAFANA JIJINI LONDON
Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya
jijini London zimefana na kupambwa na fataki za rangi tofauti, wakati
watu katika sehemu mbalimbali duniani wakifurahia mwaka mpya.
Watu milioni moja walikusanyika
Jijini London kushuhudia fataki zenye rangi tofauti zikiupamba mji
huo mkuu wa Uingereza.
Jumla ya fataki 12,000 zilipamba
anga la London, ambapo mwaka mpya ulichelewa kuingia kwa sekunde moja
kutokana na kupungua kwa kasi ya mzunguko wa dunia.
Watu waliokuwa wamekusanyika Jijini London kungojea kuukaribisha mwaka mpya
Jumapili, 1 Januari 2017
RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MWAKA MPYA KATIKA KANISA KUU JIMBO KATOLIKI LA BUKOBA MKOANI KAGERA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma
mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani
Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu
mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius
Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki
Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea
katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara
baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba
Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la
Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba
mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba
mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya
Ibada.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara
baada ya Ibada.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali
katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani
hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya
kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi
wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni Kanisani hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma kushoto pamoja
na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na masista kanisani hapo mara baada ya Ibada. PICHA NA
IKULU Jumapili, 1 Januari 2017
BALOZI SEIF AUKARIBISHA MWAKA MPYA 2017 KWA KUITAKA JAMII KUENDELEA KUSHIRIKIANA
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na
baadhi ya Viongozi na watendaji wa Ofisi yake kwenye chakula
alichokiandaa nyumbani kwake hapo Mtaa wa Kama kwa ajili ya kuuaga
mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka Mpya wa 2017.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akijichagulia mlo kwenye tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mahsriki,
Kikanda na Kimataifa Balozi Ramadhan Muombwa naye hakuwa nyuma kushiriki
kwenye tafrija hiyo.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Idara zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar wakitunisha misuli katika tafrija hiyo ya kuukaribisha
mwaka mpya wa 2017.
Wa
kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za
SMZ na SMT Nd. Khalid Bakari Amrani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya
Kukabiliana na Maafa Nd. Ali Juma Hamad na Mkurugenzi wa Idara ya
Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa Bibi Riziki Daniel Yussuf.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifurahia chakula kitamu kilichotayarishwa kwenye Tafrija hiyo ya usiku.
Familia
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ikionekana kupozi kwenye tafrija
hiyo wakifuatilia muziki laini uliokuwa ukitumbuiza katika Tafrija hiyo.
Balozi
Seif Ali Iddi, Mkewe pamoja na Familia yao wakisakata rumba kwenye
tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 nyumbani kwao Mtaa wa Kama.
Olaaaaaaaa.
Ndii. Ni wakati wa kuingia saa 6 na dakika moja ya usiku wa kuingia
mwaka mpya wa 2017 washiriki wa tafrija hiyo wakijimwaga uwanjani
kuukaribisha mwaka huo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma
Nhunga akitoa shukrani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kwa washiriki wa Tafrija ya kuukaribisha mwaka
mpya wa 2017.
Jamii imeaswa kuendelea kushirikiana katika harakati zao za kila siku za kimaisha na Kifamilia ili kukifanya kizazi chao kukua katika maadili na utamaduni unaokubalika kidini na kidunia jambo ambalo litatoa faraja kwa wazazi, walezi pamoja na Viongozi wa Kitaifa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga wakati wa hafla maalum ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka Mpya wa 2017.
Mh. Mihayo alisema hayo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyeandaa hafla hiyo Nyumbani kwake Mtaa wa Kama nje kidogo ya Kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar akiwashukuru baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi hiyo pamoja na Familia zao walioshiriki katika kuukaribisha mwaka mpya.
Katika kuuaga mwaka 2016 uliobeba matukio mbali mbali yakiwemo mengi ya udhalilishaji wa Kijinsia ya yale yaliyopoteza maisha ya Wananchi wengi kutokana na ajali za bara barani, Naibu Waziri Mihayo alisema suala la kupendana miongoni mwa Jamii ndani ya mwaka mpya wa 2017 linafaa kufanywa kuwa jambo la msingi.
Kupitia hafla hiyo ya chakula cha usiku Mhe. Mihayo Juma Nhunga kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatakia kheir ya mwaka Mpya Wananchi wote wa Zanzibar na kuwataka wale waliokoseana ndani ya mwaka uliopita wasameheane.
Alisema Mwaka mpya unahitaji zaidi mambo mapya na ya msingi ili kulifanya Taifa na wananchi wake waelekee kwenye maendeleo yatakayoleta faida na kustawisha maisha yao ya kila siku.
Hafla hiyo ya chakula cha usiku uliyowakutanisha baadhi ya Viongozi na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Familia zao iliambatana na muziki laini uliotoa burdani safi kwa washiriki hao walioshindwa kukaa kwenye viti vyao na kuonekana wakianza kuserebuka.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/1/2017.
Jumapili, 1 Januari 2017
ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa
(katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya
Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya
Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa
msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na
thamani ya sh.milioni 12.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
Takataka zikipelekwa eneo maalumu.
Takataka zikipelekwa kutupwa.
Waumini wa kanisa hilo wakipiga picha mbalimbali za tukio hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa
(kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,
wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo kutoa msaada wa magodoro
na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es
Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa
kanisa hilo.
Kiongozi wa kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa (kulia), akipanda mti.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu (kulia), akipanda mti.
Ofisa Afya wa Hospitali hiyo, Amina Pole (kushoto),
akipanda mti.
akipanda mti.
Waumini wa kanisa hilo na viongozi wao wakiwa kwenye
tukio hilo.
tukio hilo.
Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada huo. |
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa amesema migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha
hali ya amani nchini.
Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kutoa misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
“Migogoro ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa inaweza kuhatarisha amani ya nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na kuweka mambo sawa” alisema Mokiwa.
Alisema migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha kutoweka kwa amani hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo kwa karibu na kulitafutia ufumbuzi.
Alisema nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana na matukio ya kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya viroba vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.
Alisema matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi kukimbia nchi yao kwa hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya mungu.
Akizungumzia msaada uliotolewa na kanisa hilo katika hospitali hiyo ambao ni vitanda 15,magodoro 20, mashuka 40 na viatu vya tahadhri jozi 30 vyenye thamani ya Sh12 milioni alisema kanisa hilo kwa muda mrefu limekuwa likifanya maombi ya kuwaombea viongozi wa nchi na kutoa misaada ya kijamii hususan katika sekta ya afya, elimu na maeneo mengine.
Mokiwa alisema wananchi wanapokuwa katika afya bora ndipo wanapoweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo kuinua uchumi wao na
taifa kwa ujumla.
Mkuu wa kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo kote nchini kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji kama wanavyotoa michango ya harusi na sherehe nyingine.
Alisema ni jukumu la kima mmoja wetu wa kusaidia jamii na si
kuiachia serikali pekee na ndio maana kanisa hilo limekuwa likifanya hivyo kama neno la mungu linavyoelekeza kuwa tupendane kwani unapokwenda kumfariji mgonjwa inasaidia kumpa hali ya unafuu.
Akizungumza kwa niaba ya serikali na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu alilishukuru
kanisa hilo kwa msaada huo na kusema inazidisha ari ya kazi kwa wafanyakazi na kuwafariji wagonjwa ikiwa na kuwafanya wapate nafuu na kupona haraka.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Jumapili, 1 Januari 2017
UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni
Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze
(kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo,
ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa
sare za shule, daftari na penseli kwa watoto 200 watakaoanza darasa la
kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
Mtoto Issa Athumani akipokea msaada huo. Katikati mama yake Halima Issa.
Mtoto Asnat Mashaka akipokea msaada huo. Nyuma yake ni mama yake, Arat Hamisi
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho (kushoto), akizungumza kwenye tukio hilo.
Katibu Kata wa Kata ya Mnyamani (CUF), Omari Simba (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
Wazazi na walezi wakiwa na watoto wao wakisubiri kupokea msaada huo.
Vifaa hivyo vikiandaliwa kabla ya kukabidhiwa watoto.
wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Watoto na wazazi wao wakisubiri msaada huo. |
SERIKALI ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala kupitia Chama cha Wananchi (CUF), imetoa sare za shule kwa watoto 200 wanakaoanza darasa la kwanza mwezi Januari ili kuleta msukumo wa masomo katika mtaa huo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa mtaa huo, Jabiri Sanze alisema wanaziunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure na katika mazingira bora.
“Tumeamua kutoa msaada huu mdogo kwa watoto 200 waliopo katika mtaa wetu ili kutoa hamasa kwa wazazi na walezi kwani kipindi hiki cha mwezi Januari kinachangamoto kubwa na mahitaji mengi ya shule kwa wanafunzi” alisema Sanze.
Sanze alitaja msaada huo kuwa ni mashati ya shule, madaftari na penseli za kuandikia ambapo aliwaomba wazazi wasaidie eneo la sketi, kaputura, viatu na mabegi.
Alisema watoto walionufaika na msaada huo ni wavulana 86 na wasichana 114 wote kutoka katika mtaa wa Maruzuku.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho aliupengeza uongozi wa mtaa huo kwa mpango huo wa kuwasaidia watoto hao wanaotarajia kuanza darasa la kwanza na akawaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia ili kuwafikia watoto wote wa mitaa mitatu ya kata hiyo ambayo ni Mji Mpya, Mbarouk na Mnyamani.
Mjumbe wa mtaa huo Haroub Mussa aliwataka wazazi wa watoto waliopata msaada huo kutunza sare hizo na kuwa serikali ya mtaa itaendelea kushirikiana na wananchi na kuhakikisha watoto wote wanaopaswa kuanza darasa la kwanza wanakwenda shuleni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Jumapili, 1 Januari 2017
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWANDISHI WA HABARI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA AGIZO LA DC KAHAMA
TAARIFA KWA UMMA
UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC),na baadhi ya waandishi wa habari wilayani Kahama,wamekutana na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ili kupata muafaka wa tatizo la kukamatwa na kufikishwa mahakamani mwandishi wa habari wa kujitegemea Paul Kayanda.
Kikao hicho cha usuluhishi kilichofanyika leo Jumamosi Desemba 31,2016 katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo,kimehudhuriwa pia na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama.
Kayanda alikamatwa jana Desemba 30,2016 na kufikishwa mahakamani kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimtuhumu kuandika habari za kumdhalilisha na kuzisambaza kwenye barua pepe mbalimbali za vyombo vya habari.
Katika kikao ,Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,ulimuomba mkuu wa wilaya Nkurlu kutaka kufahamu kilichomsukuma kuchukua maamuzi hayo,na nini ushauri wake juu ya suala hilo lakini pia kumsikiliza mwandishi Paul Kayanda.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili,kikao kilibaini kuwepo kwa mapungufu katika habari iliyoandikwa na Kayanda kuhusu habari ya laptop mbili zilizoibiwa nyumbani kwa mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu huyo wa wilaya alikiri kuwepo kwa tukio la wizi nyumbani kwake lakini mwandishi huyo aliandika habari kwa kuingilia uhuru binafsi wa kiongozi huyo akielezea watu wanaoingia na kutoka nyumbani kwake lakini maisha anayoishi na kijana wake.
Kwa kuangalia maslahi mapana ya umma kutokana na kutegemeana katika kusukuma maendeleo ya jamii baina ya uongozi wa serikali na waandishi wa habari ,kikao kimemtaka Kayanda kumwomba radhi mkuu huyo wa wilaya kwa kuingilia uhuru wake binafsi na kuuhusisha na habari ya wizi wa laptop badala ya kujikita kwenye tukio la wizi wa laptop pekee.
Kikao pia kimebaini kuwa pamoja na mapungufu ya mwandishi, ni ukweli ulio wazi kuwa mkuu huyo wa wilaya aliibiwa kompyuta mpakato (lap top) mbili nyumbani kwake na kuagiza vijana watatu wakamatwe kwa mahojiano polisi akiwemo mmoja anayeishi nyumbani kwake japo ameelezea kuwa hakujua walishikiliwa kwa siku ngapi.
Mkuu huyo wa wilaya pia alieleza kukerwa na ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia simu ya mkononi (sms) alizodai kutumiwa na Kayanda kwa kutumia simu nyingine (tofauti na anayotumia) zenye lugha ya kumtuhumu na kumdhalilisha.
Hata hivyo kikao hakikuona kuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha kama ni za mwandishi huyo kweli au la huku kikao kikiomba sms hizo zifuatiliwe ili wamiliki wa namba hizo wajulikane .
Baada ya kujadiliana kwa kina katika kikao hicho kilichodumu kwa muda wa saa mbili,Kayanda amemwomba mkuu wa wilaya msamaha kwa mapungufu yaliyojitokeza katika habari hiyo aliyoiandika, na mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama amekubali kumsamehe mwandishi huyo akiahidi kufuata taratibu zingine kuondoa kesi mahakamani na kutaka kusafishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilikoandikwa habari hiyo.
Nkurlu amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari wilaya ya Kahama na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla katika kuandika habari zinazohusu serikali na akaomba kudumishwa kwa ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa serikali na waandishi wa habari ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya wananchi huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia weledi katika kazi zao.
Aidha Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga imewasisitiza waandishi wa habari kuzingatia weledi na kufuata maadili katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano isiyokuwa na tija kwa umma.
Pia tunawashauri wadau wote wa habari pindi inapotokea kuingia katika mgogoro wowote ama na waandishi wa habari au chombo cha habari si vyema kwenda mahakamani moja kwa moja bali wawasiliane na viongozi wa klabu za waandishi wa habari katika mkoa husika ili kusuluhishana na kuwekana sawa.
Imetolewa na
Kadama Malunde
MWENYEKITI –SPC
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu,waandishi wa habari na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama wakiwa katika kikao cha usuluhishi Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kahama
Kikao kinaendelea
Waandishi wa habari wakiondoka katika ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kikao kumalizika
CHANZO NI RWEYUNGA BLOG
Agizo la Waziri Mkuu kwa walimu wanaoishi mbali na shule zao
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza walimu wanaishi mbali na shule wakati
shule zao zina majengo wahame mara moja na warudi kuishi kwenye nyumba
za shule.
Amesema
haifai kuacha walimu waishi mbali na maeneo ya shule kwani hali hiyo
inachangia uchelewaji kazini na inapunguza muda wa kuwasimamia wanafunzi
au kuwasaidia jioni pale wanapohitajika kufanya hivyo.
Ametoa
agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chingumbwa, kata
ya Mbekenyera, wilayani Ruangwa Ijumaa, Desemba 30, 2016 kwenye mkutano
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi kijijini hapo.
“Nimeambiwa
kuwa walimu wako wachache kwa sababu hapa shuleni hakuna nyumba za
kuishi walimu. Mbona wanakaa Mbekenyera? Watawezaje kuwahi kazini
asubuhi wakati hawana magari? Mvua ikinyesha watafikaje shuleni? Kuanzia
leo, walimu wote warudi mara moja na waje kupanga hapa kijijini kwa
sababu nyumba zipo,” alisisitiza.
“Uamuzi
wa walimu kuishi jirani na shule ulifikiwa ili mwalimu awepo na
kuwasimamia wanafunzi wakati wakifanya usafi na wakati mwingine aweze
kutoa msaada kwa wanafunzi wanaojisomea jioni pindi wakihitaji msaada au
ufafanuzi,” alisema.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa,
Bw. Andrea Chezue asimamie zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
anapunguza walimu walioko Ruangwa mjini na kuwahamishia shule za
vijijini ambako kuna upungufu wa walimu.
Alisema
ili kusaidia juhudi za Serikali za kuboresha elimu nchini, ni vema kila
kijiji kikaweka utaratibu wa kuchangia matofali ili iwe rahisi kuanza
ujenzi wa nyumba za walimu.
Akiwa
katika kijiji cha Mkutingome, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la
Ruangwa aliwahamasisha wakazi wa kijiji hicho wachangie matofali 100
kutoka kila kaya ili yapatikane matofali 40,000 yatakayotumika kujenga
zahanati ya kijiji hicho.
Yeye
aliahidi kuwachangia mabati 150 ambayo kati yake, mabati 100 yatatumika
kuezekea zahanati ya kijiji na mengine 50 yatatumika kukamilisha nyumba
ya Mwalimu ambayo imekaa kwa muda mrefu bila kumaliziwa.
Katika
kuhakikisha ujenzi wa zahanati hiyo unaanza mara moja, Mkurugenzi wa
kampuni ya ujenzi ya Wanyumbani Construction, Bw. Fakihi J. Bakili
alichangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ya
kijiji cha Mkutingome. Nao Umoja wa Wachimbaji Wadogo katika mgodi wa
Namungo ambao uko jirani na kijiji hicho waliahidi kuchangia mifuko 50
ya saruji.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Sunday, January 1, 2017
Waziri Nchemba akutana na Mama wa Chid Benz.....Aeleza Alivyosikitishwa na Hali yake
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameguswa na hali ya
uathirika wa matumizi ya dawa za kulevya inayomtesa rapa Chid Benz na
kulazimika kufika nyumbani kwao kuzungumza na mama yake mzazi.
Chidi
Benz anayemiliki tuzo kadhaa za muziki alijikuta amenasa kwenye mtego
wa matumizi ya dawa za kulevya ambao sio tu ulimuondoa kwenye maisha ya
muziki bali pia uliidhoofisha afya yake na kuuondoa kabisa mwili wake wa
‘chuma’.
Kupitia
akaunti yake ya Instagram, Waziri Nchemba ameeleza kusikitishwa na hali
ya Chidi Benz na kutumia nafasi hiyo kuwataka wale wanaojihusisha na
biashara haramu ya dawa za kulevya kuacha mara moja kwani Serikali ya
Awamu ya Tano imeazimia kupambana nao.
Hivi ndivyo alivyoandika:
Nimekutana
na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo “Chid Benz”
ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na
haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika
kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge,
wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika
awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa
namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa
dola.
Mbali
ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA
kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya
kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.
Mswaada wa Urusi waungwa mkono na UNSC
Kansela Merkel apendekeza sheria mpya ili kuimarisha usalama
Serikali na upinzani zafikia makubaliano nchini Kongo
Trump huenda akakutana na rais wa Taiwan
SUNDAY NEWS 01/01/2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Januari 01, 2017
Rating:
Hakuna maoni