HABARI ZA JUUMATANO HII
Wednesday, January 4, 2017
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya January 4
Wednesday, January 4, 2017
Ziara Ya Rais Magufuli Kagera Yatumbua Watatu
Baada
ya Rais Dk. John Magufuli kuagiza watumishi wote wa Manispaa ya Bukoba
mkoani Kagera waliohusika katika ukarabati wa majengo ya Shule ya
Sekondari Omumwani ambayo yameonekana kutoendana na thamani ya fedha
zilizotumika wachunguzwe, watumishi watatu wa manispaa hiyo
wamesimamishwa kazi.
Watumishi
hao walisimamishwa jana na Katibu Tawala, Mkoa wa Kagera, Diwani
Athumani, baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu ya maji iliyomo katika
majengo ya shule hiyo.
Shule
hiyo ilikarabatiwa kuwapa hifadhi ya muda wanafunzi wa shule za
sekondari Ihungo na Nyakato zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera, Septemba 10, mwaka jana.
Baada
ya ukaguzi huo, Athumani alimtaka Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Bukoba, Chibunu Lukiko, kumtajia majina ya watumishi waliohusika moja
kwa moja katika usimamizi wa kila siku wa shughuli hiyo.
Katika
maelezo yake, Athuman alisema aligundua ukarabati uliofanywa ulikuwa
chini ya kiwango na hauendani na thamani ya Sh milioni 119 zilizotolewa
na Serikali.
“Kwanini
wakurugenzi hampendi kufuatilia miradi iliyo katika maeneo yenu? Kama
mngefuatilia mapema, mngegundua ubadhilifu uliofanyika hapa na kuchukua
hatua mapema.
“Kwa
hiyo, naagiza kuanzia leo Januari 3 (jana), mkurugenzi wa Manispaa ya
Bukoba uwasimamishe watumishi wote waliohusika ambao ni Mhandisi Kitengo
cha Ujenzi wa Manispaa ya Bukoba, Andondile Mwakitalu, Mhandisi
Msaidizi, Costane Felix na fundi Charles Kafumu.
“Hawa
lazima wasimamishwe ili kupisha uchunguzi utakaofanyika kwa ajili ya
kulinganisha kazi iliyofanywa na kiasi cha fedha kilichotumika kama
vinaendana.
“Tatizo
jingine nililoligundua ni kutokuwapo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo
kutoka kwa watumishi wa manispaa. Hao nao uchunguzi dhidi yao utafanyika
kwa uwazi na ukweli na hatutamwonea mtu.
“Sitaki kusikia shughuli hii inasimama eti kwa sababu ya hawa watu wamesimamishwa, fanya makabidhiano na wale watakaokuwapo.
“Kaimu
mkurugenzi hakikisha mnakabidhiana kila kitu, hata msumari usibaki na
uchague watu wengine wa kuendelea na kazi ya kusimamia mradi huu ili
ukamilike kwa muda uliopangwa,” alisema.
Naye
Mhandisi Mwakitalu aliyesimamishwa, alisema majengo hayo yalikuwa
katika hali mbaya na kwamba ukarabati wake unahitaji fedha nyingi ili
yarudi katika hali yake ya kawaida.
Wednesday, January 4, 2017
Ningekuwa Diamond nisingejiita simba – Darassa
Hit
maker wa wimbo ‘Muziki’ Darassa ameweka wazi maana ya ule mstari wake
wa “sio simba, sio chui, sio mamba” kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita
simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.
Darasa
amedai Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo
mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa
kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama
Simba.
“Ningekuwa
Diamond nisingejiita simba,” Darassa alikiambia kipindi cha Enewz cha
EATV. “Ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba,
simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu
anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote
kubwa, kafanya vitu vingi sana,”
Pia
rapper huyo alidai wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake
hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na
anajiamini kwa muziki wake anaofanya.
“Kwa
upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama
anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter
mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo,
ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah”. Amemalizia
Darassa
Wednesday, January 4, 2017
Waziri Mkuu Aagiza Umeme Wa Uhakika Kisarawe II
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II linakuwa na umeme wa
uhakika ili kuwezesha viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata nishati
hiyo.
Alitoa
agizo hilo jana jioni (Jumanne, Januari 3, 2017) wakati alipotembelea
kiwanda cha Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na kiwanda cha
Watercom kinachozalisha maji vilivyoko katika kata ya Kisarawe II
wilayani Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.
“Waziri
wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata umeme wa uhakika ili
kuviwezesha viwanda hivi kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza
uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika maeneo haya nao watanufaika na
upatikanaji wa nishati hiyo,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema amefarijika na jitihada za muwekezaji huyo za kuunga mkono
mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya Tanzania kujenga
uchumi wa viwanda utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025.
Awali,
Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar Faraj akisoma taarifa ya viwanda
hivyo kwa Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto zinazowakabili ni
pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo linasababisha kupanda
kwa gharama za uzalishaji.
“Punde
umeme unapokatika tunalazimika kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii
husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji ambazo huumiza kiwanda kwa
sababu haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,” alisema.
Faraji
alisema changamoto nyingine ni miundombinu ya barabara ambayo
usababisha wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda hivyo kwa
urahisi, hivyo aliiomba Serikali kuwatatulia kero hilo.
Aliongeza
kuwa kwa sasa viwanda hivyo vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo
alisema endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa umeme na barabara
wataongeza ajira kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2018.
Mapema
Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe II
iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi hiyo yenye
vyumba vitatu itawapunguzia akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata
huduma hiyo.
Wednesday, January 4, 2017
Majaliwa Akagua Maghala Ya Hifadhi Ya Chakula Chang'ombe Dar Es Salaam
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati
alipotembelea maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari
4, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala
ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar
es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala
ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar
es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wednesday, January 4, 2017
UVCCM Wampongeza Rais Magufuli Kwa Kumtumbua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kuwa umefurahishwa na
kitendo cha Rais Magufuli cha kupigania maslahi ya wanyonge na kuzuia
kupandisha bei ya umeme nchini.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka wakati wa
kikao cha watumishi wa umoja huo wa kutathmini utendaji kazi wa mwaka
2016 na kuweka utendaji wa mwaka huu.
Shaka
amesema kitendo cha Rais Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesm Mramba, ameonyesha
uzalendo, ujasiri na upendo kwa wananchi ambao walimpa dhamana ya
kuongoza nchi.
“UVCCM
tunaunga mkono uamuzi wa Rais wa kuzuia kupanda kwa bei ya umeme na
ametazama maslahi ya wananchi waliomchagua kuingia madarakani,”amesema
Shaka.
Hata
hivyo, amesema kuwa Tanesco kupitia kwa Mkurugenzi wake Mramba
aliyetumbuliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
waliwaahidi wananchi kutopandisha bei ya umeme.
Wednesday, January 4, 2017
Mkuu Wa Jeshi La Polisi Nchini, Igp Ernest Mangu Atuma Timu Ya Maofisa Wa Jeshi La Polisi Kwenda Zanzibar Kuchunguza Vitendo Vya Udhalilishaji
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa wa
Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda
Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya
udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa
vikiripotiwa mara kwa mara.
Timu
hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na
kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo
ikiwemo kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani.
IGP
Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi
za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili
kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Wednesday, January 4, 2017
Anaswa na polisi akifukua kaburi la albino
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kufukua
kaburi la marehemu ambaye likuwa ni mlemavu wa ngozi (Albino)
aliyefariki mwaka 2010 kwa lengo la kuchukua viungo vyake.
Taarifa
ya jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda a Polisi Mkoani Mbeya DCP Dhahiri
Kidavashari inasema kuwa mnamo tarehe 03.01.2017 majira ya saa 01:00
usiku katika Kijiji cha Mumba kilichopo Kata ya Ilembo, mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la JONAS JOHN mkazi wa Chapakazi alikamatwa na
askari Polisi akiwa na wenzake wawili wakifukua kaburi la marehemu
SISTER OSISARA aliyekuwa mlemavu wa ngozi (ALBINO)
Inadaiwa kuwa marehemu alifariki dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha Mumba.
Mtuhumiwa
alikutwa na majembe na makoleo ambayo walikuwa wakiyatumia kufukuria
kaburi hilo. Baada ya mahojiano mtuhumwa huyo aliwataja washirika
wenzake wawili ambao walikimbia baada ya kuwaona askari.
Jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa .
Katika
tukio lingine Mnamo tarehe 03.01.2017 majira ya saa 3:30 usiku katika
kata ya Makongolosi wilayani Chunya, mkoa wa Mbeya, mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la KELVIN KUBANDA mkazi wa Kahama alikamatwa
akiwa na bhangi kete 10 sawa na uzito wa gramu 55.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa katika kijiwe cha kuvutia Bhangi. Upelelezi unaendelea.
Jumatano, 4 Januari 2017
BALOZI SEIF AZINDUA NYUMBA ZA KUISHI MAAFISA NA ASKARI WA UHAMIAJI, PEMBA
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilikagua Jengo la
Gorofa Mbili litakalobeba Familia Sita za Maafisa na Askari wa Uhamiaji
baada ya kulizindua rasmi hapo Mtaa wa Mtukitu Chake chake Kisiwani
Pemba ikiwa ni sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Maafisa wa Uhamiaji na
Wizara ya Mambo ya Ndani walioshuhudia ufunguzi wa Jengo la Makaazi ya
Maafisa na Askari wa Uhamiaji chake chake Pemba.
Kulia ya Balozi Seif ni Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari
Msoud Sururu,Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Gneral Projestus
Rwegasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mh., Mohamed Aboud Mohamed.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Mwnajuma
Majid,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiam Iddi
na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo
Juma N’hunga.
Muonekano
wa Haiba ya Jengo Jipya la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji
liliopo katika Mtaa wa Mtukitu Chake Chake Kisiwani Pemba.
Kamishna
wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu akitoa Taarifa ya
ujenzi wa jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji wakati wa
hafla ya kulizindua rasmi.
UVCCM LONGIDO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA
Kushoto ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu
Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel na Mjumbe Baraza Kuu
UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa
kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation Joyce Kabati
Kushoto ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu
Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel na Mjumbe Baraza Kuu
UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa
kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation Joyce Kabati
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.
Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.
Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.
“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao” Neema
Katibu wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.
Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.
Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.
Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.
“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao” Neema
Katibu wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.
Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.
Mbunge Lwakatare wa CHADEMA Ammwagia Sifa Rais Magufuli
Serikali Yafuta Posho Za Vitafunwa, Mazingira Magumu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini
kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali
zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.
Ametia
agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na
watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.
“Kuanzia
sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo
za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu
na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,”
amesema.
Agizo
hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa
zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa
zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.
Aidha,
Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu
wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na
watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
“Katika
halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato
hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache
wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili
haliwezekani,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho
hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.
Aidha,
ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya
kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala
yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa
kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama
ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake.
Pia
amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na
kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka
vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri
hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika
Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Awali
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha
taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya
watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti
isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
EWURA yatangaza bei mpya za mafuta
Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza bei
mpya za nishati ya mafuta zitakazoanza kutumika kesho Jumatano huku bei
ya mafuta ya taa na dizeli ikiwa imeshuka kwa wastani wa shilingi 66
kwa lita.
Taarifa
iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi
inaonesha kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la bei ya
mafuta ya petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa kwa bei
ile ile ilivyokuwa mwezi uliopita.
Hata
hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa
mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo chini ya bei elekezi
iliyotangazwa na mamlaka hiyo kama njia ya kuchochea ushindani baina ya
wauzaji wa mafuta nchini.
Utata Wagubika Mauaji ya Afisa Mtendaji Mbeya
Mwili
wa ofisa mtendaji wa mtaa wa Kabwe, katika kata ya Iyela jijini Mbeya
Clementine Enock (34) umekutwa ukiwa umetelekezwa katika eneo la Airport
ya zamani baada ya kuuawa na watu wasiofahamika kwa kubanwa pumzi.
Kamanda
wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari alisema jana kuwa walibaini
kuwepo kwa mwili huo Januari mbili, mwaka huu majira ya saa moja asubuhi
baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kidavashari
alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo marehemu aliondoka nyumbani kwao
siku ya Mwaka mpya na kuaga kuwa anakwenda Airport kwenye sherehe ya
rafiki yake huku akiwa na gari yenye namba za usajili T234 DJM aina ya
Toyota Spacio.
Alisema
kuwa ndugu wa marehemu walipata hofu mara baada ya ndugu yao kuchelewa
kurudi nyumbani na ndipo wakaanza kumpigia simu bila mafanikio mpaka
usiku wa manane.
“Marehemu
aliaga nyumbani kwao Uyole ya Kati alikokuwa akiishi majira ya saa kumi
jioni siku ya tarehe moja kwa madai anaenda kwenye sherehe ya rafiki
yake akiwa na usafiri wa gari lake, ambapo mpaka kufika usiku wa manane
hakukuwa na taarifa yeyote ndipo hofu ikatanda kwa familia ambapo
walipiga simu kwa ndugu jamaa na marafiki na kueleza kuwa hawajui
alipo,” alisema Kidavashari.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari siku iliyofuata majira ya saa moja
asubuhi mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo la wazi
jirani na Shule ya Sekondari ya Samora ambapo uchunguzi wa awali
unaonesha kifo chake kilitokana na kubanwa pumzi na watu wasiofahamika.
Alisema
mazingira ya kifo yanaonyesha wazi kuwa marehemu aliuawa na mtu wa
karibu yake huku akisema tukio hilo lilifanywa ndani ya nyumba ya mtu.
TCRA Yatishia Kuzifutia Leseni Kampuni za Simu
Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetishia kusitisha kwa muda au kufuta
kabisa leseni ya biashara kwa kampuni zote za mawasiliano nchini,
zitakazoshindwa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
Hatua
hiyo ni kulingana na sheria mpya ya fedha ambayo imetoa ukomo wa hadi
Desemba 31 mwaka jana kampuni hizo ziwe zimejisajili katika soko hilo.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam hii leo; Mkurugenzi Mkuu wa TCRA
Mhandisi James Kilaba amesema kwa sasa wanasubiri maelezo kutoka Mamlaka
ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuhusu idadi ya kampuni za
mawasiliano zilizokidhi sifa za kusajiliwa katika soko la hisa kwa ajili
ya kuchukua hatua kwa zile zilizokaidi kutekeleza agizo hilo la
kisheria.
Mhandisi
Kilaba amesema TCRA imeikabidhi CMSA orodha ya kampuni zaidi ya 80 za
mawasiliano, orodha ambayo CMSA itaipitia kwa lengo la kuchuja na kupata
kampuni ambazo zinastahili kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es
Salaam.
Kauli
ya Mhandisi Kilaba imekuja huku taarifa kutoka soko la Hisa la Dar es
Salaam zikionesha kuwa ni kampuni tatu pekee ndizo zimejisajili katika
soko hilo, licha ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo wake Jumamosi ya
Desemba 31 mwaka jana.
Serikali kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.........Wale wa Maomo Mengine Watulie Maana Hakuna Uhaba Kwa Sasa
Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakati akiwa katika ziara yake ya kutembela wilaya mpya za jiji hilo,
akianzia na Kigamboni siku ya leo.
Majaliwa
amesema mchakato wa ajira hizo unaendelea chini ya Ofisi ya Rais
Utumishi, na muda wowote kutoka sasa mchakato huo utakapokamilika,
majina yatatolewa na walimu hao kuajiriwa.
Kuhusu
walimu wa masomo mengine, Waziri Mkuu amesema walimu wa masomo mengine
hususani ya sanaa wapo wa kutosha na kwamba wanapaswa kusubiri kwakuwa
wao wako wengi zaidi na hakuna uhaba na uhitaji wa walimu hao wa masomo
ya sanaa.
Hivi
karibuni, Wizara ya Elimu iliwataka wahitimu wa ualimu katika masomo ya
sayansi na hisabati kutuma taarifa (CV) zao ili izihakiki kabla ya
ajira, mchakato ambao tayari umekamilika na majina yalitumwa katika
wizara ya utumishi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya wiki mbili zilizopita wakati
akiongea na kituo cha EATV alisema kuwa kazi ya wizara yake ilikuwa ni
kuhakiki taarifa za wahitimu hao, na si kuajiri, huku akibainisha kuwa
zoezi hilo limekamilika na majina yako utumishi ambao ndiyo watahusika
na kuajiri.
Pia
alisisitiza kuwa kama wizara ya elimu waliomba kupewa walimu wa masomo
ya Sayansi na Hisabati haraka kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa zaidi na
kuwataka wahitimu wote waliotuma taarifa zao, wasubiri watapata majibu
muda si mrefu.
Wednesday, January 4, 2017
Polisi kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha
Familia
moja jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike
wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa
kuwa binti huyo yupo hai.
Taarifa
za kisa hicho cha kusikitisha zimevifikia vyombo vya usalama. Kwa sasa
kuna mipango ya kuhakikisha kuwa mwili wa binti huyo, Nuru Losipha
aliyezikwa kwa siri na familia yake, unafukuliwa kwa uchunguzi zaidi.
Inadaiwa
kuwa Losipha alipoteza maisha wakati akifanyiwa tohara au ukeketaji na
ngariba, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, huku familia yake
ikishuhudia.
Kitendo
hicho kilifanyika katika kijiji cha Engutoto Kata ya Mwandeti wilayani
Arumeru Desemba 28, mwaka jana, zikiwa zimebaki takriban siku tatu tu,
kabla ya mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitatu tu, hajaingia
mwaka mpya wa 2017.
Mtendaji
wa Kata ya Mwandeti, Njivaini Kivuyo awali alikuwa amepitwa na taarifa
hizo hadi vyombo vya habari vilipotinga kijijini hapo kwa uchunguzi na
ndipo alipolazimika kwenda kuripoti tukio hilo kwenye kituo cha Polisi
cha Ngaramtoni.
Kamanda
wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo aliapa kuwa liwalo na liwe na
kwamba ikiwezekana kaburi litafukuliwa ili mwili wa malaika huyo asiye
na hatia, uchunguzwe upya.
“Ndio
kwanza nazipata hizi taarifa, na kama polisi tutaomba kibali cha
mahakama ili twende kulifukua kaburi husika tujiridhishe kama kweli
mtoto huyo amezikwa humo na iwapo tutaukuta huo mwili, basi tutaanza
uchunguzi juu ya kifo chake,” alisema Kamanda arles Mkumbo.
Baba
wa marehemu, Losipha Kaiser anadai kuwa mtoto wake alifariki kutokana
na ugonjwa wa baridi yabisi na kwamba aliugua kwa kipindi kirefu kabla
ya kupoteza maisha Desemba 28, mwaka jana. Lakini madai yake hayo
yanapingana na ripoti ya muuguzi katika duka la dawa lililopo kijiji cha
jirani cha Kidali, anayeitwa Jane Andrew.
“Walimleta mtoto hapa walitaka nimsaidie tiba, lakini tayari huyo binti alikuwa amezimia na kutokwa na damu nyingi,” alidai.
Muuguzi huyo aliwahimiza wamkimbize mtoto hospitali, na hakufahamu nini kiliendelea hadi ripoti za kifo zilipomfikia.
Huku
serikali ikipiga marufuku vitendo vya ukeketaji kwa wasichana, bado
kuna familia nyingi kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa,
zinaendeleza mila hiyo kwa siri.
Kwa sasa familia hizo zimegundua mbinu mpya ya kuwatahiri watoto wa kike wakiwa wadogo sana, kuepuka kukamatwa.
Ngariba
wanaotumika kukeketa watoto, mara nyingi ni akina mama vikongwe
wasiokuwa na ujuzi, taaluma za afya na hutumia vifaa butu, ambazo
husababisha uvujaji mwingi wa damu na kuwa chanzo cha maambukizi ya
magonjwa mengine.
Wednesday, January 4, 2017
Mlinzi mwingine auawa Geita....Aliyepigwa na wafugaji Morogoro Afariki Dunia
Mkuu wa
Wilaya ya Geita, Herman Kapufi
Mauaji ya walinzi mkoani Geita yamendelea kuwa tishio kwa usalama wao baada ya mlinzi mwingine aliyekuwa akilinda maduka yapatayo 15, kuuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Mauaji ya walinzi mkoani Geita yamendelea kuwa tishio kwa usalama wao baada ya mlinzi mwingine aliyekuwa akilinda maduka yapatayo 15, kuuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Mauaji ya mlinzi huyo Kisusi Iddy (40) aliyekuwa
akilinda maduka hayo kwenye Mtaa wa Mwatulole, ni muendelezo wa matukio
ya kuuawa walinzi wa maduka na mali mbalimbali kwani katika kipindi cha
miaka miwili jumla ya walinzi 20 wameuawa.
Taarifa
zilizopatikana jana kuhusu mauaji ya mlinzi huyo na kuthibitishwa na
mwenyekiti wa mtaa huo, Fikiri Toi zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia Januari Mosi na wauaji hao hawakuiba kitu chochote.
Mwili wa Iddy ulikutwa umefunikwa kwa shuka lake alilokuwa akilitumia
lindoni, huku likiwa limetapakaa damu.
Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa
Wilaya ya Geita, Herman Kapufi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama amefuta vibali vyote vya waganga wa tiba za asili kwa
madai wao ni moja ya chanzo cha imani za kishirikina zinazosababisha
mauaji hayo.
Alisema kutokana na kukithiri kwa mauaji hayo, mamlaka yake
inakusudia kufufua Jeshi la Jadi (Sungusungu) ili kusaidia kuyadhibiti.
Hata hivyo, Kapufi alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa wakati wa
uhai wake, Iddy alikuwa analinda maduka ya wafanyabiashara yanayofikia
15 na kwamba baada ya kufuatilia, hakuwa na mafunzo yoyote ya ulinzi.
Aliyepigwa na wafugaji Moro afariki
Fabian Bago (21) anayedaiwa kushambuliwa na wafugaji katika Kijiji cha Kolelo, Morogoro, amefariki dunia
katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Frank Jacob alisema kijana
huyo alifariki dunia saa 11 jioni jana akiwa kwenye wodi ya wagonjwa
wanaohitaji uangalizi wa karibu na kwamba mwili wake umehifadhiwa
kusubiri taratibu nyingine za kipolisi.
Dk Jacob alisema mara baada ya
kufikishwa hospitalini hapo, kijana huyo alifanyiwa vipimo na matibabu
lakini alifariki dunia kutokana na majeraha makubwa kichwani
yaliyoharibu sehemu ya ubongo.
Baba mzazi wa kijana huyo, Alan Bago
alisema ameshatoa taarifa polisi kuhusina na kifo cha kijana wake na
sasa anasubiri maelekezo ya polisi ili aweze kuendelea na taratibu za
mazishi.
Wednesday, January 4, 2017
Zitto Kabwe Adai Kuna Uhaba Mkubwa wa Chakula Nchini.........Waziri wa Kilimo Ampinga
Wakati Mbunge wa
Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akidai kuwa hali ya chakula
nchini siyo nzuri kutokana na uhifadhi mbaya, Serikali imesema hali ni
shwari licha ya baadhi ya maeneo kutopata mvua za wastani.
Zitto alidai
jana kuwa Ghala la Taifa la Chakula (SGR) lina hifadhi ya chakula
kinachotosha kwa siku nane tu wakati Novemba 2015 kulikuwa na chakula
cha kutosha miezi miwili.
Kwa mujibu wa Zitto, taarifa ya Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) ya Novemba inaonyesha kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya
Chakula (NFRA), imebaki na tani 90,476 tu za chakula ambacho amedai ni
cha kutosholeza siku nane.
Hata hivyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Dk Charles Tizeba alijibu madai hayo ya Zitto akisema nchi ina
chakula cha kutosha wala siyo cha siku nane wala mwezi pekee, bali
zaidi.
Dk Tizeba alisema NFRA inakuwa na akiba ndogo kwa kuwa mwaka 2016 ndiyo ambao nchi ilipata mavuno makubwa ya tani milioni 16 ambazo hazikuwahi kutokea, hivyo maghala ya watu bado yana akiba kubwa ya chakula hivyo wakala haukununua chakula kingi.
Dk Tizeba alisema NFRA inakuwa na akiba ndogo kwa kuwa mwaka 2016 ndiyo ambao nchi ilipata mavuno makubwa ya tani milioni 16 ambazo hazikuwahi kutokea, hivyo maghala ya watu bado yana akiba kubwa ya chakula hivyo wakala haukununua chakula kingi.
“NFRA inanunua chakula
kwa kuangalia mahitaji kwa mwaka huo ukoje, watu wakivuna sana maghala
yao yanakuwa yamejaa na mahitaji ya chakula yanakuwa madogo ndiyo maana
Serikali hainunui chakula kingi. Miaka miwili iliyopita Serikali
ilinunua mahindi kwa wingi lakini yaliishia kuharibika,” alisema Dk
Tizeba.
Aliongeza kuwa Serikali sasa ina mradi wa kujenga ghala jingine
lenye uwezo wa kuhifadhi tani 260,000 ili likiungana na la sasa lenye
uwezo wa tani 246,000 nchi iwe na uwezo wa kuhifadhi tani zaidi ya
500,000.
“Kuna maeneo mahindi yameanza kukomaa na wakulima wa huko
watavuna kama kawaida, tunachokifanya tutadhibiti uuzaji wa chakula nje
ya nchi bila vibali ili chakula kisambae zaidi kwa Watanzania. Japo
siwezi kutaja kiasi cha chakula kilichopo kwa sababu za kiusalama, ila
kinatosha siyo kwa siku nane wala mwezi mmoja bali ni zaidi,” alisema Tizeba.
Juzi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za udiwani
katika kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, Zitto alisema
kauli ya Rais John Magufuli kwa wananachi wa Mkoa wa Kagera kwamba
Serikali haina shamba ni kuficha uamuzi unaosababisha kukosekana kwa
akiba ya chakula ya kutosha.
Alidai kuwa hali ya chakula nchini si
nzuri, wananchi wanashuhudia namna bei za vyakula zinavyopanda kila siku
akidai kuwa bei ya sembe na mchele zimekuwa juu na gharama za maisha
zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.
“Hali ya chakula inazidi kuwa
mbaya kwa sababu ya maamuzi mabovu ya Serikali kuhusu hifadhi ya
chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula
cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie sokoni,
hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula,”
alisema Zitto.
Aliongeza kuwa mpaka sasa NFRA ina tani 90,476 za
chakula wakati kipindi kama hicho mwaka 2015 ghala la chakula lilikuwa
na tani 459,561.
Takwimu alizozitoa Zitto Kabwe alizinukuu katika ripoti
ya BoT ya Novemba mwaka jana ambayo inaonyesha kuwa tangu Januari 2016
hadi Julai 2016, akiba ya chakula ilipungua kutoka tani 125,668 hadi
49,632, lakini hadi Oktoba mwaka huo iliongezeka hadi 90,476.
Ripoti
hiyo inaonyesha tofauti ya uhifadhi wa chakula kwa mwaka jana na miaka
mingine miwili iliyotangulia kwani mwaka 2014 Januari, kulikuwa na tani
235,309 na Desemba, tani 466,583 huku mwaka mwaka 2015 Januari kukiwa na
tani 459,561 na Desemba 180,746.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa
Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Steven Ruvuga alisema hali
halisi kwa wakulima siyo nzuri kwa kuwa mvua zilinyesha chini ya
kiwango, hivyo kuna hofu ya ukosefu wa chakula cha kutosha baadaye.
“Sasa hivi nipo Kiteto na kwa kawaida mahindi yalipaswa kuwa tayari
yameinuka kufikia walau mabega ya mtu mzima, lakini nikiyatizama sasa
bado yako chini.
"Mwaka huu kuna hatari ya ukosefu wa chakula na
naishukuru Serikali kwa kuwa imeanza kuchukua hatua katika maeneo yenye
uhitaji,” alisema Ruvuga.
Aliongeza kuwa Ghala la Taifa linapaswa kuwa
na wastani wa tani 300,000 za akiba lakini kama sasa zipo 90,476
zinaweza zisikidhi mahitaji ya kila mtu hivyo ni vyema ikabuni mpango
mbadala.
HABARI ZA JUUMATANO HII
Reviewed by RICH VOICE
on
Januari 04, 2017
Rating:
Hakuna maoni