BREAKING: Majambazi Yavamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia Mbezi na Kupora Sadaka
Majambazi
wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto
Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya
vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha wa parokia hiyo, Arnold Kimanganu
amesema kuwa majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia
kanisani.
“Majambazi
walivyofika waliwapiga walinzi, tuna walinzi wanne walimshika mlinzi
mwenye silaha wakampiga na kumnyang’anya bunduki, kumkamata mwingine
wakampiga na kumfunga na wakaingia sehemu inaitwa sakristia, wakavunja
milango ya sakristia wakakusanya matoleo yote yaliyokuwa yamehifadhiwa
yaliyokusanywa kipindi cha pasaka,” amesema Kimanganu.
Paroko
wa parokia hiyo, Sunil Kishor amesema majambazi hao walivamia kanisa
hilo saa tisa usiku na wameiba fedha na baadhi ya vifaa vya kuendesha
misa.
“Ni
kweli majambazi walivamia kanisa letu majira ya saa tisa alfajiri,
walichochukua kuna pesa za sadaka ambazo zilikuwepo sakristia, vifaa vya
misa hasa vikombe na siborio,” amesema Paroko Kishor na kuongeza kuwa;
“Kiasi
cha fedha ambacho wamechukua kadri ya hesabu ni kama milioni nane hivi,
Tumesharipoti polisi na wapo hapa kanisani wanaendelea na uchunguzi.”
Akithibitisha
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa amekiri kutokea ingawa bado hajapata taarifa ofisini kwake
kimaandishi .
‘’Ni
kweli vibaka walivamia na wameiba sadaka, lakini bado sijalipata vizuri
tukio hili nikilipata nitalitolea taarifa, lakini nathibitisha kutokea
kwa tukio hilo,” amesema Kamanda Mambosasa.
BREAKING: Majambazi Yavamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia Mbezi na Kupora Sadaka
Reviewed by RICH VOICE
on
Aprili 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni