Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC

Taarifa kutoka duru za karibu za uchunguzi wa kesi hiyo ya kubaka vinasema kwamba gavana huyo alimbaka binti huyo siku ya Jumamosi.
Bwana Bikamba ambaye kwa sasa yuko gerezani anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo ili aweze kujibu mashtaka yake ya kumwekea dawa ya kulevywa na kumfanyia tendo la ngono binti bila idhaa yake.
Wakili wa gavana huyo, Imbambo Engulu ametupilia mbali tuhuma hizo na kushutumu mahakama ya jimbo hilo kwa kumzuia gavana huyo bila kujali na cheo chake
"Kushikwa kwake ni kama uonevu, tuliomba wamuzuie kwanza nyumba kwake badala ya kumuweka gerezani moja kwa moja, majaji hawakukubali ombi letu, Nawambia kweli kuwa gavana hakufanya kitendo hicho, ni uongo."
Waziri wa sheria ,Faida mwangiliwa ambaye pia ni miongoni mwa wanaharati wa haki za wanawake ameomba sheria kumhukumu vikali gavana huyo ikiwa tuhuma hizo zitathbitishwa na mahakama
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya kongo tayari kuathibu vikali askari kadhaa na maafisa wa jeshi la Kongo wengi kwa kuwapa kifungo cha maisha .
BY BBC SWAHILI
Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC
Reviewed by RICH VOICE
on
Aprili 04, 2018
Rating:
Hakuna maoni