Milio ya risasi yasikika kwenye makao makuu ya YouTube

media
Mwanamke mmoja aliwajeruhi kwa risasi watu watatu, ambapo mmoja yuko katika hali mbaya. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne kwenye makao makuu ya YouTube karibu na mji wa San Francisco, nchini Marekani na kusababisha hofu miongoni mwa wafanyakazi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama mshambuliaji alijiua baada ya kisa hicho.
Polisi inasema shambulio hilo linahusiana na mgogoro wa kibinafsi lakini vyombo vya habari vimetoa maelezo tofauti kuhusu wasifu wa mshambuliaji huyo.
Kwa mujibu wa gazeti la San Francisco Chronicle, mtuhumiwa, anayetambuliwa kama mwanamke kutoka kusini mwa California, alikuwa na chuki dhidi ya YouTube, akiishutumu kwenye tovuti yake kutorusha video zake, ambapo baadhi ya video hizo zinaonyesha wanyama wakiteswa. Kwa mujibu wa gazeti la Mercury News, baba wa mwanamke huyo amethibitisha kwamba mwanae alikua na chuki dhidi ya You Tube.
Kwa mujibu wa polisi, ambayo haikutaja jina lolote, mwanamke mmoja aliwapiga risasi watu kwenye makao makuu ya YouTube wakati wa chakula cha mchana, kabla ya kujiua kwa bunduki yake.
 
CHANZO-RFI
Milio ya risasi yasikika kwenye makao makuu ya YouTube Milio ya risasi yasikika kwenye makao makuu ya YouTube Reviewed by RICH VOICE on Aprili 04, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...