Wema Sepetu: Sioni Wivu Diamond Kumkumbatia Hamisa Mobeto
Wakati
habari zilizopo mjini kwa sasa ni tukio la mwanamitindo Hamisa Mobetto
na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ kuteka tukio la utoaji
tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF),
kwa mrembo Wema Sepetu yeye kaichukulia kawaida.
Diamond
na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika jana ukumbi wa Mlimani City ,
walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa
mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa
filamu ya Safari ya Gwalu.
Katika
kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema
ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven
Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo
hivyo haikuwa yake.
Akizungumzia
namna alivyochukulia kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo
na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond
miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana,
amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na
Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.
“Wee
ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani ,
ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na
Diamond bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema,”amesema
Wema.
Kuhusu
hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la
watu (People’s Choice Award) kupitia filamu yake ya ‘Heaven Sent’, Wema
amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.
Pia,
aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu
wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo
kweli bali ilikuwa imelala tu.
Hata
hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni
kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha
anapata ushindi huo.
by rich voice
Wema Sepetu: Sioni Wivu Diamond Kumkumbatia Hamisa Mobeto
Reviewed by RICH VOICE
on
Aprili 02, 2018
Rating:
Hakuna maoni