Nikki Mbishi aeleza hisia zake kuhusu Wasafi TV, Babu Tale amjibu
Nikki Mbishi amesema alichofurahishwa zaidi na kituo hicho ni kwamba kimeanza kwa kupiga nyimbo mchanganyiko na bila ubaguzi kitu ambacho kinapelekea ushindani wenye usawa ambao awali haukuwepo kwenye media nyingine.
“Asante Wasafi TV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea, najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi. Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition” hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo fitna zipo tu,“ameandika Nikki Mbishi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuelezea zengwe zilizokuwa zinafanywa na vituo vingine.
“Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA” Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba. Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe.“ameeleza Nikki Mbishi.
Hata hivyo, pongezi na ushauri huo umepokelewa kwa mikono miwili na Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale. Ambapo amemjibu kwa kushukuru “Asante bwana UNJU hii ni yetu sote na tunaamini hata kwengine wataanza kupiga kwenye kuweka usawa. Mwanzo mgumu ila Mungu atatusimamia sababu tunania ya kweli na sio ushindani na mtu. Haya mtag msanii yeyote ambaye aujamuona akichezwa kokote ili huku kwao aanze kupigwa maana hii ni ya kwetu sote @wasafitv “.
Mwaka 2016, rapa Nikki Mbishi aliingia kwenye headline baada ya kutoa wimbo wake wa ‘Babu Talent’ ambao mashabiki wengi waliutafsiri kama dongo kwa Babu Tale, ambapo wimbo huo unamzungumzia mtu ambaye ananyonya wasanii wa muziki na kubania baadhi ya kazi zao kutoka.
Nikki Mbishi aeleza hisia zake kuhusu Wasafi TV, Babu Tale amjibu
Reviewed by RICH VOICE
on
Aprili 04, 2018
Rating:
Hakuna maoni