Monday, October 24, 2016

Serikali kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo kwa kipaumbele

SeeBait

Serikali ipo katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Serikali inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

“Serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”

Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Monday, October 24, 2016


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya Octoba 24



SeeBait
MAGAZETI HAYOOOOOOOOOOOO





























Monday, October 24, 2016


Mbowe aikumbuka Oparesheni UKUTA.....Asema Serikali inaendeshwa kwa hila



SeeBait



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema Demokrasia, Katiba na Sheria haziheshimiwi na kwamba  Jeshi la Polisi limekuwa wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kilichofanywa kwenye uchaguzi wa umeya wa Manispaa ya Kinondoni kinawapa sababu ya kurejea operesheni yao wanayoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA).



Mbowe amesema hayo Oktoba 23, 2016 alipofika eneo ulipofanyika uchaguzo wa Meya Kinondoni ambapo madiwani wa Ukawa walisusia uchaguzi huo na kudai kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli, ameshirikiana na CCM kuhujumu zoezi hilo, hivyo wametangaza kwenda mahakamani kupinga uchaguzi huo baada ya CCM kuendelea na uchaguzi huo na kutangaza mshindi.



Njama zinazodaiwa kufanywa na mkurugenzi huyo ni kugawanya madiwani kinyume na kanuni kwa kuhamisha madiwani wa upinzani kwenda Halmashauri ya Ubungo na kuwahamishia Kinondoni madiwani wa CCM kutoka halmashauri nyingine.



Mbowe amesema Serikali inaendeshwa kwa hila kwani licha ya uchaguzi kufanyika siku ambayo si ya kazi,  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, alikataa barua iliyoandikwa na madiwani Jumamosi Oktoba 22 kuzuia uchaguzi huo kwa kudai kuwa si siku ya kazi.



Aliendelea kwa kumlaumu Rais Dk. John Magufuli kwamba ameanzisha utamaduni wa kuuwa demokrasia na kwamba analiletea taifa madhara makubwa.



Kwa upande wake Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema),  amesema wametoka kwenye uchaguzi huo baada ya baadhi ya madiwani wao kuzuiwa kuingia kwenye kikao hicho.



Mdee alisema kuwa  CCM wameingiza madiwani ambao si wajumbe halali wa kikao hicho kwasabau wanatoka katika halmashauri zingine.



“Humo ndani yumo Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa na alisajiliwa kama mkazi wa Ilala na alipiga kura za umeya Ilala hivyo mnaweza kuona uhuni unaofanywa.



“Lakini yumo pia Tulia Akson (Dk. Tulia Akson, Mbunge wa Kuteuliwa na Naibu Spika) ambaye si mkazi wa Kinondoni yeye amesajiliwa kama mkazi wa Ubungo,” alisema Mdee.



Amesema kwa mujibu wa kanuni Halmashauri moja haiwezi kuwa na wabunge wa kuteuliwa zaidi ya watatu na kueleza kuwa katika kikao hicho wamo wabunge wanne wa kuteuliwa.



Hivyo, kutokana na hali hiyo Mdee amesema watakwenda mahakama ili kupata tafsiri za kisheria za suala hilo kupata haki.

Monday, October 24, 2016


Makamba asikitishwa na upungufu wa maji katika Ziwa Rukwa....Atoa maagizo kwa wakurugenzi

SeeBait

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.

Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.

“Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.

Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru Ziwa Rukwa.

Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalumu ‘beacons’ ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi hili lifanyike haraka.

Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. “nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa,” Makamba aliongezea.

Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuripoti na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.

Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali wa dini na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani,na kuahidi kugharamia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo nakusisitiza agenda ya mazingira iwepo.

Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika



Monday, October 24, 2016


Jinsi ya Kuandaa na Kutayarisha Dawa Lishe ya Kunenepesha,Kurutubisha na Kuongeza Mwili

SeeBait

Dawa-lishe  ya  kuongeza, kurutubisha  na  kunenepesha  mwili, ni  dawa  maalumu  kwa  watu  wenye  uzito  wa  chini  (  Under weight ) ambao  wanataka  kuongeza  mwili  na  uzito.



Dawa  hii  huwasaidia  watu  ambao  miili  yao  imedhoofu  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali.

Na  kwa  wale  watu  wembamba  ambao  wanataka  kuongeza  miili  yao, dawa  hii  huwasaidia  vizuri  sana.

FAHAMU  JINSI NA  NAMNA  YA  KUANDAA NA  KUTAYARISHA   DAWA-LISHE  MAALUMU   YA  KUONGEZA, KURUTUBISHA  NA  KUNENEPESHA  MWILI.

MAHITAJI   YA  DAWA –LISHE

i.           Dawa –lishe vijiko  viwili vikubwa.

ii.         Asali  ya  tende  vijiko  vitano  vikubwa.

iii.       Tangawizi  ya  unga  vijiko  vikubwa  viwili

iv.       Unga  wa ufuta

v.         Maziwa  fresh nusu  lita

vi.       Maji  ya  moto  kiasi  cha  milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills  )


MATAYARISHO
i. Chukua  vijiko  vinne  vyenye  dawa  lishe  yako  kisha  chemsha  na  nusu  lita  ya  maji  hadi  mchanganyiko  wako  utokote  halafu  ipua, chuja , makapi  weka  pembeni  kisha  hifadhi  juisi  yako.

ii.Tayarisha  uji kwa  kutumia  unga  wa  ufuta  na maziwa  fresh

iii.Chukua  vijiko  viwili  vikubwa  vya tangawizi  ya  unga  kisha  changanya  kwenye  kikombe  cha  maji  ya  moto  chenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  hamsini  (  250  mills )

MATUMIZI:
i. Tumia  kunywa  nusu  lita  ya  dawa –lishe  yako  kisha

ii.Tumia kula  vijiko  vinne  vikubwa  vya  asali  ya  tende

iii.Kisha tumia  kunywa  vikombe  vinne  vya  uji  wa  ufuta  ulio changanywa  na  maziwa  fresh

iv.Halafu  kunywa  glasi  moja  ya  moto  iliyo  changanywa  na  vijiko  viwili  vikubwa vya tangawizi  ya  unga.

UTAFANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  MFULULIZO.

Baada  ya  siku  thelathini, utaangalia  na  kujitathmini  kiasi  ulicho  ongezeka. Kama  utataka  kuendelea  kuongezeka  zaidi, utaendelea  kutumia  dozi  hii  hadi hapo utakapo fikia kiwango  utakacho  rizika  nacho.

BEI  YA  DAWA-LISHE : Bei  ya  Dawa-Lishe  ni  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU (TSHS.50,000/=)

JINSI  YA  KUIPATA  DAWA  LISHE:
Dawa  hii  inapatikana  katiuka  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAN  katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  SHULE  YA  SEKONDARI  YA  MT. ANNUARITE.

Unaweza  kufika  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  AU  unaweza  kuletewa  mahali popote  ulipo  jijini  Dar   Es  salaam.

Kwa  wakaazi  wa  ZANZIBAR  watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti  na  kwa  wateja  wetu  wa  ughaibuni watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Kwa  mawasiliano  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu

0766  53  83   84

Vile  vile  tunayo  dawa  ya  asili  iitwayo  JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME  pamoja  na  jinsi  dwa  ya  JIKO  inavyo  fanya  kazi  tafadhali  tembelea:

Monday, October 24, 2016


CCM Wamdhibiti Maalim Seif Zanzibar....SMZ Yapiga Marufuku Siasa Nyumba za Ibada

SeeBait
Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar, imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibada kwa shughuli za kisiasa Visiwani Zanzibar.

Msimamo huo wa Serikali umekuja siku chache tangu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kutumia kila siku za Ijumaa kufikisha ujumbe katika msikiti atakaoswali.

Akitoa tamko la Serikali jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa yote ya Zanzibar kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika mikoa yao.

“Kwa taarifa hii Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa kupitia kamati zao za ulinzi na usalama kusimamia utekelezaji wa agizo hili katika mikoa yao,” alisema Waziri Aboud.

Alisema Serikali imewaagiza wakuu hao wa mikoa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Waziri Aboud alisema kwamba viongozi wa dini na kamati zao katika nyumba za ibada watakaoruhusu  wanasiasa kuendesha shughuli za kisiasa watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kwamba hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika Misikiti ya Mbuyuni, Kihibnani na Kwabiziredi kumetokea tabia  kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kupita na kutoa hotuba za kisiasa katika misikiti hiyo.

Waziri huyo alisema kwamba shughuli za vyama vya siasa zinaendeshwa chini ya sheria N0 5 ya mwaka 1992 ambayo imeeleza wazi mipaka na shughuli za kisiasa ziendeshwe chini ya sheria hiyo.

“Vitendo vinavyofanywa na viongozi hao  wa kisiasa wanaotumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa  wanakwenda kinyume na dhamira ya katiba na sheria za nchi ikiwemo sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992” Alisisitiza Waziri Aboud.

Waziri Aboud alisema kwamba shughuli zote za  dini ya kiislamu Zanzibar zinasimamiwa kupitia sheria namba 9 ya mwaka 2001, namba 2 ya mwaka 2007 na namba 3 ya mwaka 1985 zinazoongoza Taasisi mahsusi kama vile Ofisi ya Mufti, Ofisi ya Mahakama ya Kadhi na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.

Alisema  kupitia katiba na sheria , uhuru wa mtu kuabudu dini anayoitaka umetolewa bila kuingiliwa na itikadi za vyama vya siasa kama inavyobainishwa  na katiba zote mbili ibara ya 19 ambazo zinaeleza umuhimu wa uhuru wa mtu kuamini dini aitakayo kwa misingi ya kukuza usalama na amani katika jamii.

Monday, October 24, 2016


Sare za CCM zamshusha cheo Mwalimu Mkuu

SeeBait

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM kwenye mahafali ya kidato cha nne.

Pia, taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta michango yote mashuleni.

Otieno, ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.

Monday, October 24, 2016


Lipumba aitaka Chadema Kutoingilia Mgogoro CUF......Aifananisha Opareshi UKUTA na Biskuti

SeeBait

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba,  amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoingilia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sababu hauwahusu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika kikao cha ndani, kilichofanyika Wilaya ya Kinondoni ambapo alisema Chadema kushindwa kutekeleza Operesheni Ukuta ni dhahiri chama hicho kimeshindwa kutekeleza kile wanachoahidi kwa Watanzania.

Alisema mpaka sasa kumekua na vikao mbalimbali vinavyofanywa na viongozi wa Chadema kwa ajili ya kuivuruga CUF, jambo ambalo alisema haliwekezani.

“Chadema wanajitahidi kutuvuruga kwa kutuma waasi wa chama hiki, lakini naomba niwaambie hawawezi, CUF ni ngangari hata serikali inajua na  wanachokifanya ni kupoteza muda bure.

“Unajenga Ukuta wa biskuti, ukiumwagia juisi unamong’onyoka, Ukuta gani huo, huu muziki wa CUF ni ngangari hawauwezi,” alisema Lipumba.

Alisema katika kipindi hiki ambacho wana kesi mahakamani, wanachama wa chama hicho wataendelea na shughuli za kukijenga chama hicho pamoja na kuwasisitiza  kuwa na msimamo wa kutetea chama na katiba yake, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufikia malengo waliyokusudia ya kushika dola kafika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Alisema kutokana na hali hiyo, rasilimali za chama hicho zinasimamiwa kwa umakini chini ya walinzi wa chama hicho, Blue Guard ambao Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ni wavamizi hawatambui.

“Ninamshangaa Maalim Seif sasa hivi anaibuka na kusema hawatambui walinzi wa chama Blue Guard ambao miaka yote walikua wanamlinda pamoja na rasilimali za chama, lakini hayo yamekwisha nitazidi kumwomba aje tujenge chama hata kama kesi inaendelea mahakamani,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano anayemunga mkono Profesa Lipumba, Abdallah Kambaya alisema kupoteza nafasi ya umeya na naibu wake katika Manispaa ya Kinondoni ni matokeo ya mgogoro wa CUF na kutokuwepo ushirikiano ndani ya Ukawa.

“Maalim Seif anaunga mkono Ukawa, mbona wanachama wa Ukawa wameshindwa kutusaidia ili kupata meya na naibu wake kwenye uchaguzi wa leo? (jana),” alihoji.

Monday, October 24, 2016


Serikali kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo kwa kipaumbele

SeeBait

Serikali ipo katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya inatimia.


Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Serikali inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

“Serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”

Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 24, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...