Wednesday, October 5, 2016

Tundu Lissu akosekana Tena Mahakamani Kisutu, aibukia Mwanza

SeeBait
Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza.

Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.

Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Ibrahim alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi hiyo.

“Lissu ni wakili  pekee wa mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema Kibatala.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.

Katika kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa kufuatia kunukuliwa akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la MAWIO ikiwa na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.”

 

 

Wednesday, October 5, 2016

Sinema ya CUF Yazidi Kunoga.......Bodi ya Wadhamini Nayo Yagawanyika Viipandevipande

SeeBait
Bodi ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imegawanyika vipande viwili  kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Kugawanyika kwa bodi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wake, Abdallah Katau kutangaza kutomtambua Profesa Lipumba, huku baadhi ya wajumbe wakipinga tamko hilo wakiliita ni batili kwa mujibu wa katiba ya CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajumbe wenzake, mjumbe wa bodi ya chama hicho, Peter Malebo, alisema hawatambui tamko lililotolewa na mwenyekiti wao kwani bodi hiyo inajiandaa kuwakutanisha mwenyeki wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuweza kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Alisema kutokana na hali hiyo, watakaa na wajumbe wenzao na kujadili suala hilo kabla ya kuwaita viongozi hao ikiwa ni pamoja na kujadili ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

“Tutakaa na wajumbe wenzetu ili tuweze kujadiliana mgogoro wa viongozi wetu pamoja na kupitia maazimio ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili tuweze kupata hoja ya kuwahoji kwenye kikao hicho.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa chama chetu kinarudi kwenye hadhi yake kama ilivyokua awali kuliko hivi sasa ambapo kimegubikwa na mgogoro wa uongozi wa kitaifa,” alisema Malebo.

Alisema ikiwa watashindwa kupata mwafaka wataitisha Mkutano Mkuu wa dharura  ili waweze kuwaeleza wajumbe wa mkutano huo hali ya chama na hatua za kuchukua.

“Kama mwafaka hautapatikana katika kikao hicho, tutalazimika kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu ambao pamoja na mambo mengine, tutawaeleza mgogoro wa viongozi wetu ili wajumbe waweze kutoa uamuzi,” alisema.

Alisema Bodi ya Wadhamini wa CUF inaundwa na wajumbe wanane ambapo kutoka upande wa bara ni watano na Zanzibar watatu.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Abdalah Katau, Peter Malebo, Ally Mbarouk, Amin Mrisha, Zacharia Kwangu, Yohana Mbelwa na Dk. Juma Muchi.

Alisema mpaka sasa bodi hiyo imegawanyika ambapo wajumbe kutoka Zanzibar wanamwunga mkono Maalim Seif huku wale wa bara wakimwunga mkono Profesa Lipumba hali inayozidi kupandisha joto ndani ya chama hicho.

“Kinachotutafuna  ndani ya CUF ni ubaguzi unaoonyeshwa waziwazi kutoka kwa viongozi wa Zanzibar jambo ambalo limechangia kila mtu kuwa upande wake, lakini tutaitana na kujadiliana suala hili ili tuweze kupata mwafaka,” alisema.

Alisema bodi hiyo inafanya kazi ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo iliteuliwa mwaka 2011 na itamaliza muda wake, Desemba mwaka huu.

Atoa onyo Chadema
Katika hatua nyingine, Malebo aliwataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoingilia mgogoro huo kwa madai hauwahusu.

Alisema, kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Profesa Lipumba inaonyesha wazi kuwa ameshiriki kuongeza mgogoro ndani ya chama hicho.

“Mbowe haumhusu mgogoro wa viongozi wa CUF, huu ni mgogoro wa ndani ya chama, tunamshangaa kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Lipumba, yeye ni nani ndani ya chama?, tunamuonya asirudie,” alisema.

Alisema, chama hicho kimejipanga kupambana na watu wanaoingilia mgogoro wao wakati si wanachama wa chama hicho, jambo ambalo limechangia kuendelea kuchochea vurugu hizo.

 

 

Wednesday, October 5, 2016

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi atoa ONYO kwa wanaotumia jina la cheo chake vibaya

SeeBait

 

 

Wednesday, October 5, 2016

Saed Kubenea kizimbani tena kwa kupotosha

SeeBait

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kuandika makala ya kupotosha na kusababisha hofu kwa jamii.

Kubenea, ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili Mukabatunzi alidai kuwa Julai 25, mwaka huu katika Mtaa wa Kasaba, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kubenea alichapisha habari ya uongo inayoweza kusababisha hofu na taharuki kwa jamii au kuondoa amani.

Inadaiwa Kubenea alichapisha makala hiyo kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi 31, mwaka huu, lenye namba 349 ISSN: 1832-5432 ikiwa na kichwa cha habari “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar”.

Baada ya kusomewa mashitaka, Kubenea alikana kutenda kosa hilo na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.

 

 

 

Wednesday, October 5, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Octobar 5

SeeBait

 habari za kimataifaa.


Urusi imesema imetuma mfumo wa kuzuia makombora katika mji wa bandari wa Tartus nchini Syria. Hatua hiyo inakuja huku hali ya vuta nikuvute kati ya Urusi na Marekani ikipamba moto kuuhusu mzozo wa Syria. Tangazo hilo la Urusi linakuja baada ya Marekani kusema inasitisha mazungumzo na Urusi ya kuyafufua makubaliano ya kusitisha mapigano Syria kutokana na Urusi kuendelea kuunga mkono utawala wa Rais Bashar al Assad. Majeshi ya Syria yameendeleza mashambulizi makali yanayoulenga mji unaodhibitiwa na waasi wa Aleppo. Urusi imeshutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya angani yanayowalenga raia na hospitali katika mji huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema ana nia ya kuutafutia ufumbuzi wa kidiplomasia mzozo wa Syria lakini mazungumzo kati yake na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yamekwisha. Viongozi wa kiusalama na wa sera za kigeni wa Marekani wanakutana leo kujadili njia za kidiplomasia, kijeshi, kijasusi na kiuchumi kuihusu Syria.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos atakutana na mpinzani wake mkuu Alvaro Uribe leo kujadili namna ya kuyaokoa makubaliano ya amani kati ya serikali na waasi wa FARC baada ya wapiga kura kuyakataa makubaliano hayo katika kura ya maoni iliyofanyika siku ya Jumapili iliyopita. Mkutano huo kati ya Santos na Uribe unakuja baada ya chama cha mrengo wa kulia Democratic Center kuyasusia mazungumzo ya dharura ya viongozi wa kisiasa yaliyoitishwa na Rais huyo wa Colombia siku ya Jumatatu kutafuta njia ya kuisogesha mbele nchi hiyo baada ya kura hiyo ya maoni ambayo inayaweka hatarini makubaliano kati ya serikali na waasi wa FARC ya kumaliza mzozo wa zaidi ya miongo mitano. Rais Santos amesema makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali na FARC yanakamilika tarehe 31 mwezi huu. Mzozo huo wa Colombia umesababisha vifo vya zaidi ya watu 260,000 na watu wengine 45,000 hawajulikani waliko.

 

Vyama vikuu vya upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimeitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti zaidi za kuhakikisha kunakuwepo mdahalo unaozijumuisha kila pande nchini humo kuhusu chaguzi zijazo ambazo zimesababisha hali ya taharuki katika taifa hilo. Kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani Congo Etienne Tshisekedi amewataka wafuasi wake kuandamana tarehe 19 mwezi huu iwapo hakutakuwa na hatua za tija zilizochukuliwa kuhusu uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao lakini sasa umeahirishwa. Upinzani umetaka tume ya uchaguzi na mahakama ya kikatiba kufanyiwa mageuzi ukidai asasi hizo mbili zinaegemea upande wa Rais Joseph Kabila anayeshutumiwa kuchelewesha chaguzi ili kusalia madarakani. Hapo jana, Rais Kabila alisema chaguzi zitaahirishwa ili kuhakikisha taifa hilo linajiandaa vyema kuendesha chaguzi hizo. Tume ya uchaguzi ya Congo ilisema huenda chaguzi zikafanyika mwezi Desemba 2018.

 

Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamefutilia mbali mashitaka ya uhalifu dhidi ya mchekeshaji wa Ujerumani Jan Boehmermann aliyeghani shairi liliochukulika kumtusi Rais wa Uturuki Recep Erdogan. Mkurugenzi mkuu wa kituo cha televisheni cha Ujerumani ZDF Thomas Bellut amesema kuondolewa kwa mashitaka hayo ya kumtusi kiongozi wa nchi ni habari njema kwa uhuru wa kujieleza wa Ujerumani. Boehmermann alighani shairi hilo lililozua mzozo wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Ujerumani mnamo tarehe 31 mwezi Machi. Wakili wa mwandishi huyo wa tungo za mzaha amesema waendesha mashitaka wamestahimili shinikizo kali la kisiasa na uamuzi wao unastahili heshima. Licha ya mahakama kumuondolea mashitaka ya uhalifu Böhmermann, uamuzi kamili kuhusu kesi ambapo Rais Erdogan anataka kupigwa marufuku kwa shairi hilo lililozua utata unatarajiwa kutolewa na mahakama ya Hamburg.

 

Wabunge wa Umoja wa Ulaya waeidhinisha makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi yaliyofikiwa Paris, Ufaransa mwaka jana ambayo yataanza kutekelezwa rasmi mapema mwezi ujao. Hatua hiyo inauweka Umoja wa Ulaya katika njia ya kuukabidhi Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa idhini yake, hali ambayo itaiweka jumuiya ya kimataifa katika hatua inayohitajika ya utekelezaji. Makubaliano ya Paris yanazitaka nchi zote kuweka mipango kufikia lengo la kuzuwia joto kupanda hadi nyuzi joto mbili za Celsius juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda na kupambana kubakia katika kiwango cha nyuzi joto 1.5 Celsius ikiwa itawezekana. Makubaliano hayo ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira yanahitaji kuungwa mkono na angalau nchi 55 ili kuidhinishwa rasmi na Umoja wa Ulaya.

 

Kimbunga kwa jina Mathew, kinachotajwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kuzikumba nchi za Caribbean katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kimeikumba Haiti na Cuba. Kimbunga hicho kinachosafiri kwa upepo mkali wa kilomita 230 kwa saa kimesabisha maelfu ya watu kutafuta hifadhi salama kuepuka maafa. Umoja wa Mataifa umekitaja kimbunga Mathew kuwa mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu kuikumba Haiti tangu tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha janga la kibinadamu nchini humo mwaka 2010. Katika taifa jirani na Haiti, Jamhuri ya Dominican, watu wanne wameuwa na athari za kimbunga hicho kilichosababisha mvua kubwa. Taarifa za awali zinasema Cuba haijaathirika sana na kimbunga hicho ikilinganishwa na Haiti. Kimbunga Mathew kinatarajiwa kuendelea kuwa na nguvu kikielekea katika majimbo kadhaa ya Marekani. Gavana wa jimbo la South Carolina ameagiza zaidi ya watu milioni moja kuhamishiwa maeneo salama.

 katika michezoooo


RASHFORD ATAKUWA SUPASTAA!


RASHFORD-ROONEYKEPTENI wa Manchester United na England Wayne Rooney ameeleza kuwa Chipukizi Marcus Rashford atapanda chati na kuwa Supastaa mwenye Jina kubwa kwenye Soka.
Rashford, mwenye Miaka 18, ameibuka na kupanda juu haraka mno baada ya Meneja aliepita wa Man United Louis van Gaal kumpa nafasi kucheza kwa mara ya kwanza Timu ya Kwanza kwenye UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Midtjylland Mwezi Februari.
Kwenye Gemu hiyo Kijana huyo akapiga Bao 2 na Siku 3 baadae, kwenye Mechi yake ya kwanza ya EPL, Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal akapiga tena Bao 2.
Tangu wakati huo Rashford amekuwa ni moto kwenye Mechi zote anazochezeshwa.
Ingawa Rooney amekiri bado Staa huyo hajakomaa lakini amebainisha uwezo na kipaji chake kitamfikisha mbali.
Rooney ameeleza: "Marcus anafanya vizuri. Ni Kijana mdogo mwenye mvuto mkubwa Duniani hivi sasa. Nina hakika akiendelea kufanya bidii na kukua basi atakuwa Supastaa Miaka ijayo!"
Radhford alikuwemo kwenye Kikosi cha England kilichokuwa Fainali za EURO 2016 huko France Juni na Julai chini ya Kocha Roy Hodgson lakini alipokuja Sam Allardyce na kuisimamia England Mechi 1 tu hakuitwa.
Badala yake Rashford akachukuliwa England U-21, chini ya Gareth Southgate, na yeye kupiga Hetitriki kwenye ushindi dhidi ya Norway.
Radhford sasa amerejeshwa tena England ambayo sasa ipo chini ya Meneja wa muda Gareth Southgate na Jumamosi itacheza na Malta kwenye Mechi ya Kundi lao la Nchi za Ulaya zinazosaka kwenda Russia Mwaks 2018 kucheza Fainali za Kombe la Dunia huku Rashford akitabiriwa sana kuanza Mechi hiyo.
Hivi sasa Rashford pia yumo Kikosi cha Kwanza cha Man United chini ya Meneja Jose Mourinho na kumfanya Rooney asugue Benchi.
Rooney amenena: "Ni muhimu Wachezaji chipukizi wanaofurahisha wazawadiwe wakistahili na nadhani anastahili!

 

KOMBE LA DUNIA 2018: BONUCCI AWANIA KUIBONDA TENA SPAIN KAMA WALIVYOITENDA KWENYE EURO 2016!


ITALY-SPAINALHAMISI Italy watapambana na Spain kwenye Mechi ya Pili ya Kundi G la Nchi za Ulaya kuwania nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia na Leonardo Bonucci anataka Italy waibonde tena Spain kama ilivyokuwa Mwezi Julai kwenye EURO 2026.
Bonucci, Sentahafu anaechezea Juventus, amesema wao wanataka waifunge Spain kama walivyoitoa  kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 walipoichapa 2-0.
Wakati huo Spain walikuwa ndio Mabingwa Watetezi wa Ulaya.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 wa Makundi watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia
++++++++++++++++++++++++
Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi hii itakayochezwa Alhamisi huko Juventus Stadium Mjini Turin Nchini Italy, Bonucci amesema: "Nkifikiria Paris, nafurahia sana. Kumbukumbu hiyo inatupa morali kwani tuliwabwaga Vigogo Duniani ingawa wakati huo hawakuwa imara sana!"
Hata hivyo, Bonucci amekiri Mechi hii ya sasa ni tofauti kwani kila Timu sasa ina Kocha Mpya.
Italy sasa wapo chini ya Giampiero Ventura baada kuondoka Antonio Conte na Spain wako chini ya Julen Lepetegui baada ya kung'oka Vicente del Bosque.
Kwenye Mechi zao za kwanza za Kundi G Spain, ikiwa Nyumbani, iliibomoa Liechtenstein 8-0 na Italy, wakiwa Ugenini waliipiga Israel 3-1.
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Alhamisi Oktoba 6
KUNDI D
Austria v Wales                
Moldova v Serbia             
Republic of Ireland v Georgia               
KUNDI G
2145 Italy v Spain            
Liechtenstein v Albania               
Macedonia v Israel           
KUNDI I
Iceland v Finland             
Kosovo v Croatia             
Turkey v Ukraine             
Ijumaa Oktoba 7
KUNDI A
France v Bulgaria             
Luxembourg v Sweden               
Netherlands v Belarus                
KUNDI B
Hungary v Switzerland               
Latvia v Faroe Islands                
Portugal v Andorra           
KUNDI H
Belgium v Bosnia-Herzegovina              
Estonia v Gibraltar           
Greece v Cyprus              
Jumamosi Oktoba 8
KUNDI C
1900 Azerbaijan v Norway          
Germany v Czech Republic          
Northern Ireland v San Marino              
KUNDI E
1900 Armenia v Romania            
1900 Montenegro v Kazakhstan            
Poland v Denmark            
KUNDI F
1900 England v Malta                
Scotland v Lithuania         
Slovenia v Slovakia          
Jumapili Oktoba 9
KUNDI D
1900 Wales v Georgia                
Moldova v Republic of Ireland               
Serbia v Austria               
KUNDI G
1900 Israel v Liechtenstein         
Albania v Spain                
Macedonia v Italy            
KUNDI I
1900 Finland v Croatia               
1900 Ukraine v Kosovo              
Iceland v Turkey              
Jumatatu Oktoba 10
KUNDI A
Belarus v Luxembourg                
Netherlands v France                 
Sweden v Bulgaria            
KUNDI B
Andorra v Switzerland              
Faroe Islands v Portugal             
Latvia v Hungary              
KUNDI H
Bosnia-Herzegovina v Cyprus                
Estonia v Greece              
Gibraltar v Belgium           
Jumanne Oktoba 11
KUNDI C
Czech Republic v Azerbaijan                 
Germany v Northern Ireland                 
Norway v San Marino                 
KUNDI E
1900 Kazakhstan v Romania                 
Denmark v Montenegro              
Poland v Armenia             
KUNDI F
Lithuania v Malta             
Slovakia v Scotland          
Slovenia v England

 



Simba imepigwa faini ya Sh milioni 5 kutokana na mashabiki wake kung’oa viti vya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati timu yao ikicheza na Yanga ikiwa ni baada ya mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kufunga, lakini kabla alikuwa ameshika mpira.

Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imefikia uamuzi wa kuipa Simba adhabu hiyo.

Kama hiyo haitoshi, kamati hiyo imeionya Simba kwa kusisitiza ni onyo kali na kama itatokea tena itatoa adhabu kali.

Moja ya adhabu ambazo zimetajwa ni pamoja na Simba kucheza bila ya mashabiki.


Msisitizo wa kamati hiyo, umesema adhabu hiyo imetolewa kutoka kwa mujibu wa kanuni ya 42(3) na 24(7) za Ligi Kuu Bara.

 

STAND UNITED
Vikosi vya Mbeya City na Stand United vimechimbana mkwara mzito kila upande ukitamba kuibuka na ushindi katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii huko mkoani Mbeya.

Timu hizo zinakutana zikiwa na jeuri ya kuibuka na ushindi katika michezo yao ya mwisho ya ligi msimu huu, ambapo City iliifunga Mwadui kwa bao 1-0 na kukamata nafasi ya saba ikiwa na pointi 11, Stand ikaitungua Majimaji mabao 2-0 na kufikisha pointi 15, ikiwa nafasi ya pili, nyuma ya kinara Simba mwenye 17.

Ofisa Habari wa Stand, Deo Makomba, ameeleza kuwa hawana wasiwasi na mwendo walionao sasa, wamepania kumfunga kila watakayekutana naye ingawa wanajua Mbeya City ni timu ngumu lakini wataichapa hukohuko kwao.

“Cha msingi waamuzi wawe ‘fair’ tu na watende haki lakini kuhusu kikosi chetu tunakiamini na benchi la ufundi lipo vizuri, mchezo hautakuwa mwepesi lakini tumepanga kushinda katika kila mchezo ulio mbele yetu, maana nia yetu ni kuhakikisha tunamaliza katika nafasi tatu za juu msimu huu,” alisema Makomba.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa City, Dismas Ten, alisema: “Tunachokitaka siku zote ni ushindi na ukizingatia tupo nyumbani, kwa hiyo tumejizatiti ingawa mpira ni dakika 90, hizo zitaamua nani mshindi baada ya mchezo. Timu itaanza maandalizi (jana) leo jioni tayari kwa ajili ya mchezo huo.”

 

TFF ‘YAJIBARAGUZA’ ETI HAIJAMFUNGIA SAANYA, INAMCHUNGUZA TU…LAKINI YAKUBALI KUFUTA KADI YA MKUDE


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekerwa na kuvuja kwa taarifa ya Kamati ya Saa 72 kilichoketi jana na kuwafungia waamuzi wawili wa mechi ya watani, Simba na Yanga. Na katika kile kinachoonekana ‘kujibaraguza’, Kamati hiyo imetoa taarifa eti haiwajafungia Martin Saanya na Samuel Mpenzu, badala yake inawachunguza. Lakini taarifa za uhakika kutoka kwenye kikao cha Kamati jana usiku zilisema, Saanya na Mpenzu kila mmoja amefungiwa miaka miwili.
Taarifa rasmi ya Kamati iliyotolewa leo imesema kwamba waamuzi hao pamoja na Ferdinand Chacha sasa wanachunguzwa kwa uchezeshaji wao, lakini Simba SC imetozwa faini ya Sh. 5,000,000  na kutakiwa kufidia gharama za uharibu waliofanya Jumamosi.   Mashabiki wa Simba walifanya vurugu Uwanja wa Taifa Jumamosi baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban. Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele. Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya. Na Mpenzu naye anadaiwa kukataa bao safi la Simba lililofungwa na Ibrahim Hajib mapema kipindi cha kwanza akidai aliotea. Taarifa pia imesema Kamati hiyo imefuta adhabu ya kadi nyekundu ya Mkude, baada ya kubaini hakuwa na hatia, wakati Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara ametozwa faini ya Sh. 200, 000 kwa kuingia uwanjani baada ya mechi. Katika hatua nyingine, klabu ya Azam FC imetozwa faini ya Sh. 3,000,000 kwa kosa la kuvaa nembo ya mdhamini (Vodacom) upande mmoja badala ya pande zote mbili. 


 

Tuesday, October 4, 2016

Waziri Mkuu Alaani Mauaji Ya Watafiti Chamwino, Dodoma

SeeBait
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji kuwaua watumishi wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali.

Mauaji ya watafiti hao, Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema Serikali imesikitishwa na mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo mkoani Arusha ambao walikuwa kazini kuchunguza sampuli za udongo ili kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.

“Kutokana na tetemeko lilitokea mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha watalaamu mbalimbali kufanya uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni endelevu au la katika maeneo mengine. Kitendo cha watu kujichukulia hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi ambao walikuwa kazini hakikubaliki,” amesema

. Amesema watalaamu hao walifika katika Wilaya ya Chamwino na kufanya kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo walipoenda eneo la kijiji cha Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa wakiwa kazini.

“Serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho’’ amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewatoa wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama na kila anayekuja yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila anayehamia hapa atakuwa salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa salama,’’ amesema.

Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, Waziri Mkuu amesema hali hiyo inajitokeza hivi sasa baada ya wananchi wengi kutambua thamani ya ardhi.

Amesema miaka ya nyuma watu wachache walitambua thamani ardhi hivyo kuchukua maeneo makubwa na kuyamiliki. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa migogoro hiyo inamalizika kwa kuweka kuweka msisitizo kuwe mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima ardhi yote na kutoa hati kwa wananchi.

“Tunataka ardhi yote ipimwe na kila mtu anayepewa ardhi apewe hati ya kumiliki na si vinginevyo’’ amesema. Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwaasa waandishi wa habari wawe makini na kazi yao na wajiepushe na upotoshaji kwenye taarifa wanazozitoa kwa wananchi. Amesema vyombo vya habari ni kiungo muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo aliwataka viongozi wote wa umma washirikiane na vyombo vya habari kwa kutoa habari za utekelezaji wa kazi za Serikali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea msaada wa sh. milioni 11.42 kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali mkoani Dodoma zikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.

Michango aliyopokea leo imetolewa na Mzee Thakar Singh na familia yake sh. milioni 5; NSSF Dodoma (sh. milioni 1.2); Shirika la Bima ya Taifa tawi la Dodoma (sh. milioni moja); Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (sh. milioni moja) na Ofisi Rais TAMISEMI (sh. milioni 2). Wengine ni TRA-Dodoma (sh. milioni moja); Dodoma FM (sh. 200,000) na Mwalimu Mstaafu, Mama Amina Mafuru aliyetoa sh. 20,000/-.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA. JUMANNE, OKTOBA 04, 2016

 

 

 

Tuesday, October 4, 2016

Taarifa Kwa Wataalamu Wa Afya Wanaotarajia Kuanza Mafunzo Kwa Vintendo (Internship).

SeeBait
Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 05, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...