Saturday, October 22, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Octoba 22

SeeBait

Friday, October 21, 2016

Rais Magufuli Aweka Jiwe La Msingi Mradi Wa Hosteli Za Wanafunzi Katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam

SeeBait
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Oktoba, 2016 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho.

Wakati Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi Rais Magufuli aliyeambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameipongeza TBA na wadau wote wanaoshiriki katika ujenzi huo zikiwemo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa hatua kubwa ya ujenzi iliyofikiwa tangu ujenzi uanze tarehe 01 Julai, 2016 na amebainisha kuwa kwa kutumia TBA mradi huo utatumia kiasi kidogo cha fedha.

"Nawapongeza sana TBA kwa kazi nzuri mliyoifanya mpaka sasa, mradi huu utatumia Shilingi Bilioni 10 tu, Wakandarasi kutoka nje walitaka kujenga mabweni haya ya wanafunzi kwa Shilingi Bilioni 100, sasa mtaona wenyewe tumeokoa Shilingi ngapi" amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ameahidi kuwa, kwa kuwa majengo hayo yanauwezo wa kubeba ghorofa sita, Serikali itafanya utaratibu wa kutumia moja ya likizo za wanafunzi kuongeza ghorofa nyingine mbili ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata nafasi.

Kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Dkt. Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu ambapo wanafunzi takribani 93,000 wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 watakaoanza masomo watapatiwa mikopo lakini ameweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.

"Na ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.

"Kwa sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa" amesisitiza Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala amesema wakati ujenzi huo ukiendelea chuo kimetenga Shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwenye mapato yake kwa ajili ya kununua samani ikiwa ni pamoja na vitanda vya wanafunzi na pia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashughulikia ujenzi wa uzio, jiko na bwalo la chakula.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Wabunge, Makatibu Wakuu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Oktoba, 2016
 
 

Friday, October 21, 2016

Rais Magufuli aagiza HESLB kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni.

SeeBait
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  kwa gharama ya shilingi bilioni 10.

Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.

“Serikali inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga watoto maskini.

Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.

Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.

Naye Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako  alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Desemba 2016.

Katika hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.

Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.
 
 

Friday, October 21, 2016

Alichosema Rais Magufuli kuhusu mikopo ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu

SeeBait
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi zaidi ya 118,000 watanufaika.

Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo, Rais Magufuli amesema miongoni mwa hao watakaonufaika, wanafunzi 93,000 ni wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 ni watakaoanza masomo mwaka huu huku akiweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.

"Na ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.

"Kwa sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa" amesisitiza Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.
 
HABARI ZA KIMATAIFAAAA
 

Habari | 22.10.2016 | 06:03

Watu 55 wamefariki dunia na wengine takriban 600 wamejeruhiwa baada ya treni iliyokuwa imejaa watu imeanguka nchini Cameroon hapo jana ilipokuwa ikisafiri kutoka mji mkuu Yaounde kuelekea mjini Douala. Waziri wa uchukuzi wa Cameroon Edgar Alain Mebe Ngo'oo amesema mabehewa kadhaa ya treni hiyo iliyokuwa imejaa watu yaling'oka kutoka njia ya reli muda mfupi kabla ya kufika katika mji wa Eseka. Watu wengi walilazimika kutumia usafiri wa treni hiyo kuelekea Douala baada ya mvua kubwa iliyonyesha usiku wa Alhamisi kusomba daraja muhimu na kukatiza usafiri wa magari. Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika lakini duru zinaarifu kuwa mabehewa zaidi yaliongezwa kwenye treni hiyo ili kubeba abiria zaidi. Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.


Uchunguzi wa kimataifa umegundua kuwa majeshi ya serikali ya Syria ndiyo yaliyohusika katika shambulizi la tatu la silaha za sumu. Hayo ni kulingana na ripoti ya nne ya faragha iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana baada ya uchunguzi uliodumu kwa miezi 13.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na wa shirika linalodhibiti na kupiga marufuku silaha za sumu OPCW wanavilaumu vikosi vya jeshi la Syria kwa kutumia gesi ya sumu katika mji wa Qmenas katika jimbo la Idlib mnano mwezi Machi mwaka jana. Jeshi hilo pia linashutumiwa kwa kutumia sumu katika miji ya Talmenes na Sarmin katika nyakati tofauti. Wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS pia wanashutumiwa kwa kutumia gesi aina ya mustard katika vita vinavyoendelea Syria.


Jumuiya ya kujihami ya NATO imemteua Arndt Freytag von Loringhoven aliyekuwa naibu wa mkuu wa shirika la ujasusi la Ujerumani kuwa mkuu wa kwanza wa ujasusi wa NATO. Freytag von Loringhoven atakiongoza kikosi kilichopewa jukumu la kuratibu shughuli za kijasusi za nchi wanachama wa NATO ili kufuatilia kwa karibu shughuli za kijeshi za Urusi na kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi. Freytag von Loringhoven mwenye umri wa miaka 59 hivi sasa ni balozi wa Ujerumani katika Jamhuri ya Czech na anatarajiwa kuacha wadhifa huo mwishoni mwa mwaka huu. 


Chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kimekatalia mbali makubaliano yaliyotiwa saini Jumanne wiki hii ambayo yatamruhusu Rais Joseph Kabila kusalia madarakani hadi 2018 kwa kuahirishwa chaguzi kuu zilizokuwa zifanyike mwezi ujao hadi mwezi April 2018. Chama cha UDPS kikiongozwa na Etienne Tshisekedi kimesema kinakataa vikali mpango huo ambao kimeutaja kuwa ni ukiukaji mkubwa wa katiba.Siku ya Jumanne, viongozi wa makundi yaliyokuwa yakishiriki mdahalo wa kitaifa walitia saini makubaliano ya kurasa 24 mjini Kinshasa yanayomruhusu Rais Kabila kusalia madarakani wakati ambapo chaguzi zimeahirishwa. Kanisa Katoliki Congo limesema makubaliano yoyote kuhusu uchaguzi wa rais sharti yaeleze bayana kuwa Kabila hatagombea muhula wa tatu madarakani. Kiongozi huyo alipaswa kuachia madaraka mwezi Desemba mwaka huu baada ya mihula miwili madarakani kuambatana na katiba ya nchi hiyo. 


Uchunguzi mpya wa maoni umeonya kuwa asilimia hamsini ya Warepublican nchini Marekani watakubali ushindi wa mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton huku asilimia 70 ya wapiga kura wa Republican wakisema iwapo atashinda uchaguzi wa urais itakuwa ni kutokana na wizi wa kura.Asilimia 70 ya wapiga kura wa Democrats wamesema watakubali ushindi wa mgombea urais wa Republican Donald Trump. Uchunguzi huo wa maoni uliotolewa jana na shirika la habari la Reuters na shirika linaloendesha uchunguzi wa maoni la Ipsos ni kufuatia madai ya mara kwa mara ya Trump kuwa vyombo vya habari na mfumo wa uchaguzi nchini Marekani vina njama ya kufanya udanganyifu wa kura ili kumwangusha.Trump amesema atakubali matokeo ya uchaguzi iwapo tu ataibuka mshindi. Kwa upande wake Bi Clinton amesema atakubali matokeo jinsi yatakavyokuwa. Uchaguzi mkuu unatarajiwa tarehe 8 Novemba.


Sudan imeyahimiza mataifa zaidi ya Afrika yaliyo wanachama wa mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ICC kujiondoa kutoka mahakama hiyo ikisisitiza kuwa ICC ni chombo cha kikoloni kinachowaandama tu viongozi wa Kiafrika.Hapo jana Afrika Kusini ilitangaza inajiondoa kutoka ICC baada ya kushutumiwa vikali mwaka jana kwa kutomkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir anayetafutwa na ICC kujibu mashitaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur. Uamuzi huo wa Afrika Kusini unafuatia ule wa Burundi ambayo pia imetangaza rasmi inajiondoa kutoka ICC.Burundi pia imeisifu Afrika Kusini kwa uamuzi wake na kuongeza inatarajia nchi zaidi kujiondoa. Marekani imesema inatiwa wasiwasi na uamuzi huo wa Afrika Kusini wa kutaka kujiondoa ICC. Kenya na Namibia pia zimeelezea nia ya kutaka kujiondoa kama wanachama wa mkataba wa Roma. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani uamuzi huo. Kati ya kesi 10 zilizochunguzwa na ICC tangu 2002, tisa ni dhidi ya mataifa ya Afrika. 


Askari nchini Ufaransa wamefanya mgomo katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris wakidai hawana silaha za kutosha hata za kujihami na kiasi cha askari 3,000 waliandamana usiku wa Alhamisi. Mamia ya polisi hao waliandamana pia hapo jana usiku karibu na makao makuu ya polisi ya Paris, mijini Calais, Lille, Toulon na miji mingine.Akizungumza mjini Brussels baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema atakutana na wawakilishi wa askari hao ofisini mwake mapema wiki ijayo kusikia malalamiko yao. Kilichochochea maandamano hayo ni tukio lililotokea katika mji mmoja ulio karibu na Paris mapema mwezi huu ambapo genge la wahalifu waliwashambulia askari wanne kwa bomu la kutengezwa na petroli walipokuwa wakishika doria. 

HABRI ZA KIMICHEZOOO .
 

Na katika michezo, Hamburg SV ilicharazwa mabao 3-0 na Eintracht Frankfurt katika mechi ya kandanda la ligi kuu ya hapa Ujerumani Bundesliga iliyosakatwa jana usiku. Hamburg ilijipata pabaya baada ya mchezaji wake Lewis Holtby kujifunga na kuipa Eintracht Frankfurt bao la kwanza katika dakika ya 35. Kisha katika kipindi cha pili Shani Tarashaj na Haris Seferovic wakahakikisha kuwa pointi tatu zinaelekea Frankfurt.Hamburg haijashinda mechi yoyote msimu huu na mashabiki waliwazomea kwa kuonyesha mchezo dhaifu hapo jana. Katika mechi ya leo kati ya Bayern Munich na Borussia Moenchengladbach, Mshambuliaji wa Bayern Frank Ribberry ndiye mchezaji pekee atakayekosa kucheza kutokana na maumivu ya misuli. 


NEYMAR ASAINI MKATABA MPYA BARCELONA, KUBAKI HADI 2021


BARCA-NEYMAR-NEW-CONTRACTMWEZI JULAI, FC Barcelona ilitangaza kuwa Neymar amekubali Dili mpya ya Miaka Mitano na Jana Mabingwa hao wa Spain wamethibitisha kuwa ameshaini.
Jana Klabu ya Barcelona iliposti kwenye Mtandao wa Twitter Picha ya Mbrazil huyo na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, wakipeana mikono kuthibitisha Dili imekamilika.
Neymar, akiongea na Barça TV, alisema anasikia furaha kubwa kwa kusaini Mkataba mpya kwani anajisikia yuko Nyumbani.
Alisema: “Kabla sijaja Barcelona nilijua ni Klabu kubwa na ina Wachezaji wazuri sana na hilo lilinipa wasiwasi. Lakini nilipofika tu nikagundua ni Watu wema na hilo lilinigusa moyoni na kunisaidia kujisikia Nyumbani!”
++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
- Neymar amefunga Mabao 91 katika Mechi 150 tangu 2013.
++++++++++++++++++++++
Mwezi Julai Barca ilithibitisha kuwa kwenye Mkataba huu Mpya na Neymar, ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua katika Mwaka wa Kwanza wa Mkataba huo basi itapaswa kulipa Euro Milioni 200, Mwaka wa Pili wa Mkataba Dau ni Euro Milioni 222 na kwa Miaka Mitatu iliyobaki kwenye Mkataba Dau litakuwa Euro Milioni 250.
Neymar alijiunga na Barca kutoka Santos ya Brazil Mwaka 2013 kwa Mkataba wa Miaka Mitano na kuweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Copa del Rey mara 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI 1.



CHELSEA v MAN UNITED: MOURINHO KUREJEA STAMFORD BRIDGE!


>CONTE: ‘APOKEWE VYEMA, AMEANDIKA STORI YA KLABU HII!’
>MOU: ‘TUKIFUNGA SITASHANGILIA KAMA MTOTO MWEHU!’
CHE-MAN-CONTE-MOUJUMAPILI, Stamford Bridge Jijini London itakuwepo Mechi ya EPL, Ligi Kuu England kati ya Wenyeji Chelsea na Manchester United na, mbali ya kuwa ni Mechi ya Timu zinazovutana na kuleta msisimko kila Msimu, safari hii mvuto mkubwa ni kurejea kwa mara ya kwanza Uwanjani hapo kwa Jose Mourinho.
Jose Mourinho alikuwa Meneja wa Chelsea kwa vipindi viwili tofauti na kutimuliwa Desemba 2015 na kisha, kabla Msimu huu kuanza, kujiunga na Man United.
Hivi sasa Chelsea ipo chini ya Meneja Mpya kutoka Italy, Antonio Conte, ambae nae alishika hatamu kabla Msimu huu kuanza.
Akiongea kuhusu Mechi yao ya Jumapili, Conte, amewataka Wadau wa Stamford Bridge kumpokea vizuri Jose Mourinho.
Conte ameeleza: “Namuheshimu sana. Alitwaa Ubingwa mara 3 hapa na ni Mtu muhimu kwa Klabu hii. Anastahili kupokewa vyema kwa sababu aliandika Stori ya Klabu hii, sehemu ya Historia ya Klabu hii!”EPL-OKT17
Kwa Mourinho, hii itakuwa mara ya pili kwake kutua Stamford Bridge kama Meneja wa Timu pinzani baada ya Mwaka 2010 kutua na Inter Milan na kushinda.
++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-MOURINHO alikaa Chelsea kwa Vipindi Viwili kama Meneja, Miaka ya 2004-2007 na 2013-2015.
++++++++++++++++++++++
Mwenyewe Jose Mourinho amesema ‘hatashangilia kama Mtoto mwehu’ ikiwa Timu yake itafunga bao dhidi ya Chelsea.
Pia Mourinho amesema hatafanya lolote ikiwa Mashabiki Uwanjani watampokea kwa kumpinga.
Mbali ya mvuto huu wa Mourinho, Mechi hii ni muhimu mno kwa Klabu zote mbili ambapo, baada ya Mechi 8, Chelsea wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 16 na Man United wapo Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 14.
Vinara wa EPL ni Man City, ambao wamefungana na Arsenal, na wana Pointi 19 na hivyo ushindi kwa Chelsea au Man United ni muhimu mno ikiwa watataka kutotupwa mbali toka mbio za Ubingwa hasa kwa vile Msimu uliopita Klabu zote 2 hazikuwemo 4 Bora.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 22
1430 Bournemouth v Tottenham           
1700 Arsenal v Middlesbrough              
1700 Burnley v Everton              
1700 Hull v Stoke            
1700 Leicester v Crystal Palace             
1700 Swansea v Watford            
1700 West Ham v Sunderland               
1930 Liverpool v West Brom                 
Jumapili Oktoba 23
1530 Man City v Southampton    
1800 Chelsea v Man United   
 
 

RIPOTI SPESHO

YANGA: KUELEKEA MKUTANO MKUU WA DHARURA KUIBARIKI ‘YANGA YETU’, MWENYEKITI MANJI ANENA MZEE AKILIMALI ‘AMENG’ATUKA’ UANACHAMA!


YANGA-HQ-MANJI-1MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, ameeleza kuwa Wapinzani wote wa mchakato wa Yanga kukodishwa kwa Kampuni ya Yanga Yetu Limited kwa Miaka 10 wanakaribishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Dharura utakaofanyika Jumapili Oktoba 23 Uwanja wa Kaunda, Makao Makuu ya Yanga, Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Wanahabari hapo Jana kwenye Makao Makuu ya Yanga, Mtaa wa Twiga na Jangwani Jijini Dar es Salaam, Manji amemwelezea Mpinzani Mkuu wa azma ya Yanga kukodishwa, Mzee Ibrahim Akilimali, kuwa ashapoteza haki ya kuwa Mwanachama wa Yanga kwa vile alikuwa hajalipia Ada ya Uanachama kwa Miezi 6 iliyopita.
Manji amemshauri Mzee Akilimali akitaka kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jumapili basi atapaswa kurudi kwenye Tawi lake kuomba upya Uanachama.
Vile vile, Mwenyekiti Manji amewakaribisha Wapinzani wote wa Yanga kukodishwa wahudhurie Mkutano Mkuu na kutoa michango yao wakihakikishiwa ulinzi badala ya kupayuka kwenye Vyombo vya Habari.
Manji pia alidokeza mipango yake ya maendeleo kwa Yanga na kudokeza kuwa Uwanja wa Gezaulole huko Kigamboni utakuwa ni wa Mazoezi na Gym wakati Uwanja wa Kisasa wa kuchezea Mechi utajengwa hapo hapo Jangwani kwenye Makao Makuu ya Yanga.
WAKATI HUO HUO, Mdau mmoja mkubwa wa Yanga amedai kuwa wanaopinga Mabadiliko ndani ya Yanga ni ‘Wapumbavu na Malofa tu’ ambao ni wanyonyaji wa Yanga badala ya wao kuisaidia Yanga kukua na kujitegemea.
Mdau huyo amedai zama za Klabu kubwa kutegemea kuzungushwa Kofia kwa Wanachama na Wadhamini ili kujiendesha zimepitwa na wakati na sasa Watu wajipange upya kuendesha Klabu kisasa, kitaaluma na kibiashara kwa ufanisi mkubwa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
AJENDA ZA MKUTANO MKUU WA DHARURA, Oktoba 23:
1. SALA NA UTAMBULISHO WA WAGENI WAALIKWA:
1.1. Sala ya Wakristo ya Kubariki Kikao.
1.2. Sala ya Waislamu ya Kubariki Kikao.
1.3. Utambulisho wa wageni waalikwa waliohudhuria, pia wenye udhuru – Waziri wa Michezo na Sanaa; Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dar-Es-Salaam (DRFA) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
2. KUFUNGUA KIKAO
3. KUPITIA DONDOO ZA KIKAO KILICHOPITA CHA MKUTANO WA WANACHAMA NA KUIDHINISHA.
4. KUTHIBITISHA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI NA KUMPUMZISHA MJUMBE MMOJA NA kuongeza mjumbe mwingine kwenye baraza la wadhamini. mwenyekiti kuomba ridhaa ya kumteua mjumbe mmoja bila ya kuitisha mkutano mkuu kupunguza gharama kwaklabu.
5. KUPITIA NA KUJADILL MUHTASARI YA MAKUBALIANO YA BODI YA WADHAMINI kulingana na maagizo ya wanachamakukodisha timu ya Yanga na nembo ya Yanga kwa kipindi cha miaka kumi na kupata maamuzi kupitia kura za wanachama.
6. KUJADILI MWEYEKITI ABAKI KAMA MWENYEKITI AU kulingana na maslahi yake kwenye kampuni, kama italeta mgongano katika kampuni yake inayokodisha timu ya Yanga na nembo ya Yanga kwa kipindi cha miaka kumi ili kupata maamuzi kupitia kura za wanachama.
7. KURUDIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA ILIYOAGIZWA NA WANACHAMA KUPITIA VIKAO VYAO MBALIMBALI na baadhi kukataliwa na TFF, baadhi hazijasajiliwa kazi na BMT na baadhi RITA wamezikalia bila kuzifanyia kazi kwa sababu zisizojulikana kupata msimamo wa Wanachama kwa kuzingatia katiba ya Yanga inayosema mikutano ya wanachama ndio yenye mamlaka ya mwisho ilimradi tu maamuzi hayo yaangukie ndani ya sheria za nchi na si sahihi vyombo hivyo kuingiliaa maamuzi halali ya wanachama.
8. KUPITIA UTENDAJI WA KAMATI YA MASHINDANO, RATIBA YA LIGI KUU BARA, ADHABU YA YANGA KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AMBAYO ILISABABISHWA NA FUJO ZA MASHABIKI WA SIMBA.  
9. KUPATA MAAMUZI JUU YA WANACHAMA AMBAO HAWAFIKI KATIKA MIKUTANO BADALA YAKE WANAKUWA WASEMAJI WA YANGA BILA KUWA NA MAMLAKA HAYO na kuleta uchonganishi wa wazi ndani ya klabu, kupotsoha jamii nakuchafua majina ya viongozi wa klabu.
10. TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO KUJAZIA NAFASI ZILIZO WAZI na kupata mwongozo wakutumia katiba ipi kati ya 2010 au 2014.pamojana masahihisho baada ya 2014, au bila ya masahihisho ya 2014 yaliyoamuliwa na wanachama.
11. HOTUBA YA MWENYEKITI –maoni na msimamo wake juu ya maazimio ya wanachama kwenye kikao; kusema anayoyajua ya siri kuhusu yanga na adui wa Yanga na kufafanua wanaoleta vurugu Yanga, baadhi ni mamluki wa wafanyabiashara wenzake walioshindwa kumshinda kwa njia halali na sasa wanaitumia yanga kama sehemu pekee iliyobaki kumuumiza kupitia mbinu zinazotumika hasa kwa kuleta vurugu ndani ya yanga ili kumchafua yeye binafsi, kufanya kwao hivyo ni kushusha hadhi ya klabu na maoni yake kwa maslahi ya yanga, kipi kifanyike.
12. MENGINEYO.
13. SALA.
13.1. Sala ya waislamu ya kubariki maamuzi ya mkutano.
13.2. Sala ya wakristo kubariki maamuzi ya mkutano.
14. Kufunga mkutano.


VPL: LEO MECHI 6, MABINGWA YANGA WAPO KAITABA KUIVAA KAGERA SUGAR!


VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa
Jumamosi Oktoba 22
African Lyon  v Mbeya City [Saa 8 Mchana]
Ndanda FC v Mwadui FC
Mtibwa Sugar v Stand United
Kagera Sugar v Yanga
Azam FC v JKT Ruvu [Saa 1 Usiku]
Maji Maji FC v Ruvu Shooting
+++++++++++++++++++++++
VPL-2016-17-LOGO-1LEO zipo Mechi 6 za VPL, Ligi Kuu Vodacom, na moja ni ile ya Mabingwa Watetezi Yanga ambao wapo Ugenini huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kucheza na Kagera Sugar.
Mechi nyingine 5 za Leo ni mbili zitakazochezwa Jijini Dar es Salaam wakati Azam FC wakicheza na JKT Ruvu juko Azam Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Saa 1 Usiku na ya pili ni ile ya Uwanja wa Uhuru kati ya African Lyon na Mbeya City.
Mechi nyingine ni huko Manungu, Morogoro kati ya Wenyeji Mtibwa Sugar na Stand United na huko Songea kati ya Maji Maji FC na Ruvu Shooting.VPL-OKT20B
Hadi sasa Simba ndio wapo kileleni mwa VPL sasa wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 10 baada ya kushinda Mechi 8, Sare 2 na Kutofungwa.
Timu ya Pili ni Stand United wenye Pointi 20 kwa Mechi 11 na wa 3 ni Yanga wenye Pointi 18 kwa Mechi 9.
Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.
++++++++++++++++++++++++
VPL
YANGA - Mechi zao:
Okt 22 Kagera Sugar v Yanga
Okt 26 Yanga v JKT Ruvu
Okt 29 Yanga v Mbao FC
SIMBA - Mechi zao:
Okt 23 Simba v Toto African
Okt 29 Mwadui v Simba
Nov 2 Stand United v Simba
++++++++++++++++++++++++
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Jumapili Oktoba 23
Simba v Toto Africans
Tanzania Prisons v Mbao FC
Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 22, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...