HABARI YA KIMICHEZO YA HIVI PUNDE 

 

SIMBA RAHA TUPU, MBAO WALIBANA WAKAACHIA WENYEWE, WAMEKUFA 1-0


BAO la dakika za lala salama la kiungp Muzamil Yassin limeifanya Simba SC iendelee kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Simba SC inafikisha pointi 26 baada ya kucheza 10 ikishinda nane na kutoa sare mbili – hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi. Mchezo huo uliochezeshwa na Hance Mabena, aliyesaidiwa na Hajji Mwalukuta wote wa Tanga na Michael Mkongwa wa Njombe, ulianza kwa kasi Simba washambulia zaidi lango la Mbao na dakika ya 18, shuti la Mrundi Laudit Mavugo lilipanguliwa na kipa Emmanuel Mseja na kumkuta Ibrahim Hajibu ambaye naye alipga nje.   
Muzamil Yassin, mfungaji wa bao pekee la Simba dakika ya 87 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Mshambuliaji Mrundi wa Simba, Laudit Mavugo akiminyana na beki wa Mbao FC, Asante Kwasi raia wa Ghana

Winga wa Simba, Shizza Kichuya akimtoka beki wa Mbao FC, Steve Mganya 

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib akipambana katikati ya wachezaji wa Mbao FC 

Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto akipambana na beki wa Mghana wa Mbao, Asante Kwasi  



Mavugo tena dakika ya 20 akamdakisha kipa kwa shuti dhaifu baada ya krosi ya beki Mkongo, Janvier Besala Bokungu.   Mbao nao wakajibu shambulizi baada ya nyota wa zamani wa Yanga, Hussein Swedi kupiga shuti lililopanguliwa na kipa Muivory Coast, Vincent Angban dakika ya 30. Hajib akapiga nje tena dakika ya 41 na Mavugo akapiga juu ya lango dakika ya 43 wote wakiwa wamebaki na kipa wa Mbao. Pius Buswita alijichanganya dakika ya 48 na kushindwa kufunga akiwa kwenye nafasi nzuri ndani ya eneo la hatari la Simba. Kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto akapiga nje dakika ya 54 na dakika ya 60 Blagnon akaifungia Simba bao lililokataliwa na refa Mabena kutoka Tanga akidai kwamba mchezaji aliunawa mpira kabla ya kufunga. Hatimaye Muzamil Yassin aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mtibwa Sugar akawainua vitini mashabiki wa Simba dakika ya 87 akifunga bao zuri kwa kumalizia krosi ya mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon. Kwa ujumla Simba ilicheza vizuri tangu kipindi cha kwanza na kupeleka mashabulizi mengi langoni mwa Mbao, lakini bahati haikuwa yao ingawa pia leo winga Shizza Kichuya aliwekewa ulinzi mkali. Washambuliaji Ibrahim Hajib na Laudit Mavugo walioanzishwa pamoja leo hawakuweza kufurukuta mbele ya ukuta wa Mbao FC ulioongozwa na kiungo mkabaji kutoka Burundi, Youssuf Ndikumana. Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Hussein Sued aliishia kuwasumbua kidogo mabeki wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali na Mganda, Juuko Murshid lakini hakuweza kufunga. Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Frederick Blagnon dk51, Ibrahim Hajib/Mohamed Ibrahim dk58 na Mwinyi Kazimoto. Mbao FC; Emmanuel Mseja, Hussein Sued/Frank Damas dk64, Steve Mganya, Steve Kigocha, Asante Kwasi, Pius Buswita/Boniphace Maganga dk52, Youssouf Ndikumana, Robert Magadula, Salmin Hoza, Emmanuel Mvurekure na Dickson Ambundo. 

 

KONGAMANO LA MABADILIKO YANGA JUMAMOSI TAIFA, LIVE AZAM TV


KONGAMANO kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia litafanyika Jumamosi Oktoba 22 mwaka huu ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam. Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), likiwa na lengo la kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa.
Wanachama wa Yanga wakiwa katika moja ya mikutano ya klabu yao 
Katika taarifa yake, Katibu wa TASWA, Amir Mhando amesema leo kwamba Kongamano halina nia ya kuzuia mabadiliko au kuharakisha mabadiliko katika klabu hizo, badala yake inataka litumike kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wa mpira wa miguu kuhusu mifumo hiyo na aina nyingine ya mifumo ya uendeshaji wa klabu duniani, hivyo kusaidia kujibu maswali mbalimbali  ambayo pengine hayajibiwi ipasavyo. Amesema baadhi ya mambo yatakayozungumziwa ni umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo, pia harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake na itazungumziwa pia mifumo ya uendeshaji ya klabu mbalimbali duniani. "Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka," amesema. Tunaomba mashabiki na wadau wengine mbao hawakualikwa watambue tunathamini mawazo yao, lakini nafasi ya wanaotakiwa kuhudhuria ni chache hivyo wafuatilie kupitia vyombo vya habari.

 

MPAMBANO WA LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII …ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”


NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”.  Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi. Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Saalam. Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.
“Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima aidumbukize ngoma yake ya “Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazotumbuiza. Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye vita vikubwa vya maneno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi.

Thursday, October 20, 2016

Serikali Yapunguza Deni La Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii

SeeBait

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali tayari imeshalipa sh. bilioni 722.7 kati ya sh. bilioni 964.2 za madeni ya michango ya jumla ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 20, 2016) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa wadau wa NSSF ulioanza leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Arusha na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600.

Amesema sekta hiyo imekua kwa asilimia 15 kutoka sh. trilioni 8.9 mwaka 2015 hadi kufikia sh. trilioni 10.2 mwaka 2016. “Hadi kufikia Juni 2016, takwimu zinaonesha idadi ya wanachama imeongezeka na kufikia milioni 2.1. Rasilmali za mifuko zimefikia shilingi trilioni 10.28 na mafao yaliyolipwa kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Juni 2016 ni shillingi trilioni 2.93. Michango ya wanachama kwa mwaka ni shilingi trilioni 2.15 uwekezaji katika nyanja mbalimbali umefikia kiasi cha shilingi trilioni 9.29,” ameongeza.

Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara awaandikie barua waajiri wote wanaodaiwa na shirika hilo na kuwataka wawasilishe fedha wanayodaiwa mara moja na wale ambao hawatalipa ndani muda utakaowekwa wafikishwe mahakamani na yeye apewe taarifa.

“Kumekuwepo na changamoto ya muda mrefu ya baadhi ya waajiri kutolipa michango kwa wakati hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa wanachama hasa wanapofikia muda wa kustaafu. Suala hili halikubaliki, hivyo natoa maelekezo kwa waajiri wote nchini waheshimu sheria na wawasilishe michango yao kwa wakati,” amesisitiza.

Mbali ya kuwabana waajiri, Waziri Mkuu pia amewataka wanunuzi wa nyumba za shirika hilo na wapangaji wote wanaodaiwa wakamilishe malipo yao na wasipofanya hivyo ndani ya muda uliopangwa wafikishwe mahakamani.

“Nimeambiwa pia lipo tatizo la wadaiwa wa nyumba yaani wanunuzi na wapangaji. Suala hili lilitolewa maelekezo na Waziri wa Nchi, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Nataka nisisitize kuwa watu wote walionunua nyumba za NSSF na bado hawajakamilisha malipo na wale waliopanga lakini hawalipi kodi wanatakiwa kulipa haraka au wakabidhi nyumba hizo kwa NSSF ziuzwe kwa watu wengine, vinginevyo nao wafikishwe mahakamani.”

Akizungumzia utendaji wa shirika hilo, Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa shirika hilo na Bodi ya Wadhamini kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa sukari nchini. Amesema kiwanda kitakachojengwa, kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza wanachama katika mfuko wa NSSF.

“Nimefurahishwa na uamuzi wa NSSF na PPF kuungana ili kukabiliana na tatizo la sukari nchini. Tumeelezwa hapa kuwa mashirika haya yatashirikiana kujenga Kiwanda cha Sukari kitakachozalisha tani 200,000 kwa mwaka. Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la Mkulazi lililopo mkoani Morogoro,” amesema.

Mapema, akielezea utendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara alisema limeboresha mafao ya wanachama wake kutoka sh. 80,000 hadi sh. 100,000 kwa mwezi.

Alisema limeanza kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga nyumba za watumishi Dodoma ili kuendana na uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma. “Upembuzi bado unaendelea lakini tumeshabaini kuna uwezekano wa kujenga nyumba 200 hadi 300 mkoani Dodoma,” alisema.

Kuhusu uwekezaji kwenye ujenzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni, Dar es Salaam, Prof. Kahyarara alisema uwekezaji huo unalipa kwa sababu makusanyo ya tozo kwa watumiaji yamefikia asilimia 109. “Tuna uhakika kwamba fedha tulizowekeza zitarudi,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 45 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 900 yenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya waathirika wa tetememo la ardhi mkoani Kagera. Amepokea msaada huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Prof. Samuel Wangwe.

Akiwasilisha msaada huo, Prof. Wangwe alisema wameguswa na tatizo lilitokea mkoani Kagera na wameamua kutoa mchango ili kusaidia juhudi za Serikali kukabiliana na maafa hayo. Pia alisema wamekamilisha ahadi yao ya madawati 6,000 yenye thamani ya sh. milioni 400 ambayo waliitoa awali.

Waziri Mkuu aliwashukuru kwa misaada hiyo na kuwahakikishia kwamba itafikishwa kwa walengwa.
 

Thursday, October 20, 2016

Dk Slaa Aingilia Kati Ugomvi wa Godbless Lema na RC Gambo.......Huu Hapa ni Ujumbe Wake

SeeBait

Ugomvi wa maneno kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema limemuibua katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa aliyeandika ujumbe mrefu akimkingia kifua mbunge huyo.

Gambo na Lema walirushiana maneno juzi mbele ya wafadhili kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maendeleo wa ujenzi wa hospitali itakayohudumia bure wanawake na watoto uliogharimu shilingi bilioni 9.

Kupitia ujumbe huo uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambao alithibitisha kuwa ni wa kwake, Dk Slaa amemrushia lawama Mkuu huyo wa Mkoa akidai kuwa anaijua vizuri historia ya ardhi na mradi huo.
==> Usome Hapo Chini 
 
 Mrisho Gambo,
Naamini hii ID ni ya kwako na hasa kwakuwa kwenye post unaonekana ukizungumza, napata uhakika kuwa ni wewe.

1) Mkuu wa Mkoa, nakuheshimu kwa kuwa cheo chako ni kikubwa sana. Hata hivyo, ulichokifanya leo na " propaganda unazopiga zimenifanya nikudharau na kukupuuza. Ningeliweza kuishia katika kukudharau na kukupuuza, lakini

2) Aibu uliyoiletea Taifa letu leo, inanifanya " nipige kelele" kuwa " siasa za maji taka siyo wakati wake huu.

a). Mhe.Mrisho Gambo, wewe kama Mkuu wa Mkoa unayo au mamlaka au vyombo vya dola kukusaidia kufanya utafiti wa maana kuliko aibu kubwa uliyoiletea Taifa letu mbele ya Wahisani/ Wafadhili wetu kupitia Maternity Africa. Hukufanya hivyo, umeamini propaganda kuliko busara na hekima. Kwa hilo siwezi kukusamehe wala kukuheshimu pamoja na cheo au vyeo vyote ulivyonavyo.

b). Mrisho Gambo, ungelikuwa wa busara iwapo ungelimwomba kiongozi au mwakilishi wa ADF (ulikuwa na uwezo wa kujua ADF ni nani na historiaya yake ni ipi- kwa kupenda propaganda hukufanya hivyo) au Mwakilishi wa Maternity Africa hasa Happy (ambaye alisaini pia barua ya kukualika kuwa mgeni rasmi, au hata Mhe.Mbunge Lema ambaye kimsingi ndiye chimbuko la upatikanaji wa Ardhi hiyo kutoka kwa Marehemu Advocate Mawala (Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi), na pia chimbuko la Upatikanaji mradi kutoka kwa wafadhili wetu.

Kutokupenda kushauriwa na hao wenye kujua mradi imekufanya "kuonekana juha" na " mwongo" kwa kuwa historia haifutwi kwa " propaganda za jukwaani". Lakini kwa bahati mbaya athari ya propaganda imeenda mpaka kuichafua Taifa letu kwa wahisani. Ujenzi ndiyo kwanza unaanza. Umeombwa kufanya "Ground Breaking ceremony", unadhani wawakilishi wa wahisani na hasa kule kwenye chimbuko la fedha wanapata picha gani ya Taifa letu.

c). Mrisho Gambo, busara na hekima ya kawaida ingelikuwezesha kuelewa barua ya mwaliko ambayo imesisitiza mara mbili hivi, kuwa wahusika ni taasisi isiyojihusisha na siasa. Wakasema mradi kwa muda sasa umekumbwa na matatizo yenye sura ya kisiasa. Ulipaswa kutafakari, kutafiti na kutafiti njia makini zaidi ya kuona wakina mama wajawazito, wenye fistula na watoto wachanga hawakosei au hata hawacheleweshewi kupata huduma hiyo kwa sababu za kipuuzi tu. Eti unasoma historia! Unaijua historia au unaota ndoto!

Nimepiga kelele kwa kuwa ninaijua vizuri hiyo historia A to Z. Sikuambii ungeliniuliza, lakini wapo kwenye kikao hicho ambao wasingelihitaji kuisoma bali kuitoa kichwani historia hiyo, tangu kupatikana kwa Ardhi, mchakato wa kuchora ramani, kuisajili na kupata vibali vyote vya Kituo hicho cha Afya (japo kwa kweli ni hospitali, inaitwa kituo cha Afya tu kwa. Sababu za kisheria).

3) Mrisho Gambo, kwa hili Watanzania wa Arusha na wote wenye kujua ukweli hatutakusamehe kwa aibu uliyotupatia, na kujenga misingi ya kutufungia miradi mingine kwa wahisani wetu.

Kama una chembe dogo la busara:
a). Utakaa chini na kutafakari umekosea wapi.

b). Uwe na unyenyekevu uwaite wahusika wote ofisini kwako waombe wakupe " historia kamili" na wakupe mchakato mzima mpaka kufikia siku hii muhimu ya "Ground Breaking ceremony (uzinduzi wa Kazi ya ujenzi).

c). Ukipata Taarifa kamili, uwe na unyenyekevu, acha kiburi. Kiburi hakikusaidii wala haitasaidia jamii unayopaswa kuwatumikia (unless una malengo tofauti). Kwa unyenyekevu mkubwa Waombe msamaha Wahisani wetu kwa kuwaingiza katika " siasa ya Arusha" ambayo hawahusiki nayo; awaombe msamaha wakina mama, watoto na jamii ya Wananchi wa Arusha wapenda maendeleo kwa kuwachafua na kuwaletea vurugu kiasi cha kuifanya Arusha ionekane kila leo ni mahali pa vurugu, kumbuka vurugu husababishwa na viongozi wasiotumia busara na hekima. Uongozi ni busara na hekima siyo mabavu wala nguvu ya mamlaka.

Nimeyasema haya kwa uchungu mkubwa. Mimi siko kwenye siasa, na wala sina interest na siasa. Siangalii uso wa mtu. Kama ambavyo niliaga kuwa " Nastaafu Party Politics, lakini nitapiga kelele pale maslahi ya Taifa langu yanavyokanyagwa" nitakuwa mwendawazimu kunyamaza wakati mradi wa Tshs Takriban 9 Billioni unahatarishwa na upuuzi na uzembe wa kiongozi mmoja mwenye kuendekeza propaganda zisizo na msingi.

Nawaomba sana Radhi wahisani wetu. Mtuvumilie siyo kwa ajili yetu bali kwa ajili ya kina mama na watoto walengwa wa huduma itakayotolewa na " Kituo cha Mama na Mtoto" (propaganda kwamba Hospitali ni ya mke wa Lema zipuuzeni).

Happy, umevumilia mengi katika miradi mingi uliyofadhili na kuisimamia. Usirudi nyuma. Timiza ndoto yako iliyoanza katika umri mdogo sana. Matunda yanaonekana pamoja na vikwazo vya mara kwa mara vya wapinga maendeleo. Viongozi, " Tenganisheni siasa na Maendeleo" Watumikieni Watanzania bila kuangalia nyuso zao, mrengo wao. Siasa ni sayansi na siasa ni utumishi.

Dr.Wilbroad Peter Slaa 


Thursday, October 20, 2016

Wawili mbaroni kwa wizi wa miundombinu ya TANESCO Yenye Thamani ya Milioni 61

SeeBait
Wakazi wawili wa Manispaa ya Kinondoni wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kukutwa na miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yenye thamani ya Sh milioni 61.

Walikutwa na miundombinu ya shirika hilo ikiwemo vifaa kwa ajili ya kuunganishia umeme.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 10 jioni katika maeneo tofauti ya manispaa hiyo.

Alisema katika tukio la kwanza, maeneo ya Makumbusho, polisi wakishirikiana na kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miundombinu ya Tanesco, walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo kwa watu wanaohujumu miundombinu ya shirika hilo.

“Kikosi kazi walifika eneo hilo katika nyumba ya Wilfred Baruti (45) mkazi wa Makumbusho na kufanya upekuzi katika nyumba hiyo na vilipatikana vifaa mbalimbali vinavyotumika kuunganisha umeme vya Tanesco,” alisema Mkondya.

Aidha, alisema pia polisi walikwenda katika nyumba nyingine ya Beatrice Emmanuel (42) mkazi wa Salasala Mabanda Mengi walikofanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa ambavyo ni nyaya aina ya drums mbili, rola ya nyaya aina ya AICC ya umeme wa milimeta 50 ambazo hutumiwa na Tanesco kituo cha Kilimahewa cha Kawe, wilayani Kinondoni.

Alisema upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa kuhusu wizi huo wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni 61,Kulia ni Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.
 
 
 

Thursday, October 20, 2016

Jeshi la Polisi Dar laua majambazi Hatari 6

SeeBait
Watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi hatari, wameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Mbezi kwa Yusuf Makondeni katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Lucas Mkondya, watuhumiwa hao waliuawa katika majibizano ya risasi na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha.

Mkondya alisema wamepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kikundi cha watu wenye silaha, wamejipanga kufanya tukio la ujambazi kwa kutumia silaha kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitoka Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), tawi la Barabara ya Nyerere, ambaye angepita katika barabara hiyo kwenda mkoani Morogoro.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, polisi waliweka mtego na majambazi hao wakitumia gari aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T970 DGZ rangi ya fedha, walionekana wakilifukuza gari la mfanyabiashara huyo, kisha kulipita na kumsimamisha kwa nguvu.

“Majambazi wawili wakiwa na bastola walishuka katika gari hilo. Baada ya kugundua kuwa wameingia kwenye mtego wa polisi, walianza kufyatua risasi kwa askari wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao walianza kushuka huku wakifyatua risasi kuelekea kwa askari,” alisema Kaimu Kamanda Mkondya.

Alisema kutokana na hali hiyo, askari walianza kujibu mashambulizi na kuwaua majambazi hao na baada ya upekuzi, zilipatikana bastola mbili, moja ya kijeshi aina ya Chinese ikiwa na risasi moja ndani ya kasha la risasi; na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita ya risasi yaliyookotwa katika eneo la tukio.

Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa ujambazi.

Katika tukio lingine la Oktoba 17, mwaka huu saa 2:00 usiku katika maeneo ya Tegeta Masaiti, watuhumiwa watatu wa ujambazi wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya Fekon yenye namba MC370 BEY, wakiwa na bunduki aina ya shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walivamia duka la Abdallah Juma (46), mkazi wa Tegeta na kupora fedha za mauzo na kuiba vocha za mitandao mbalimbali, ambazo thamani yake haijafahamika.

“Polisi baada ya kupata taarifa waliwafukuza majambazi hao, walipoona wanakaribiwa na askari, walitupa chini begi walilokuwa nalo na kutelekeza pikipiki yao kisha kukimbia, begi lilipopekuliwa lilipatikana na silaha hiyo,” alisema.

Aidha, wananchi wenye hasira waliendelea kuwakimbiza majambazi hao na kumuua mmoja huku wengine wakikimbilia kusikojulikana. 
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.

Alisema watuhumiwa hao, Ally Makwega (53) mkazi wa Tandika na Fabian Greyson (39) mkazi wa Yombo walikamatwa Oktoba 4, mwaka huu saa 6:00 usiku.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba MC292 AMD aina ya Boxer rangi nyekundu, wanayoitumia kufanya uhalifu, wakiwa na funguo bandia 75 ambazo huzitumia katika kuvunja nyumba mbalimbali ya biashara za kulala wageni, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.

Baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uvunjaji wa maghala na kuiba katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. 
 

Thursday, October 20, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Octoba 20

SeeBait

Thursday, October 20, 2016

Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mhandisi Wa Maji Lindi

SeeBait
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander (pichani mwenye mafaili) kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi.

Waziri Mkuu amemkabidhi Mhandisi huyo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Bw. Stephen Chami na kumuelekeza afanye uchunguzi zaidi juu ya suala hilo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano, Oktoba 19, 2016  wakati alipotembelea mradi wa maji wa Ng'apa ambapo aliagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo.

"Kamanda wa TAKUKURU fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema analipwa Wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Mhandisi hiyo anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za ofisi pamoja na kupokea mshahara bila la kulipa kodi ya mapato ya mshahara (PAYE), kujilipa kiwango kikubwa cha posho pamoja na kusafiri kwa muda mrefu.

Waziri Mkuu alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia hawaonekani kwenye vituo vyao vya kazi. "Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es Salaam."

Alipoulizwa sababu za kutokuwepo ofisini kwake kwa muda mrefu, Mkurugenzi huyo alisema kwamba alikuwa Dar es Salaam akiandika maombi ya fedha kwa ajili ya kutatulia changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo.

"Unatumia siku ngapi kuandika proposal, msomi unatumia mwezi mzima kuandika proposal na unakaa Dar es Salaam hata Katibu Mkuu wako hajui na huko unajilipa posho tu! Tena badala ya kulipwa sh.120,000 kwa siku wewe unajilipa sh.150,000. Hatuwezi kuvumilia hali hii,” amesema.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake siku tatu mkoani Lindi na amerejea jijini Dar es Salaam.
                        
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
 

Thursday, October 20, 2016

Kamati ya Bunge Yakataa faini ya 500,000/- Kwa Kila Kosa Barabarani

Kamati  ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala imekataa mapendekezo ya kufanyia marekebisho Sheria ya Leseni za Uchukuzi ya mwaka 1973 yenye lengo la kuongeza kiwango cha adhabu ya faini hadi kufikia asilimia 500 kwa watakaokiuka masharti ya leseni hizo.

Mapendekezo hayo yaliwasilishwa mbele ya kamati hiyo mjini Dodoma jana na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).

Baada ya kuyakataa mapendekezo hayo, kamati hiyo imetoa muda wa siku mbili kwa Sumatra kuhakikisha inawasilisha mbele ya kamati hiyo mapendekezo yanayokubalika.

Sumatra inapendekeza kuongeza kiwango cha adhabu ya faini kutoka kati ya Sh 10,000 na Sh 50,000 hadi Sh 200,000 na 500,000 kwa watoa huduma za uchukuzi, watakaokiuka masharti ya leseni zao.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Mchengerwa alisema mapendekezo hayo, yatazidi kuwaongezea mzigo Watanzania badala ya kuwasaidia. 

Alisema kiwango hicho cha faini kubwa, kamwe hakitazuia tatizo la ajali za barabarani, zaidi ya kuongeza ukubwa wa tatizo la rushwa.

“Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwasaidia wananchi, lakini mapendekezo haya yatazidi kuwaongezea mzigo kwa sababu kiwango cha faini hizi kama kitapitishwa, watoa huduma za uchukuzi watahamishia hasara yao kwa wananchi,” alisisitiza.

Aliitaka mamlaka hiyo, kwenda kuyafanyia kazi tena mapendekezo hayo kwa kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuwasilisha viwango vya faini vinavyokubalika. 

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Joseph Mhagama ambaye pia ni mbunge wa Madaba, alisema mapendekezo hayo hayana nyongeza yoyote, itakayoisaidia serikali katika kudhibiti tatizo la ajali barabarani.

“Kwa sasa serikali imeweka nguvu zake katika kupunguza ajali za barabarani, lakini kiwango cha faini hizi hakina uhusiano wowote na jitihada hizi zaidi ya kuiongezea Sumatra mapato na kuwapa mzigo walipa kodi,” alisema.

Akiwasilisha mapendekezo ya mamlaka hiyo mbele ya Kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe alisema mapendekezo ya marekebisho ya sheria hiyo, yamelenga  kuiboresha zaidi sheria hiyo ya leseni za uchukuzi.

Alisema marekebisho hayo, pia yatasaidia mamlaka hizo kuendana na mahitaji ya sasa hasa katika eneo la adhabu ya faini, hali itakayopunguza kiwango kikubwa cha kukiukwa kwa masharti ya leseni hizo za uchukuzi.
 
 

Thursday, October 20, 2016

RC Mrisho Gambo apigiwa simu Rais Magufuli. Soma walichozungumza

SeeBait
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu  na kumwambia kuwa ana imani naye na kuwa hajafikiria kutengua uteuzi wake labda kumpandisha cheo.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  baada ya taarifa kuhusu Rais kutengua uteuzi wake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa alipigiwa simu nyingi na watu wengi lakini kabla hajawajibu Rais Magufuli akampigia simu na kumueleza kuwa ana imani naye na kuwa ahakikishe anawatumikia wananchi wa Arusha kwani yeye sio bosi wao bali ni mtumishi wao.

Pia mkuu wa mkoa alieleza kuwa Rais amempa maagizo ya kuhakikisha anasimamia wananchi wa mkoa wa Arusha walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na nchi kwa ujumla.

Aidha, ili kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli ndiye aliyempigia simu, Rais aliomba kuongea na yeyote aliyekuwa karibu ndipo mkuu wa mkoa akampa mmoja wa waliokuwa katika mkutano huo kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli.

Habari ya kutenguliwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya mkuu huyo wa mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuhusu mradi wa ujenzi wa hospitali itakayotoa huduma kwa mama na mtoto mkoani humo.
 
kimataifaaaaaaaaaa
 

Habari | 20.10.2016 | 17:11

Urusi imekubali kusitisha mapigano kaskazini mwa Aleppo, Syria kwa siku tatu kuanzia leo Alhamis na inalifikiria ombi la Umoja wa Mataifa la kuongeza siku nyingine ya nne. Mshauri mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kiutu, Jan Egeland amesema Umoja wa Mataifa, Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu wanaweza kuanza kuwaondoa watu waliojeruhiwa kutoka katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi kuanzia kesho ijumaa. Ameongeza kwamba uhakikisho wa usalama umetolewa na pande zote zinazohasimiana katika mzozo huo. Hata hivyo ameonya kwamba mpango huo wa kuwaondoa mamia ya raia unaweza kuwa mgumu kwa sababu jambo lolote linaweza kutokea. Wagonjwa na waliojeruhiwa watachagua ikiwa wanataka kupelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali mashariki mwa Aleppo au mjini Idlib
 
 
Viongozi wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels, Ubelgiji hawatashiriki majadiliano au mazungumzo ya Uingereza kujitoa katika Umoja huo na Waziri Mkuu wa taifa hilo Theresa May ambaye anahudhuria mkutano huo kwa mara ya kwanza. Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk amesema hayo mara baada ya kuwasili kwamba May, anatarajiwa kuwaelezea kwa kifupi viongozi wengine 27 lakini hapatakuwa na majadiliano hadi pale atakapoanza rasmi mchakato wa kujiondoa. Tusk amekanusha madai kuwa waziri mkuu wa Uingereza anaweza kupokelewa kiuadui na kusema kwamba mazungumzo yatakwenda mazuri. Kuhusu masuala mengine, Tusk amesema Umoja wa Ulaya utabaki na machaguo yote ya kuhusu vikwazo kwa Urusi kutokana na matendo yake nchini Syria. Ameongeza kwamba anayo matumaini Ubelgiji itafikia muafaka wa kutia saini mkataba wa biashara huria na Canada hapo kesho Ijumaa.
 
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ametangaza hii leo mjini Beijing China, kujitenga na mshirika wake wa siku nyingi Marekani wakati akijaribu kuweka uwiano sawa wa kidiplomasia baina ya taifa lake na China. Kauli yake hiyo ameitoa baada ya kukutana na Rais wa China, Xi Jinping ambapo wameahidi kuimarisha uaminifu na urafiki na kuumaliza mzozo wa bahari. Jinping amesema mataifa hayo ni majirani katika bahari ambayo hayapaswi kuwa na uadui na mafarakano. Duterte yupo nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambayo inathithibitisha kutaka kujitenga na Marekani na kuegemea katika mahusiano na China. Viongozi hao wawili wamekuwa na mazungumzo ya kina na kushuhudia utiaji saini wa mikataba 13 ya ushirikiano katika biashara, miundombinu na kilimo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema kwamba idadi ya wakimbizi wa kutokea Sudan Kusini walioingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka mara mbili mwezi uliopita na kufikia elfu 54, wakati mapigano yakiendelea kulikumba taifa hilo changa duniani. Mamia wameuawa nchini Sudan Kusini katika mapigano yaliyoibuka mwezi Julai baina ya majeshi ya Rais Salva Kiir na makamu wa zamani wa rais Riek Machar. Sudan Kusini inakuwa taifa la tatu ambalo ni chanzo kikubwa cha wakimbizi wanaokimbilia Kongo, baada ya Rwanda na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika ripoti yake UNHCR imesema kuwasili kwa wakimbizi hao wa Sudan Kusini ni jambo linalopingwa na wanaharakati wa ndani wa Kongo ingawa wao wanasema wanapinga uwepo wa wapiganaji wa kiongozi wa waasi Riek Machar. Kongo ina jumla ya kiasi ya wakimbizi 430,000 waliosajiliwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa. 

Mahakama kuu nchini Pakistan leo imemwamuru Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Nawaz Sharif kutoa maelezo ya kuhusika kwa familia yake katika kashfa ya fedha na kuzidisha shinikizo kwa kiongozi huyo ambaye serikali yake iliwahi kuondolewa madarakani mara mbili katika miaka ya 90. Mahakama hiyo imetoa muda wa wiki mbili kwa Sharif ili kujibu hati tano za mashtaka zilizofunguliwa na wanasiasa wa upinzani akiwemo nyota wa mchezo wa kriketi Imran Khan. Khan amepanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Islamabad mwezi Novemba Pili, ili kumshinikiza waziri mkuu huyo kuachia madaraka. Hati hizo zilipatikana kama sehemu ya nyaraka milioni zilizovuja katika hati za Panama mapema mwezi huu na kuonyesha kwamba watoto wa kiongozi huyo walinunua mali jijini London, Uingereza kupitia makampuni ya nje ya nchi. Sharif aliahidi kushirikiana na mahakama katika madai dhidi ya familia yake.

KATIKA MICHEZOOOOOOOOOOOO
 
Thursday, October 20, 2016 PIQUE KUKAA NJE WIKI TATU. BEKI wa Barcelona, Gerard Pique anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Manchester City jana huko Camp Nou. Mara ya kwanza ilionekana kuwa beki huyo anaweza kukaa nje kwa siku 10 lakini baada ya vipimo sasa imebainika kuwa itakuwa wiki tatu. Kutokana na hilo sasa Pique anatarajiwa kukosa mechi za La Liga dhidi ya Valencia, Granada na Sevilla pamoja na ule wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya City. Kwa upande mwingine beki wa kushoto Jordi Alba naye anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili kufuatia kupata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo huohuo wa jana. Posted by beki3 at 7:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest RODGERS AMTETEA TOURE. MENEJA wa Celtic, Brendan Rodgers amesema hakuna yeyote duniani aliyeumia zaidi kuliko Kolo Toure baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach. Beki huyo mkongwe wa kimataifa wa Ivory Coast makosa yake aliyofanya katika safu ya ulinzi ndio yalipelekea Lars Stindl na Andre Hahn kufunga mabao hayo mawili na kuipa timu hiyo ya Ujerumani ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi. Toure mwenye umri wa miaka 35, naye pia anajilaumu kwa kipigo hicho. Akihojiwa, Rodgers amesema Toure ni mchezaji mkweli hivyo matukio ya jana lazima yamuumize. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anamwamini Toure kama mpambanaji hivyo anadhani atasahau magumu hayo na kuendelea kucheza kwa ubora wake. Posted by beki3 at 7:16 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest SIWEZI KUBADILI FALSAFA ZANGU - GUARDIOLA. MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kamwe hawezi kubadili falsafa yake pamoja na kikosi chake kufumuliwa mabao 4-0 na klabu yake ya zamani wa Barcelona. Lionel Messi alifunga hat-trick dhidi ya City huku kipa Claudio Bravo akitolewa kwa kushika mpira nje ya eneo lake. Akihojiwa Guardiola amesema hakuna mabadiliko atakayofanya na ataendelea kutumia falsafa hiyohiyo. Akizungumza kuhusu Bravo, Guardiola amesema ni kipa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi hivyo hana shaka naye pamoja na kosa alilofanya. Barcelona wanaongoza kundi C wakiwa na alama tisa, tano zaidi ya City. Posted by beki3 at 7:05 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest NINGEKUWA MAN UNITED KAMA FERGUSON ANGEKUWEPO - VAN PERSIE. MSHAMBULIAJI nyota wa Fenerbahce Robin van Persie amesema angeweza kuwepo katika kikosi cha Manchester United katika mchezo wa leo wa Europa League kama Sir Alex Ferguson angekuwa bado yupo Old Trafford. Van Persie alichaguliw akuwa mchezaji bora wa mwaka wa United katika msimu wake wa kwanza Old Trafford 2012-2013 ambapo pia walitwaa taji la Ligi Kuu. Akihojiwa kama anadhani angeweza bado kuwa United ikiwa Ferguson angeendelea kubakia, Van Persie amesema anadhani bado angekuwa yuko United. Van Persie aliendelea kudai kuwa wakati akisajiliwa United kulikuwa na mipango ya Ferguson kubakia kwa miaka michache zaidi lakini hilo halikutokea. Posted by beki3 at 7:04 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest SIMEONE AVIMBA KICHWA NA KIKOSI CHAKE. MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema amefurahishwa na jinsi timu yake ilivyomiliki mchezo katika ushindi waliopata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Rostov jana. Ushindi huo umeifanya Atletico kuongoza kundi D na Simeone amewapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri. Simeone amesema ulikuwa mchezo mgumu lakini waliwafahamu wapinzani wao na jinsi wanavyocheza. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa wapinzani wao walikuwa wakijilinda kwa kipindi kirefu lakini hilo halikuwakatisha tama wachezaji wake kutengeneza nafasi chache na kutumia waliyopata na kuondoka na alama zote tatu. Posted by beki3 at 7:03 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest MICHO AJITUTUMUA PAMOJA NA UGANDA KUPANGWA KUNDI LA KIFO AFCON. KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic maarufu kama Micho, amesema kuwa hakuna kinachoshindikana baada ya kupangwa kundi moja na Ghana, Mali na Misri katika ratiba ya michuano ya Mataifa ya Afrika iliyopangwa jijini Libreville, Gabon jana jioni. Akihojiwa mara baada ya upangwaji wa ratiba hiyo, Micho alieleza kuwa wakipata maandalizi mazuri wana uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi ya timu kubwa walizonazo katika kundi D. Micho amesema siku zote hakuna linaloshindikana na ili uwe bora ni lazima upambane na walio bora ili kuonyesha uwezo wako. Kocha huyo alienndelea kudai kuwa kundi lao ni gumu na lenye ushindani lakini anawaamini wachezaji wake pamoja na uongozi wa Shirikisho la Soka la nchini hiyo-FUFA. Uganda wataanza kampeni zao za Afcon kwa kucheza na Ghana Januari 17, Misri Januari 21 mechi zote zikifanyika huko Port Gentil kabla ya kuivaa Mali katika mchezo wao wa mwisho wa kundi Januari 25 huko Oyen. Posted by beki3 at 6:59 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Wednesday, October 19, 2016 MAN UNITED IMEONGEZA MASHABIKI MILIONI NANE. WINGA wa zamani wa Manchester United, Jasper Blomqvist anaamini klabu hiyo imejiongezea mashabiki milioni nane wa Paris Saint-Germain-PSG kufuatia kumsajili Zlatan Ibrahimovic majira ya kiangazi. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden alicheza kwa miaka minne Parc des Princes, akishinda mataji 11 na klabu hiyo kabla ya kuondoka kiangazi kufuatia kumaliza mkataba wake. Akihojiwa Blomgvist amesema kutokana na umaarufu mkubwa wa Ibrahimovic nchini Sweden anadhani PSG watakuwa wamepoteza mashabiki wengi nchini humo wanaoweza kufikia hata milioni nane. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa Ibrahimovic ana jina kubwa Sweden yuko kila mahali hata mpaka kipindi hiki ambacho ameacha kucheza soka.

Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Thursday, October 20, 2016 PIQUE KUKAA NJE WIKI TATU. BEKI wa Barcelona, Gerard Pique anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Manchester City jana huko Camp Nou. Mara ya kwanza ilionekana kuwa beki huyo anaweza kukaa nje kwa siku 10 lakini baada ya vipimo sasa imebainika kuwa itakuwa wiki tatu. Kutokana na hilo sasa Pique anatarajiwa kukosa mechi za La Liga dhidi ya Valencia, Granada na Sevilla pamoja na ule wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya City. Kwa upande mwingine beki wa kushoto Jordi Alba naye anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili kufuatia kupata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo huohuo wa jana. Posted by beki3 at 7:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest RODGERS AMTETEA TOURE. MENEJA wa Celtic, Brendan Rodgers amesema hakuna yeyote duniani aliyeumia zaidi kuliko Kolo Toure baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach. Beki huyo mkongwe wa kimataifa wa Ivory Coast makosa yake aliyofanya katika safu ya ulinzi ndio yalipelekea Lars Stindl na Andre Hahn kufunga mabao hayo mawili na kuipa timu hiyo ya Ujerumani ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi. Toure mwenye umri wa miaka 35, naye pia anajilaumu kwa kipigo hicho. Akihojiwa, Rodgers amesema Toure ni mchezaji mkweli hivyo matukio ya jana lazima yamuumize. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anamwamini Toure kama mpambanaji hivyo anadhani atasahau magumu hayo na kuendelea kucheza kwa ubora wake. Posted by beki3 at 7:16 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest SIWEZI KUBADILI FALSAFA ZANGU - GUARDIOLA. MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kamwe hawezi kubadili falsafa yake pamoja na kikosi chake kufumuliwa mabao 4-0 na klabu yake ya zamani wa Barcelona. Lionel Messi alifunga hat-trick dhidi ya City huku kipa Claudio Bravo akitolewa kwa kushika mpira nje ya eneo lake. Akihojiwa Guardiola amesema hakuna mabadiliko atakayofanya na ataendelea kutumia falsafa hiyohiyo. Akizungumza kuhusu Bravo, Guardiola amesema ni kipa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi hivyo hana shaka naye pamoja na kosa alilofanya. Barcelona wanaongoza kundi C wakiwa na alama tisa, tano zaidi ya City. Posted by beki3 at 7:05 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest NINGEKUWA MAN UNITED KAMA FERGUSON ANGEKUWEPO - VAN PERSIE. MSHAMBULIAJI nyota wa Fenerbahce Robin van Persie amesema angeweza kuwepo katika kikosi cha Manchester United katika mchezo wa leo wa Europa League kama Sir Alex Ferguson angekuwa bado yupo Old Trafford. Van Persie alichaguliw akuwa mchezaji bora wa mwaka wa United katika msimu wake wa kwanza Old Trafford 2012-2013 ambapo pia walitwaa taji la Ligi Kuu. Akihojiwa kama anadhani angeweza bado kuwa United ikiwa Ferguson angeendelea kubakia, Van Persie amesema anadhani bado angekuwa yuko United. Van Persie aliendelea kudai kuwa wakati akisajiliwa United kulikuwa na mipango ya Ferguson kubakia kwa miaka michache zaidi lakini hilo halikutokea. Posted by beki3 at 7:04 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest SIMEONE AVIMBA KICHWA NA KIKOSI CHAKE. MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema amefurahishwa na jinsi timu yake ilivyomiliki mchezo katika ushindi waliopata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Rostov jana. Ushindi huo umeifanya Atletico kuongoza kundi D na Simeone amewapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri. Simeone amesema ulikuwa mchezo mgumu lakini waliwafahamu wapinzani wao na jinsi wanavyocheza. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa wapinzani wao walikuwa wakijilinda kwa kipindi kirefu lakini hilo halikuwakatisha tama wachezaji wake kutengeneza nafasi chache na kutumia waliyopata na kuondoka na alama zote tatu. Posted by beki3 at 7:03 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest MICHO AJITUTUMUA PAMOJA NA UGANDA KUPANGWA KUNDI LA KIFO AFCON. KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic maarufu kama Micho, amesema kuwa hakuna kinachoshindikana baada ya kupangwa kundi moja na Ghana, Mali na Misri katika ratiba ya michuano ya Mataifa ya Afrika iliyopangwa jijini Libreville, Gabon jana jioni. Akihojiwa mara baada ya upangwaji wa ratiba hiyo, Micho alieleza kuwa wakipata maandalizi mazuri wana uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi ya timu kubwa walizonazo katika kundi D. Micho amesema siku zote hakuna linaloshindikana na ili uwe bora ni lazima upambane na walio bora ili kuonyesha uwezo wako. Kocha huyo alienndelea kudai kuwa kundi lao ni gumu na lenye ushindani lakini anawaamini wachezaji wake pamoja na uongozi wa Shirikisho la Soka la nchini hiyo-FUFA. Uganda wataanza kampeni zao za Afcon kwa kucheza na Ghana Januari 17, Misri Januari 21 mechi zote zikifanyika huko Port Gentil kabla ya kuivaa Mali katika mchezo wao wa mwisho wa kundi Januari 25 huko Oyen. Posted by beki3 at 6:59 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Wednesday, October 19, 2016 MAN UNITED IMEONGEZA MASHABIKI MILIONI NANE. WINGA wa zamani wa Manchester United, Jasper Blomqvist anaamini klabu hiyo imejiongezea mashabiki milioni nane wa Paris Saint-Germain-PSG kufuatia kumsajili Zlatan Ibrahimovic majira ya kiangazi. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden alicheza kwa miaka minne Parc des Princes, akishinda mataji 11 na klabu hiyo kabla ya kuondoka kiangazi kufuatia kumaliza mkataba wake. Akihojiwa Blomgvist amesema kutokana na umaarufu mkubwa wa Ibrahimovic nchini Sweden anadhani PSG watakuwa wamepoteza mashabiki wengi nchini humo wanaoweza kufikia hata milioni nane. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa Ibrahimovic ana jina kubwa Sweden yuko kila mahali hata mpaka kipindi hiki ambacho ameacha kucheza soka.

Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO JUU, GERMANY, BRAZIL ZAIKARIBIA, TANZANIA YAPOROMOKA 12 NI YA…..!


FIFA-RANKINGSFIFA Leo imetoa Listi ya Ubora Duniani na Vinara wamebaki Argentina lakini sasa wanakaribiwa na Mabingwa wa Dunia Germany na Brazil waliopanda kuchukua Nafasi za Pili na za Tatu wakati Beligium ikishuka Nafasi 2.
Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka Nafasi 12.
Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio Nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa Novemba 24.
FIFA-RANKING-TZ
20 BORA:
1 Argentina
2 Germany
3 Brazil
4 Belgium
5 Colombia
6 Chile
7 France
8 Portugal
9 Uruguay
10 Spain
11 Wales
12 England
13 Italy
14 Switzerland
15 Poland
16 Croatia
17 Mexico
18 Costa Rica
19 Ecuador
20 Netherlands

Thursday, October 20, 2016 PIQUE KUKAA NJE WIKI TATU. BEKI wa Barcelona, Gerard Pique anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Manchester City jana huko Camp Nou. Mara ya kwanza ilionekana kuwa beki huyo anaweza kukaa nje kwa siku 10 lakini baada ya vipimo sasa imebainika kuwa itakuwa wiki tatu. Kutokana na hilo sasa Pique anatarajiwa kukosa mechi za La Liga dhidi ya Valencia, Granada na Sevilla pamoja na ule wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya City. Kwa upande mwingine beki wa kushoto Jordi Alba naye anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili kufuatia kupata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo huohuo wa jana.

Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef

KISAGO CHA BARCA: GUARDIOLA HABADILI FALSAFA YA MBINU ZAKE!


>”MPAKA SIKU YA MWISHO UKOCHA TUTAANZA KWA PASI YA KIPA WETU!”
CITY-BRAVO-RCPep Guardiola amesema hatabadili Falsafa ya Mbinu zake licha ya Manchester City Jana kutwangwa 4-0 na Klabuyake ya zamani Barcelona huko Nou Camp kwenye Mechi ya Kundi C la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi hiyo Lionel Messi alipiga Hetitriki na moja kufungwa na Neymar huku Kipa wa City Claudio Bravo, Mchezaji wa zamani wa Barca, aliefanya kosa kubwa na kuzawadiwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54.
Guardiola ameeleza: “Hamna mabadiliko. Mpaka Siku yangu ya mwisho kama Kocha ntajaribu kuanza kwa kucheza toka kwa Kipa wetu!”
Huku Barca wakiongoza Bao 1, mapema Kipindi cha Pili, Kipa Bravo aliinasa Pasi ndefu na alipotaka kuanza Mpira kwa Beki wake kama ilivyo kawaida yake badala ya kupiga mbele, Pasi yake hiyo ikanaswa na Luis Suarez ambae alipiga juu Mpira kumvuka Bravo na Kipa huyo akaruka juu na kuucheza Mpira kwa Mikono wakati akiwa nje ya Boksi.
Kwa kosa hilo, Bravo akapewa Kadi Nyekundu na City kubaki Mtu 10.
Kuhusu kosa hilo la Bravo ambae aliletwa City kutoka Barca kumbadili Kipa Namba Wani wa England Joe Hart kwa sababu tu hutumia miguu kuanzisha Gemu toka Golini na kuwapasia Mabeki wake badala ya kubutua mbele, Guardiola ameeleza: “Wakati mwingine kuna makossa ana wakati mwingine unalazimika kupiga Mpira nje lakini mara nyingi, tukicheza vizuri, Mpira huanzia kwa Pasi ya Kipa.”
Aliongeza: “Ni wazi anajua alichofanya kwa sababu ana uzoefu mkubwa nay eye ni mmoja kati ya Makipa Bora katika Miaka 10 iliyopita, sina wasiwasi nae!”
Hivi sasa City hawajashinda katika Mechi zao 4 zilizopita lakini bado wapo kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, na kipigo hiki ni cha kwanza kwa Guardiola katika Mechi zake 11 tangu ashike hatamu Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
- Pep Guardiola ataifikia Rekodi yake ya kwenda Mechi nyingi bila kushinda, ya Mechi 5, ikiwa Jumapili watashindwa kuifunga Southampton.
+++++++++++++++++++++++++++
Akiongelea Timu yake kuifikia kiwango cha Barcelona, Guardiola amefafanua: “Tumefungwa 4-0 lakini sie ni Klabu mpya, ndio tunaanza kujuana. Kwa Miaka 35 hatukuwepo Ulaya! Siku zote ni ngumu kucheza na Barceloana ukiwa na 11. Tulipokuwa 10 Gemu ilikwisha!”
Msimamo hivi sasa kwenye Kundi C ni kuwa Barca wako kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya City walio Nafasi ya Pili na wa 3 ni Borussia Monchengladbach na mkiani ni Celtic.
UCL-C-OKT20
MAN CITY – Mechi zijazo:
Jumapili Oktoba 23
EPL   
1530 Man City v Southampton        
Jumatano Oktoba 26
EFL Cup – Raundi ya 4
2200 Man Utd v Man City       
Jumamosi Oktoba 29
EPL
1700 West Brom v Man City            
Jumanne Novemba 1
UCL - Kundi C      
Man City v Barcelona    


TATHMINI: LEO MANCHESTER UNITED V FENERBAHCE


MANUNITED-FENERHII LEO Manchester United wataingia Uwanjani kwao Old Trafford Jijini Manchester kucheza Mechi yao ya 3 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Ikiwa hii Leo, kwenye Mechi nyingine ya Kundi A, Feyenoord itashindwa kuifunga Zorya Luhansk huko Rotterdam, Netherlands, basi Man United wakiifunga Fenerbahce watatwaa uongozi wa Kundi A.
Timu zote, Man United na Fenerbahce, zinaingia kwenye Mechi hii zikitoka kwenye Sare za 1-1 katika Ligi za Nchini kwao wakati Fenerbahce, chini ya Kocha Mholanzi Dick Advocaat, wakitoka 1-1 na Osmanlispor Jumapili iliyopita matokeo ambao yamezidi kuwadidimizi kwenye ligi na kuleta wasiwasi kwa hatima ya Kocha wao.
Man United wao walitoka 1-1 na Liverpool huko Anfield hapo Jumatatu Usiku.
Kwenye Kundi A, Fenerbahce, ambao ndio Vinara, kwenye Mechi 2 za kwanza, walitoka Sare na Zorya Luhansk Ugenini na kushinda Nyumbani 1-0 dhidi ya Feyenoord wakati Man United walifungwa 1-0 na Feyenoord huko Rotterdam na kuichapa Zorya Luhansk 1-0 Uwanjani Old Trafford.
Akiongea hapo Jana, Meneja wa Man United Jose Mourinho alikuwa mgumu kudokeza Kikosi chake kitakachoanza hii Leo mbali ya kusema Luke Shaw atakuwemo na kudokeza Henrikh Mkhitaryan yuko fiti na yumo katika kundi la Wachezaji wanaoweza kucheza.
Pia, Majeruhi Anthony Martial na Morgan Schneiderlin, wamerejea Mazoezini na huenda wakashiriki.EUROPALIGI-A-STAND-OKT19
Kwa upande wa Fenerbahce, inaweza ikamtumia Mchezaji wa zamani wa Man United Robi van Persie ambae hii itakuwa ni mara ya kwanza kurejea Old Trafford tangu auzwe huko Mwaka Jana.
Van Persie amerejea Uwanjani hivi karibuni baada ya kuwa majeruhi kwa muda.
Pia Fenerbahce inae Sentahafu Martin Skrtel, Mchezaji wa zamani wa Liverpoo, Mahasimu wa Man United, ambae nae alihamia huko mwanzoni mwa Msimu huu na huyu ni hakika kuanza Mechi hii akishirikiana na beki Simon Kjaer.
Katika safu yao ya mashambulizi yupo Mchezaji wa Mkopo kutoka Sunderland, Jeremain Lens, ambae ndie huwapa kasi mbele.
++++++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Mechi ya kwanza kabisa kwa Wayne Rooney kuichezea Man United ni Septemba 2004 dhidi ya Fenerbahce kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Rooney alipiga Hetitriki wakati Man United ikishinda 6-2.
+++++++++++++++++++++++++++++
Man United na Fenerbahce zimeshakutana mara 4 huko nyuma na Man United kushinda mara 3 na Fenerbahce mara 1 huko Instanbul wakati Man United wakichezesha Kikosi dhaifu kwenye Mechi ya Ulaya wakati wakiwa tayari wameshafuzu Kundi lao.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED – Mechi zao za Kundi A:
**Saa za Bongo
MD 1 – Alhamisi Sep 15 – Feyenoord 0 Man United 1
MD 2 – Alhamisi Sep 29 22:05 –  Man United 1 Zorya Luhansk 0
MD 3 – Alhamisi Okt 20 22:05 – Man United v Fenerbahce SK
MD 4 – Alhamisi Okt 27 2000 –  Fenerbahce SK v Man United
MD 5 – Alhamisi Nov 24 2305 – Man United v Feyenoord
MD 6 – Alhamisi Des 8 2100 –  Zorya Luhansk v Man United
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Man United: Romero, Darmian, Smalling, Bailly, Shaw, Pogba, Fellaini, Rashford, Rooney, Lingard, Ibrahimovic
Fenerbahce: Demirel, Van der Wiel, Kjaer, Skrtel, Kaldirim, Topal, Souza, Potuk, Van Persie, Sen, Emenike
REFA: Benoît Bastien (France)
UEFA EUROPA LIGI
Ratiba:
Alhamisi Oktoba 20
KUNDI A
Feyenoord v Zorya Luhansk 2205
Man United v Fenerbahçe 2205   
KUNDI B
BSC Young Boys v Apoel Nicosia 2205   
Olympiakos v FC Astana 2205     
KUNDI C
FSV Mainz 05 v Anderlecht 2205 
Saint-Étienne v FK Qabala  2205 
KUNDI D
AZ Alkmaar v Maccabi Tel-Aviv 2205     
Dundalk v Zenit St Petersburg 2205      
KUNDI E
AS Roma v Austria Vienna  2205 
Viktoria Plzen v Astra Giurgiu 2205        
KUNDI F
KRC Genk v Athletic Bilbao 2205 
Rapid Vienna v Sassuolo 2205    
KUNDI G
Celta Vigo v Ajax 2000     
Standard Liege v Panathinaikos 2000    
KUNDI H
Konyaspor v Sporting Braga 2000
Shakt Donsk v KAA Gent 2000    
KUNDI I
FC RB Salzb v Nice 2000   
FK Krasnodar v Schalke 2000      
KUNDI J
FK Qarabag v PAOK Salonika 1800        
Slovan Liberec v Fiorentina 2000
KUNDI K
Hapoel Be'er Sheva v Sparta Prague 2000       
Inter Milan v Southampton 2000 
KUNDI L
Osmanlispor v Villarreal 2000      
Steaua Buc v FC Zürich 2000      
TAREHE MUHIMU
Droo
26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16
17/03/17: Robo Fainali
Makundi
15/09/16: Mechidei 1
29/09/16: Mechidei 2
20/10/16: Mechidei 3
03/11/16: Mechidei 4
24/11/16: Mechidei 5
08/12/16: Mechidei 6
16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Marudiano
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi za Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Marudiano
24/05/17: Fainali (Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden)


RIPOTI SPESHO

VPL: JAHAZI AZAM FC LAZIDI KUTOTA, MECHI 6 BILA USHINDI!

>LEO SIMBA KUIPIGA BAO MBAO FC?
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Jumatano Oktoba 19
Azam FC 1 Mtibwa Sugar 1
Ruvu Shooting 1 Mwadui FC 1
Ndanda FC 1 Mbeya City 1
Tanzania Prisons 2 Stand United 1
Toto Africans 0 Yanga 2
African Lyon 0 Maji Maji FC 2
++++++++++++++++++++++++
VPL-2016-17-LOGO-1AZAM FC, Timu ambayo iliibuka na kuwa tishio kubwa kwa Vigogo wa Soka Nchini Yanga na Simba, Msimu huu jahazi lao lazidi kutota baada ya Jana kutoka Sare 1-1 na Mtibwa Sugar ukiwa ni mwendelezo wao mbovu wa kutoshinda katika Mechi 6 za VPL, Ligi Kuu Vodacom.
Azam FC, chini ya Kocha toka Spain Zeben Hernandez, sasa wapo kwenye wimbi la Mechi 6 bila ushindi lililoanzia kwa vipigo toka kwa Simba na VPL-OKT20Ndanda FC, Sare na Ruvu Shooting na kisha kufungwa na Stand United na kufuata Sare na Yanga na hii ya Mtibwa Sugar.
Mechi hii, iliyoanza Jana Saa 1 Usiku huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, ilianza kwa Mtibwa Sugar kufunga Bao Dakika ya Pili tu kupitia Rashid Mandawa na Azam FC kusawazisha katika Dakika ya 11 kupitia Penati ya Himid Mao.
Matokeo hayo yameiweka Mtibwa Sugar Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 16 kwa Mechi 11 wakati Azam FC wapo Nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 13 kwa Mechi 10.
Leo VPL itaendelea kwa Mechi 1 ndani ya Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Vinara Simba na Mbao FC.
HABARI ZA AWALI:
++++++++++++++++++++++++
VPL: MABINGWA YANGA WAINYUKA TOTO, NDANDA-MBEYA SARE, STAND UNITED YANYOOSHWA NA PRISONS!
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba/Matokeo:
Jumatano Oktoba 19
Azam FC v Mtibwa Sugar [Kuanza Saa 1 Usiku]
Ruvu Shooting 1 Mwadui FC 1
Ndanda FC 1 Mbeya City 1
Tanzania Prisons 2 Stand United 1
Toto Africans 0 Yanga 2
African Lyon 0 Maji Maji FC 2
++++++++++++++++++++++++
Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga, hii Leo wameichapa Toto Africans 2-0 huko CCM Kirumba Mwanza na kujichimbia Nafasi ya Tatu.
Yanga sasa wana Pointi 18 kwa Mechi 9 wakitanguliwa na Stand United wenye Pointi 20 kwa Mechi 11 na kileleni wapo Simba waliocheza Mechi 9 na wana Pointi 23.
Bao za Yanga hii Leo zilifungwa kila Kipindi na Mzambia Obrey Chirwa na Penati ya Simon Msuva.
Kwenye Mechi nyingine hii Leo, huko Mlandizi Ruvu Shooting na Mwadui FC zilitoka 1-1 na ni matokeo ambayo pia yalitokea huko Nangwanda, Mtwara, Ndanda FC walipocheza na Mbeya City,na ngoma kuwa 1-1.
Huko Sokoine, Mbeya Tanzania Prisons iliinyuka Stand United Stand United 2-1 na kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam African Lyon ililala 2-0 toka kwa Maji Maji FC.
Mechi iliyobakia jii Leo ni ya huko Chamazi, Azam Complex, wakati Wenyeji Azam FC wakicheza na Mtibwa Sugar kwenye Mechi iliyoanza Saa 1 Usiku.
VPL itaendelea tena Alhamisi kwa Mechi  kati ya Simba na Mbao FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
++++++++++++++++++++++++
VPL
YANGA - Mechi zao:
Okt 22 Kagera Sugar v Yanga
Okt 26 Yanga v JKT Ruvu
Okt 29 Yanga v Mbao FC
SIMBA - Mechi zao:
Okt 20 Simba v Mbao FC
Okt 23 Simba v Toto African
Okt 29 Mwadui v Simba
Nov 2 Stand United v Simba
++++++++++++++++++++++++
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Alhamisi Oktoba 20
Simba v Mbao FC

Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 20, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...