Monday, October 24, 2016
Serikali kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo kwa kipaumbele
Fani
hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati,
uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi
asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na
miundombinu.
Serikali
inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani
hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya
kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa
wataalamu waliowakusudia kubaki.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella
Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo
kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na
utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano
na serikali.
Alisema
suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa
lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni
ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini
lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.
Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.
“Serikali
itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi
wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe,
wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”
Alisema
kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza
kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi,
zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.
Monday, October 24, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya Octoba 24
MAGAZETI HAYOOOOOOOOOOOO |
Monday, October 24, 2016
Mbowe aikumbuka Oparesheni UKUTA.....Asema Serikali inaendeshwa kwa hila
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema Demokrasia, Katiba na Sheria haziheshimiwi na kwamba Jeshi la Polisi limekuwa wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kilichofanywa kwenye uchaguzi wa umeya wa Manispaa ya Kinondoni kinawapa sababu ya kurejea operesheni yao wanayoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA).
Mbowe
amesema hayo Oktoba 23, 2016 alipofika eneo ulipofanyika uchaguzo wa
Meya Kinondoni ambapo madiwani wa Ukawa walisusia uchaguzi huo na kudai
kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli, ameshirikiana
na CCM kuhujumu zoezi hilo, hivyo wametangaza kwenda mahakamani kupinga
uchaguzi huo baada ya CCM kuendelea na uchaguzi huo na kutangaza
mshindi.
Njama
zinazodaiwa kufanywa na mkurugenzi huyo ni kugawanya madiwani kinyume
na kanuni kwa kuhamisha madiwani wa upinzani kwenda Halmashauri ya
Ubungo na kuwahamishia Kinondoni madiwani wa CCM kutoka halmashauri
nyingine.
Mbowe
amesema Serikali inaendeshwa kwa hila kwani licha ya uchaguzi kufanyika
siku ambayo si ya kazi, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, alikataa barua
iliyoandikwa na madiwani Jumamosi Oktoba 22 kuzuia uchaguzi huo kwa
kudai kuwa si siku ya kazi.
Aliendelea
kwa kumlaumu Rais Dk. John Magufuli kwamba ameanzisha utamaduni wa
kuuwa demokrasia na kwamba analiletea taifa madhara makubwa.
Kwa
upande wake Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), amesema wametoka
kwenye uchaguzi huo baada ya baadhi ya madiwani wao kuzuiwa kuingia
kwenye kikao hicho.
Mdee alisema kuwa CCM wameingiza madiwani ambao si wajumbe halali wa kikao hicho kwasabau wanatoka katika halmashauri zingine.
“Humo
ndani yumo Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa na
alisajiliwa kama mkazi wa Ilala na alipiga kura za umeya Ilala hivyo
mnaweza kuona uhuni unaofanywa.
“Lakini
yumo pia Tulia Akson (Dk. Tulia Akson, Mbunge wa Kuteuliwa na Naibu
Spika) ambaye si mkazi wa Kinondoni yeye amesajiliwa kama mkazi wa
Ubungo,” alisema Mdee.
Amesema
kwa mujibu wa kanuni Halmashauri moja haiwezi kuwa na wabunge wa
kuteuliwa zaidi ya watatu na kueleza kuwa katika kikao hicho wamo
wabunge wanne wa kuteuliwa.
Hivyo, kutokana na hali hiyo Mdee amesema watakwenda mahakama ili kupata tafsiri za kisheria za suala hilo kupata haki.
Monday, October 24, 2016
Makamba asikitishwa na upungufu wa maji katika Ziwa Rukwa....Atoa maagizo kwa wakurugenzi
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January
Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara
yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan
pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri
Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000
kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016
chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.
“Tafiti
zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine
kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na
ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.
Katika
ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri
Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa
mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru
Ziwa Rukwa.
Pia,
wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga
pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa
alama maalumu ‘beacons’ ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi
hili lifanyike haraka.
Aidha,
Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha
masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na
ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. “nimetembea zaidi ya kilomita 200
sijaona miti iliyopandwa,” Makamba aliongezea.
Wakazi
wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani
itakuwa lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuripoti na
miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri
Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi
katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.
Katika
hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali wa dini
na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani,na kuahidi
kugharamia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo nakusisitiza
agenda ya mazingira iwepo.
Mkoani
Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na
wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika
Monday, October 24, 2016
Jinsi ya Kuandaa na Kutayarisha Dawa Lishe ya Kunenepesha,Kurutubisha na Kuongeza Mwili
Dawa-lishe
ya kuongeza, kurutubisha na kunenepesha mwili, ni dawa maalumu
kwa watu wenye uzito wa chini ( Under weight ) ambao wanataka
kuongeza mwili na uzito.
Dawa
hii huwasaidia watu ambao miili yao imedhoofu kutokana na
sababu mbalimbali kama vile kuugua magonjwa na maradhi
mbalimbali.
Na kwa wale watu wembamba ambao wanataka kuongeza miili yao, dawa hii huwasaidia vizuri sana.
FAHAMU JINSI NA NAMNA YA KUANDAA NA KUTAYARISHA DAWA-LISHE MAALUMU YA KUONGEZA, KURUTUBISHA NA KUNENEPESHA MWILI.
MAHITAJI YA DAWA –LISHE
i. Dawa –lishe vijiko viwili vikubwa.
ii. Asali ya tende vijiko vitano vikubwa.
iii. Tangawizi ya unga vijiko vikubwa viwili
iv. Unga wa ufuta
v. Maziwa fresh nusu lita
vi. Maji ya moto kiasi cha milimita mia mbili na hamsini ( 250 mills )
MATAYARISHO
i.
Chukua vijiko vinne vyenye dawa lishe yako kisha chemsha na
nusu lita ya maji hadi mchanganyiko wako utokote halafu ipua,
chuja , makapi weka pembeni kisha hifadhi juisi yako.
ii.Tayarisha uji kwa kutumia unga wa ufuta na maziwa fresh
iii.Chukua
vijiko viwili vikubwa vya tangawizi ya unga kisha changanya
kwenye kikombe cha maji ya moto chenye ujazo wa milimita mia
mbili hamsini ( 250 mills )
MATUMIZI:
i. Tumia kunywa nusu lita ya dawa –lishe yako kisha
ii.Tumia kula vijiko vinne vikubwa vya asali ya tende
iii.Kisha tumia kunywa vikombe vinne vya uji wa ufuta ulio changanywa na maziwa fresh
iv.Halafu kunywa glasi moja ya moto iliyo changanywa na vijiko viwili vikubwa vya tangawizi ya unga.
UTAFANYA HIVYO MARA MBILI KWA SIKU KWA MUDA WA SIKU THELATHINI MFULULIZO.
Baada
ya siku thelathini, utaangalia na kujitathmini kiasi ulicho
ongezeka. Kama utataka kuendelea kuongezeka zaidi, utaendelea
kutumia dozi hii hadi hapo utakapo fikia kiwango utakacho rizika
nacho.
BEI YA DAWA-LISHE : Bei ya Dawa-Lishe ni SHILINGI ELFU HAMSINI TU (TSHS.50,000/=)
JINSI YA KUIPATA DAWA LISHE:
Dawa
hii inapatikana katiuka duka la dawa asilia la NEEMA HERBALIST
& NUTRITIONAL FOODS CLINIC lililopo jijini DAR ES SALAAN
katika eneo la TABATA MAKOKA karibu na SHULE YA SEKONDARI YA
MT. ANNUARITE.
Unaweza kufika moja kwa moja katika ofisi zetu AU unaweza kuletewa mahali popote ulipo jijini Dar Es salaam.
Kwa
wakaazi wa ZANZIBAR watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa
boti na kwa wateja wetu wa ughaibuni watatumiwa dawa kwa njia
ya POSTA au DHL.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa simu
0766 53 83 84
Vile
vile tunayo dawa ya asili iitwayo JIKO ambayo inatibu na
kuponyesha kabisa TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.
Kufahamu kuhusu SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME pamoja na jinsi dwa ya JIKO inavyo fanya kazi tafadhali tembelea:
Monday, October 24, 2016
CCM Wamdhibiti Maalim Seif Zanzibar....SMZ Yapiga Marufuku Siasa Nyumba za Ibada
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibada kwa shughuli za kisiasa Visiwani Zanzibar.
Msimamo
huo wa Serikali umekuja siku chache tangu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim
Seif Sharif Hamad, kutumia kila siku za Ijumaa kufikisha ujumbe katika
msikiti atakaoswali.
Akitoa
tamko la Serikali jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa yote
ya Zanzibar kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika mikoa yao.
“Kwa
taarifa hii Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa kupitia kamati zao za
ulinzi na usalama kusimamia utekelezaji wa agizo hili katika mikoa yao,”
alisema Waziri Aboud.
Alisema Serikali imewaagiza wakuu hao wa mikoa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo.
Waziri
Aboud alisema kwamba viongozi wa dini na kamati zao katika nyumba za
ibada watakaoruhusu wanasiasa kuendesha shughuli za kisiasa
watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Alisema
kwamba hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi
Unguja katika Misikiti ya Mbuyuni, Kihibnani na Kwabiziredi kumetokea
tabia kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kupita na kutoa hotuba za
kisiasa katika misikiti hiyo.
Waziri
huyo alisema kwamba shughuli za vyama vya siasa zinaendeshwa chini ya
sheria N0 5 ya mwaka 1992 ambayo imeeleza wazi mipaka na shughuli za
kisiasa ziendeshwe chini ya sheria hiyo.
“Vitendo
vinavyofanywa na viongozi hao wa kisiasa wanaotumia nyumba za ibada
kama majukwaa ya kisiasa wanakwenda kinyume na dhamira ya katiba na
sheria za nchi ikiwemo sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992” Alisisitiza Waziri Aboud.
Waziri
Aboud alisema kwamba shughuli zote za dini ya kiislamu Zanzibar
zinasimamiwa kupitia sheria namba 9 ya mwaka 2001, namba 2 ya mwaka 2007
na namba 3 ya mwaka 1985 zinazoongoza Taasisi mahsusi kama vile Ofisi
ya Mufti, Ofisi ya Mahakama ya Kadhi na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya
Amana.
Alisema
kupitia katiba na sheria , uhuru wa mtu kuabudu dini anayoitaka
umetolewa bila kuingiliwa na itikadi za vyama vya siasa kama
inavyobainishwa na katiba zote mbili ibara ya 19 ambazo zinaeleza
umuhimu wa uhuru wa mtu kuamini dini aitakayo kwa misingi ya kukuza
usalama na amani katika jamii.
Monday, October 24, 2016
Sare za CCM zamshusha cheo Mwalimu Mkuu
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno
anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM
kwenye mahafali ya kidato cha nne.
Pia,
taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya
walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu
ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta
michango yote mashuleni.
Otieno,
ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo
kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti
wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye
amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya
Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.
Monday, October 24, 2016
Lipumba aitaka Chadema Kutoingilia Mgogoro CUF......Aifananisha Opareshi UKUTA na Biskuti
Kauli
hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
wanachama wa chama hicho katika kikao cha ndani, kilichofanyika Wilaya
ya Kinondoni ambapo alisema Chadema kushindwa kutekeleza Operesheni
Ukuta ni dhahiri chama hicho kimeshindwa kutekeleza kile wanachoahidi
kwa Watanzania.
Alisema
mpaka sasa kumekua na vikao mbalimbali vinavyofanywa na viongozi wa
Chadema kwa ajili ya kuivuruga CUF, jambo ambalo alisema haliwekezani.
“Chadema
wanajitahidi kutuvuruga kwa kutuma waasi wa chama hiki, lakini naomba
niwaambie hawawezi, CUF ni ngangari hata serikali inajua na
wanachokifanya ni kupoteza muda bure.
“Unajenga Ukuta wa biskuti, ukiumwagia juisi unamong’onyoka, Ukuta gani huo, huu muziki wa CUF ni ngangari hawauwezi,” alisema Lipumba.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho wana kesi mahakamani, wanachama wa chama
hicho wataendelea na shughuli za kukijenga chama hicho pamoja na
kuwasisitiza kuwa na msimamo wa kutetea chama na katiba yake, jambo
ambalo linaweza kuwasaidia kufikia malengo waliyokusudia ya kushika dola
kafika Uchaguzi wa mwaka 2020.
Alisema
kutokana na hali hiyo, rasilimali za chama hicho zinasimamiwa kwa
umakini chini ya walinzi wa chama hicho, Blue Guard ambao Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ni wavamizi hawatambui.
“Ninamshangaa
Maalim Seif sasa hivi anaibuka na kusema hawatambui walinzi wa chama
Blue Guard ambao miaka yote walikua wanamlinda pamoja na rasilimali za
chama, lakini hayo yamekwisha nitazidi kumwomba aje tujenge chama hata
kama kesi inaendelea mahakamani,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano anayemunga mkono
Profesa Lipumba, Abdallah Kambaya alisema kupoteza nafasi ya umeya na
naibu wake katika Manispaa ya Kinondoni ni matokeo ya mgogoro wa CUF na
kutokuwepo ushirikiano ndani ya Ukawa.
“Maalim
Seif anaunga mkono Ukawa, mbona wanachama wa Ukawa wameshindwa
kutusaidia ili kupata meya na naibu wake kwenye uchaguzi wa leo?
(jana),” alihoji.
Monday, October 24, 2016
Serikali kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo kwa kipaumbele
Fani
hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati,
uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi
asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na
miundombinu.
Serikali
inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani
hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya
kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa
wataalamu waliowakusudia kubaki.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella
Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo
kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na
utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano
na serikali.
Alisema
suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa
lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni
ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini
lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.
Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.
“Serikali
itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi
wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe,
wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”
Alisema
kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza
kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi,
zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.
Reviewed by RICH VOICE
on
Oktoba 24, 2016
Rating:
Hakuna maoni