habari za leooo
Monday, October 10, 2016
Mahakama Kuu Yatoa Kibali Kwa CUF Kufungua Kesi Dhidi ya Msajili wa Vyama na Lipumba ....... Bodi Ya Wadhami wa Chama Hicho Yatoa Onyo Kali Kwa Mabenki Hapa Nchini
Wakati
taariza zinazomtuhumu Profesa Ibrahim Lipumba kufungua akaunti benki
kwa lengo la kuingiziwa fedha za ruzuku ya Chama cha Wananchi (CUF)
kinyume cha sheria kwa ajili ya kukivuruga chama hicho zikienea.
Bodi
ya Wadhamini ya CUF imetoa onyo pamoja na kuwatahadharisha watu
wanaotumika kusaini nyaraka feki kwa lengo la kufungua akaunti hizo, pia
imezitahadharisha benki zote nchini kutofungua akaunti yoyote kwa jina
la CUF pasipo kupata muhtasari wa bodi halali ya chama hicho.
Katika
hatua nyengine, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julias Mtatiro
amefafanua kuwa wenye mamkaka halali ya kufungua akaunti ya chama hicho
ni Bodi yake ya wadhamini pamoja na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif
Sharif Hamadi.
“Tunatoa
onyo, kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kwamba tumeshafungua
shauri na utaratibu wa kisheria umeshaanza kuchukua mkondo wake,
tumesikitika kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,
kinyume cha sheria namba tano 1992 ya vyama vya siasa na kinyume cha
katiba, Msajili kwa mara ya kwanza anaziandikia benki zilizosajiliwa na
BOT akizitaka kumfungulia akaunti Lipumba za kuwekea fedha,” amesema Mtatiro.
Mtatiro amedai kuwa ”Benki
itakayomfungulia akaunti Lipumba ni makosa makubwa. Sababu huwezi
fungua akaunti ya taasisi au chama bila ya bodi yake ya wadhamini kukaa
kikao na kuandaa muhtasari kwa ajili ya kupeleka benki ili kufungua
akaunti.Lipumba na watu wake wameandaa nyaraka feki pamoja na barua ya
msajili kutaka kufungua akaunti. Tunajua amepeleka katika benki
mbalimbali,
“NMB
ilikataa sasa wanapeleka benki ya Exim na ilishapewa taarifa kuwa uhuni
huu haukubaliki na masuala ya fedha yako chini ya katibu mkuu kwa
mujibu wa katiba ya cuf,” amesema.
Sambamba
na onyo lililotolewa na bodi hiyo, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Dar es Salaam leo imekubali maombi yake ya kufungua shauri la kuitaka
mahakama hiyo kutoa amri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji
Francis Mutungi ya kutoendesha shughuli zake za usimamizi wa vyama vya
siasa kinyume cha sheria, pamoja na kutengua barua yake inayomtambua
profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha maombi hayo, Wakili Juma
Nassoro amesema kuwa Jaji wa mahakama hiyo Munisi, amekubali maombi yao
na kwamba jopo la mawakili wa CUF linatarajia kuwasilisha maombi rasmi
wiki hii.
“Jaji
Munisi baada ya kutusikiliza vifungu vya sheria tulivyotumia, Mahakama
imekubali ombi letu ili tuweze kufungua maombi ya kuomba mahakama itamke
kufuta barua ya msajili inayomtambua Lipumba kama mwenyekiti halali wa
CUF. Pia Itoe zuio rasmi kwa msajili kutofanya shughuli zake nje ya
utaratibu ambao amepewa chini ya sheria ya vyama vya siasa,” amesema Nassoro.
Amesema baada ya mahakama kuridhia maombi yao, iliwataka kuwasilisha maombi rasmi ndani ya siku14 kuanzia leo.
“Tumeambiwa
tuwasilishe maombi ndani ya siku 14, lakini tutayawasilisha ndani ya
siku Saba na tutaiomba mahakakama iyasikilize kwa Hati ya dharula ili
shughuli za chama ziendelee,” amesema.
Monday, October 10, 2016
Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wa Nchi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam 10th Oktoba 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne
wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.
"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika baadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi" amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.
Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.
"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.
"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika baadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi" amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.
Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.
"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
Monday, October 10, 2016
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Yatupiwa Lawama Kwa Kuchelewa Kutoa Majina ya Wanufaika wa Mikopo
Wakati
vyuo vikuu vikikaribia kufunguliwa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) imelaumiwa kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika
huku yenyewe ikisema itahakikisha majina yanatolewa sanjali na tarehe za
vyuo kufunguliwa.
Pia, HESLB imesema miongoni mwa vipaumbele vitakavyozingatiwa kwenye utoaji wa mikopo katika mwaka wa masomo 2016/2017 ni kwa wanafunzi wenye mahitaji makubwa, waliotoka kwenye kaya masikini, waliosoma shule za kata na waliotoka vijijini.
Kauli
hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kutupiwa lawama kwa kuchelewa kutoa
majina ya wanufaika wa mikopo kabla hawajaripoti vyuoni, hasa wanafunzi
wa mwaka wa kwanza.
Mkurugenzi
wa mtandao wa haki za wanafunzi (TSNP), Shitindi Venance alisema hadi
sasa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa
kwanza wa masomo 2016/2017, ambao wameomba mkopo bado hawajui ni kiasi
gani wamepewa.
Malalamiko
ya Shitindi yamerejea kilichotokea mwaka jana baada ya wanafunzi
kuripoti vyuoni, lakini majina yalipotolewa na bodi hiyo baadhi yao
hawakuwa wanu- faika hali iliyosababisha usumbufu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema miongozo ya utoaji wa
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni tofauti na mwaka
jana.
“Utaratibu
wa mwaka huu ni tofauti kwa kuzingatia wanafunzi wanaoanza masomo na
wale wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali,” alisema Badru.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kuwa majina ya wanufaika wa mikopo yataanza kutolewa
kwa kuzingatia tarehe ambayo chuo husika kinafunguliwa.
“Kila
chuo kinafunguliwa kwa mujibu wa tarehe iliyopangwa kwa hiyo na sisi
tunatoa majina kuendana na utaratibu wa chuo husika,” alisema.
Hata
hivyo, Badru alisema uta- ratibu wa kupanga viwango vya mikopo kwa
wanafunzi na kisha kutoa orodha ya majina ya wanufaika haihusishi bodi
ya mikopo peke yake.
Alisema
kabla ya kuidhinisha majina ya wanufaika na mikopo, lazima Tume ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TCU) iwe imeshatoa orodha ya majina wa wanafunzi ambao
imewadahili kwa kuzingatia vigezo vyao, halafu majina hayo yatumwe
vyuoni.
Alisema mzunguko wote huo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu ndiyo maana huchukua muda.
Monday, October 10, 2016
Lipumba Afungua Akaunti Mpya ya Ruzuku CUF.......Benki ya NMB Yalaumiwa kwa Kuvujisha Siri
Siri
kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la
chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka
kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala.
Prof.
Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa
Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.
Abdul
Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na
Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa
limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima,
akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya
Prof. Lipumba.
“Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?” alihoji Kambaya.
Hata hivyo, alipotafutwa
Kambaya ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na
kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa,
hakuwa tayari kufafanua akidai kuwa si wakati muafaka.
“Tutaeleza
mambo hayo kwa wakati muafaka, kama kuna jambo tunakuwa accused
(tunatuhumiwa), iulizeni ofisi ya msajili au benki husika, wao wana
taarifa kamili,” alisema.
Ofisi
ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza imenukuliwa na
vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Prof. Lipumba kwa
benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo amedai kuwa
ofisi ya msajili haijui matumizi ya akaunti hiyo.
Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yanayodaiwa ni kuchukua ruzuku za chama hicho zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Alhamis ya tarehe 06 Septemba mwaka huu.
Uongozi
wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi
na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala
hilo leo Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.
Monday, October 10, 2016
Spika wa Bunge Job Ndugai afumua Kamati ya Bunge na Kuisuka Upya
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya
mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi,
akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na
Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na
sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda
Kamati za Bunge kadri anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya
yamelenga katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
“Kanuni
ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016
inampa Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati
mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kuongeza, kubadilisha
au hata kupunguza idadi ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.
Mabadiliko
hayo yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe
wote wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua
viongozi wa kamati hiyo.
Monday, October 10, 2016
Mkutano wa ACT- Wazalendo Watoa Maazimio Mazito Dar
Chama cha ACT-
Wazalendo kimemuomba Rais John Magufuli kuunda timu ya wataalamu kupitia
upya rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba na kuitisha mkutano mkuu
wa kikatiba ili kuipitisha.
Chama hicho kilisema mchakato wa kura za maoni uanze upya ili kupata Katiba Mpya.
Chama hicho kilisema mchakato wa kura za maoni uanze upya ili kupata Katiba Mpya.
Hayo ni
miongoni mwa maazimio matatu yaliyotolewa na chama hicho kwenye
mkutano wa siku moja wa kidemokrasia.
Akisoma maazimio hayo, Ofisa
Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis alisema, “chama kimeazimia
mchakato wa kuandika Katiba Mpya uanze kwa kufanya marekebisho ya sheria
ya kura ya maoni na Sheria ya mchakato wa Katiba.”
Alisema, iwapo
Serikali itaamua kwenda na Katiba Inayopendekezwa iliyopo sasa chama
hicho kitaipinga kwa kufanya kampeni ya hapana kwenye kura ya maoni.
Alisema wakati mchakato wa Katiba ukiwa umesimama, Baraza la Wawakilishi
Zanzibar limepitisha sheria ya kutafuta mafuta na gesi kinyume na matakwa ya
Katiba ya Muungano ambayo inatambua mafuta na gesi kuwa ni masuala ya
muungano.
“Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeshauri kuwa chama
kimwelekeze mbunge wake kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kufanya
mabadiliko, kwa kuondoa mafuta na gesi kama jambo la muungano ili
kuiwezesha Zanzibar kutafuta mafuta na gesi asilia bila vikwazo,”
alisema.
Khamis alisema chama hicho kimeazimia kufanya maadhimisho ya
miaka 50 ya Azimio la Arusha Februari, 2017.
“Katika maadhimisho hayo
chama kifanye mkutano mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha na kutanguliwa
na Halmashauri Kuu ya chama kwenye ukumbi uleule ambao Tanu ilifanya na
kuzaa Azimio la Arusha mwaka 1967,” alisema.
Ofisa huyo alisema katika
maadhimisho hayo chama kimeshauriwa kuwa wataalamu wa ndani na nje
waalikwe kujadili mafanikio na changamoto za Azimio la Arusha katika
miaka 25 iliyopita.
Pia, wataalamu watajadili madhara ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 huko Zanzibar.
Pia, wataalamu watajadili madhara ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 huko Zanzibar.
habari za leooo
Reviewed by RICH VOICE
on
Oktoba 10, 2016
Rating:
Hakuna maoni